Kwanini Marekani wana economic cooperation with China? Dunia ina unafiki sana

Kwanini Marekani wana economic cooperation with China? Dunia ina unafiki sana

Moja ya jambo limeniacha na peace of mind ni kuwa neutral sana kwenye siasa za Tanzania zisizoeleweka.

Nimeona mahali JF mleta mada ameleta document ya Desemba 2025 ambapo bunge la senate la Marekani limepanga kupitisha muswada unaagiza kutathmini ushirikiano wa Tanzania na China kijeshi, kiuchumi na kisiasa.

Wanasubiri tu Trump abariki muswada huo kwa kumwaga wino Tanzania ishughulikiwe.

Kwa miongo kadhaa media na wachambuzi wa Magharibi wakiongozwa na Marekani wamekuwa wakiiaminisha dunia kuwa China haina Demokrasia, uhuru wa maoni, wala uhuru wa vyombo vya habari hakuna.

Na kama haitoshi wanasema kuwa Serikali ya China huwa inawanyanyasa, kuwatesa na kuwaua jamii ya Waislamu iliyopo Xinjiang.

Mbona hao Marekani bado wanafanya biashara za billions of dollars na China?

Nchi ambayo haifuati Demokrasia ya Magharibi na wanadai inaua Waislamu Xinjiang?

Wamuondoe Xi na chama cha CPC basi tuone au waondoe economic cooperation na China.

Lakini ndio kwanza wiki 2 zilizopita Trump alienda kutafuta deals China. Dunia ina unafiki sana, inataka akili sana ku-deal na Marekani na nchi za Magharibi.

By the way hapa ni mahali Watanzania waondoe uCCM, uCHADEMA, uhanarakati, na Pro-U.S mentality panataka akili sana. Kwa sehemu muswada ulisema:
​

Directs the Administration to evaluate the extent of the People’s Republic of China’s military, economic and political engagement in Tanzania, including cooperation that could undermine democratic institutions and U.S. interests in the region.
​
Hizo interests za Marekani ni zipi?​
Mambo mawili au zaidi yanaweza kuwa kweli kwa pamoja. China haina demokrasia(achana na ujinga wa kusema demokrasia ya Magharibi, hakuna demokrasia ya Mashariki, Kusini au Kaskazini), China haina uhuru wa maono wala vyombo huru vya habari , ni kweli pia China inawalazimisha Waislamu wa China kufuata taratibu za kichina zaidi kuliko za Kiarabu. Hizi zote ni fact sio masuala la kubishaniwa. Ni kweli pia Marekani inafanya biashara na kila taifa duniani hata maadui zake kama Cuba na Russia mpaka sasa hivi.

Ni kweli pia serikali ya Marekani na serikali nyingine za West zina contradictions kubwa katika sera na utendaji wao wa geopolitics, ni kweli pia serikali ya CCM ya Tanzania inatawala kidikteta bila ridhaa ya raia wake, inahusika kupoteza watu na haiko competent kuletea maendeleo.

Zaidi ni kwamba binadamu wote wana contradictions zao, sio Wamarekani tu bali hata China wenyewe kwao mfano wananyonga mafisadi na wala rushwa ila Africa kampuni za kichina ni halali kutoa rushwa na kushirikiana na viongozi mafisadi.
 
Moja ya jambo limeniacha na peace of mind ni kuwa neutral sana kwenye siasa za Tanzania zisizoeleweka.

Nimeona mahali JF mleta mada ameleta document ya Desemba 2025 ambapo bunge la senate la Marekani limepanga kupitisha muswada unaagiza kutathmini ushirikiano wa Tanzania na China kijeshi, kiuchumi na kisiasa.

Wanasubiri tu Trump abariki muswada huo kwa kumwaga wino Tanzania ishughulikiwe.

Kwa miongo kadhaa media na wachambuzi wa Magharibi wakiongozwa na Marekani wamekuwa wakiiaminisha dunia kuwa China haina Demokrasia, uhuru wa maoni, wala uhuru wa vyombo vya habari hakuna.

Na kama haitoshi wanasema kuwa Serikali ya China huwa inawanyanyasa, kuwatesa na kuwaua jamii ya Waislamu iliyopo Xinjiang.

Mbona hao Marekani bado wanafanya biashara za billions of dollars na China?

Nchi ambayo haifuati Demokrasia ya Magharibi na wanadai inaua Waislamu Xinjiang?

Wamuondoe Xi na chama cha CPC basi tuone au waondoe economic cooperation na China.

Lakini ndio kwanza wiki 2 zilizopita Trump alienda kutafuta deals China. Dunia ina unafiki sana, inataka akili sana ku-deal na Marekani na nchi za Magharibi.

By the way hapa ni mahali Watanzania waondoe uCCM, uCHADEMA, uhanarakati, na Pro-U.S mentality panataka akili sana. Kwa sehemu muswada ulisema:
​

Directs the Administration to evaluate the extent of the People’s Republic of China’s military, economic and political engagement in Tanzania, including cooperation that could undermine democratic institutions and U.S. interests in the region.
​
Hizo interests za Marekani ni zipi?​
Xi
China imewahi kuwekewa vikwazo vingi sana, lbda wewe hujafuatilia tu. Ila tu China vile vile wana leverage. Halafu wanayo 'absorption" capacity kubwa kuliko viinchi kama Tanzania. Absorption nina maana kuwa China ni kubwa, na liuchumi wake ni kubwa, unaweza uka-sacrifice sehemu moja ukashangaa inazidi kupumua kwa nguvu tu. Sawa sawa kwenye ndondi, heavy weight na light weight wakipigana, light weight utapiga heavy weight ngumi kumi lakini atahimili. Light weight ngumi moja tu ya heavy weight anaweza kuzilai.

Leverage- tunahitajiana na tunaongea. Vikao vinavyofanywa kati ya China na Marekani ni vingi mno kama siyo kila wiki basi kila mwezi Na ukisikia wanavyoongea ni kabisa wanaelewana, constructive argument. Kuna wakati wanakaruzana lakini kuna heshima.

China amewahi kuwekewa Vikwazo kwenye mauaji ya Tianamen 1989, amewahi kuwekewa 2019 kuhusu Hong Kong, kwani hamuoni? Lakini Mchina anasimama anaanza kubisha na kujadili na mchina anaogopa sana uchumi wake usihathirike kwa sababu bila ya kuuza nje Ulaya au Marekani hawewezi kutoboa.

Kwa sasa manufacturing duniani wanategemea world factory yaani China, na consumer mkubwa Marekani na Ulaya.

Kuhusu suala la Waislam wa Xinjiang Province wachina walifanya kazi kubwa sana kuongea na UN, USA, Ulaya na kote huko, mara ya Mwisho unakumbuka Mkuu wa UN human righ yule mama wa Chile aliachia ngazi kwa sababu ya suala hili. Baada ya kuzulu China na kuangalia kule Xinnjiang alikataa kutoa report. Ikazikwa akaachia ngazi.

Watu wanaongea, siyo hao vichaa wenu, ati "Who are you" anapigiwa makofi anaona sifa.
 
Historia yetu sisi haiwezi kutengewa na demokrasia, Nyerere aliipata hii nchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia uliosamimwa na Wakoloni, Alivikuta vyama vingi akavufuta na baadaye wakavirudisha tena, makubaliano yetu sisi ni uongozi up upatikane kupitia uchaguzi huru na haki, China na Gulf states za Uarabuni wao hawajawahi kuwa na demokrasia, labda pia hawahiitaji lakini sisi tunahiitaji kulingana na historia yetu.

Ni vigumu sana kuwa na udikteta kwenye Taifa lenye Wakristo wengi.
Unaijua vizuri Historia ya Tanzania? Kabla ya kuja kwa wakoloni jamii za kale zilikuwana mfumo gani wa kiutawala?
 
Mahusiano ni kwamba inaonekana China inapata kirahisi deals za kuvuna rasilimali Africa kwa sababu serikali ya China haidai uwajibikaji wowote kutoka kwa serikali za Africa kuhusiana na raia. Yani kama kuna madini maalumu kijiji fulani serikali ya Africa hata ikiua kijiji kizima ili kuwapa kampuni ya kichina kuchimba serikali ya China haitahoji au kusema chochote na pia hakuna mwanaharakati wa kichina wa kusema chochote tofauti na ilivyo kwa US.
China haiendi Afrika kama mlezi wa kisiasa bali kama mshirika wa biashara

Sera yake ya kutokuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine inamaanisha inaheshimu mamlaka ya serikali za Afrika kufanya maamuzi yao wenyewe

Ikiwa kuna ukandamizaji au ufisadi, jukumu la kwanza ni la viongozi wa nchi husika, si la China

Kulaumu China kwa kila tatizo la Afrika ni kuondoa uwajibikaji kwa wale wanaotawala Afrika

China inanunua rasilimali haiendeshi serikali za Afrika. Tatizo la viongozi wabovu ni la Afrika, si la China
 
China haina demokrasia(achana na ujinga wa kusema demokrasia ya Magharibi, hakuna demokrasia ya Mashariki, Kusini au Kaskazini)
Inategemea unamaanisha demokrasia kwa kipimo gani

China haina demokrasia ya vyama vingi na uchaguzi wa ushindani wa kitaifa kama ilivyo kwenye mfumo wa Magharibi.

China ina aina yake ya demokrasia ya mashauriano ambapo kuna uchaguzi wa ngazi za chini (kijiji na mtaa)

Maamuzi hufanywa kupitia mfumo wa chama na taasisi za serikali na maoni ya wananchi hupokelewa kupitia vyombo vya chama, mashauriano na tafiti za kijamii

Kwa tafsiri ya kimataifa ya demokrasia (vyama vingi + uchaguzi huru wa kitaifa), China si demokrasia

Lakini kwa tafsiri yake yenyewe, China ina aina yake ya demokrasia inayolenga utulivu na maendeleo badala ya ushindani wa vyama

Kama demokrasia ya Magharibi ya ushindani wa vyama ndiyo kipimo pekee cha mafanikio, basi kwa nini China imepiga hatua kubwa za maendeleo kuliko nchi nyingi zenye uchaguzi wa vyama vingi?
​
 
China haina uhuru wa maono wala vyombo huru vya habari
Kuna vyombo vingi vya habari nchini China vinavyofanya kazi, na vinaweza kuripoti mambo ya kijamii, uchumi, ajali, rushwa za chini, na masuala ya huduma za umma

China inaona jukumu la vyombo vya habari si tu kuikosoa serikali, bali pia kulinda utulivu wa jamii na maendeleo ya nchi
 
ni kweli pia China inawalazimisha Waislamu wa China kufuata taratibu za kichina zaidi kuliko za Kiarabu.
Waislamu wananyanyaswaje nchini China? Hizo ni propaganda za media za Magharibi.

China ina Waislamu milioni 30 na wanaishi peacefully.

Kuna misikiti zaidi ya 30,000 nchini China.

Na Xinjiang pekee ina misikiti 20,000 idadi ya misikiti per capita katika jiji la Xinjiang ni kubwa kuliko nchi nyingi za kiislamu.

Na Waislamu wa Xinjiang wanapewa nafasi katika serikali ya China, wanaajiriwa, na wapo ambao ni celebs

Kwa nini media za Magharibi hazizingatii manyanyaso na mauaji ya kweli dhidi ya Waislamu yanayofanywa na Israel ikisaidiwa na Marekani Palestina na sehemu zingine za Middle East?
​
 
ila Africa kampuni za kichina ni halali kutoa rushwa na kushirikiana na viongozi mafisadi.
Si kweli

Mbona kampuni za Magharibi zinapewa mikataba ya utafunaji wa rasilimali za Afrika huku serikali za Afrika zikiambulia asilimia ndogo ya mapato
?
 
[][/][]Hizo interests za Marekani ni zipi?[/]
Ni kwamba hujui chochote, ndiyo maana unajiandikia hovyo hovyo tu!

Haya ndiyo matatizo ya elimu yetu siku hizi.

Na huyu unaweza kukuta ni mwalimu huko mashuleni, na yeye anafundisha vijana mambo asiyokuwa nayo ufahamu wowote.

Ni kujipigia tu mradi liende!
Uliambiwa na nani kuwa "Marekani na China ni "partners". Unajuwa maana ya neno hilo?

Lakini la muhimu kabisa kwangu kufuatana na maandishi yako, kinachokupa kulalamika hasa ni nini: kwa huo mswada wa hao maseneta?

Wewe unafaidika na uovu wa Samia Suluhu Hassan anaofanya hapa Tanzania?
Hili pekee zaidi ya hayo mengine yote uliyohoji huku ukiwa hujui chochote juu yake ndilo la muhimu kwa waTanzania.

Unajifanya kuandika juu ya vitu usivyovifahamu ili kutetea uovu wa Samia Tanzania?
 
Ni kwamba hujui chochote, ndiyo maana unajiandikia hovyo hovyo tu!

Haya ndiyo matatizo ya elimu yetu siku hizi.

Na huyu unaweza kukuta ni mwalimu huko mashuleni, na yeye anafundisha vijana mambo asiyokuwa nayo ufahamu wowote.

Ni kujipigia tu mradi liende!
🚮 🚮 🚮
 
Si kweli

Mbona kampuni za Magharibi zinapewa mikataba ya ytafunaji wa rasilimali za Afrika huku serikali za Afrika zikiambulia asilimia ndogo ya mapato
?
Kwa hiyo huo mswada wa maseneta hao wa Marekani hautufai kwa sababu ya hiyo mikataba unayoizungumzia wewe?
Samia aendelee kuua waTanzania kwa sababu Marekani hufanya mikataba isiyofaa kwa nchi za kiafrika?
 
China amewahi kuwekewa Vikwazo kwenye mauaji ya Tianamen 1989, amewahi kuwekewa 2019 kuhusu Hong Kong, kwani hamuoni? Lakini Mchina anasimama anaanza kubisha na kujadili na mchina anaogopa sana uchumi wake usihathirike kwa sababu bila ya kuuza nje Ulaya au Marekani hawewezi kutoboa.
Achana na propaganda za Magharibi, nchi za Magharibi furaha yao ni kuona China haifanikiwi kiuchumi na kijamii

Tukio la Tiananmen lilikuwa nyuma ya CIA na mashirika ya Marekani yanayodai ya kidemokrasia kutaka kuihujumu China

Walianza kwa kuwashinikiza wanafunzi wafanye maandamano na kuigomea serikali yao

Na hii ni mbinu ambayo Marekani imekuwa ikiitumia kwa miaka mingi kuchochea maandamano, color revolution na kisha kupandikiza viongozi vibaraka.

Jambo la kushukuru CPC ilisimama imara dhidi ya vitendo hivyo na hakuna ukandamizaji wowote uliotokea

Media za Magharibi huwa zinapotosha kuwa kuna mauaji ya wanafunzi yalitokea siku hiyo na hii ni kwa sababu walifeli jaribio hilo

Ndio maana sikuzote China imekuwa ikisema tukio hilo ni tukio la machafuko yaliyodhibitiwa ili kulinda utulivu wa taifa, si kama tukio la ukandamizaji wa demokrasia

Kilichotokea Tiananmen mwaka 1989 ndicho kilitaka kitokeee Hong Kong 2019, script ni ileile Marekani ilitaka kuwatumia wanafunzi wakiongozwa na Joshua Wong kuleta machafuko

Ila walidhihitiwa leo Hong Kong iko salama
 
🚮 🚮 🚮
Sitanii. Ni kwamba hujui kitu katika hayo uliyoyaandika hapo.

Pengine ni njia to ya kupitia ili kutetea uovu unaofanywa na Samia Tanzania.
Maana sasa ni wazi kazi yenu ni kupindisha tu kila jambo, kama anavyofanya Kombo.

Mnayo kazi ngumu sana.
 
Taja sehemu nilipotetea
 
Achana na propaganda za Magharibi, nchi za Magharibi furaha yao ni kuona China haifanikiwi kiuchumi na kijamii

Tukio la Tiananmen lilikuwa nyuma ya CIA na mashirika ya Marekani yanayodai ya kidemokrasia kutaka kuihujumu China

Walianza kwa kuwashinikiza wanafunzi wafanye maandamano na kuigomea serikali yao

Na hii ni mbinu ambayo Marekani imekuwa ikiitumia kwa miaka mingi kuchochea maandamano, color revolution na kisha kupandikiza viongozi vibaraka.

Jambo la kushukuru CPC ilisimama imara dhidi ya vitendo hivyo na hakuna ukandamizaji wowote uliotokea

Media za Magharibi huwa zinapotosha kuwa kuna mauaji ya wanafunzi yalitokea siku hiyo na hii ni kwa sababu walifeli jaribio hilo

Ndio maana sikuzote China imekuwa ikisema tukio hilo ni tukio la machafuko yaliyodhibitiwa ili kulinda utulivu wa taifa, si kama tukio la ukandamizaji wa demokrasia

Kilichotokea Tiananmen mwaka 1989 ndicho kilitaka kitokeee Hong Kong 2019, script ni ileile Marekani ilitaka kuwatumia wanafunzi wakiongozwa na Joshua Wong kuleta machafuko

Ila walidhihitiwa leo Hong Kong iko salama
Kwa hiyo hizi ni habari mpya kwako ambazo unataka kuwashirikisha waTanzania wazijue; na wakijuwa wakubali kuwa hao wamarekani kupitia kwa maseneta wao wanatumia njia hizo hizo kuvuruga hali ya Tanzania chini ya Samia?
 
Kuhusu suala la Waislam wa Xinjiang Province wachina walifanya kazi kubwa sana kuongea na UN, USA, Ulaya na kote huko, mara ya Mwisho unakumbuka Mkuu wa UN human righ yule mama wa Chile aliachia ngazi kwa sababu ya suala hili. Baada ya kuzulu China na kuangalia kule Xinnjiang alikataa kutoa report. Ikazikwa akaachia ngazi.
Suala la Xinjiang ni upotoshaji, China ilishawaalika delegates kutoka U.N na nchi za Kiislamu waende kufanya uchunguzi huru kama kweli madai ya kuwa Waislamu wa Xinjiang wanaonewa

Ziara hizo zote hasikuonyesha kuwa kuna ukandamizaji. Tatizo kubwa ni kwamba watu mmelishwa propaganda na media za Magharibi

Suala la Xinjiang sio suala la kidini kama wengi mnavyodhani ni suala la kigeopolitcs na ushindani wa kiuchumi

Xinjiang kwa sasa imekuwa mojawapo ya maeneo ya utalii maarufu zaidi duniani, ilipokea watalii wapatao milioni 265 mwaka jana. Wakiwa huko hawajawahi kusema kuwa kuna unyanyasaji

Kwa hiyo Marekani ina uchungu sana na Waislamu wanaoishi kwa amani Xinjiang kuliko wale wanaowaua M.E kama Gaza wakishirikiana na Israel? Tumia akili siku nyingine

20260530_061853.jpg

20260530_062746.jpg
 
Back
Top Bottom