Kwanini Marekani wana economic cooperation with China? Dunia ina unafiki sana

Tiananmen square incidence ilikuwa 1989, kwa nini baada ya hapo Marekani na nchi za Magharibi waliendelea kufanya FDI China?
 
Chawa wengi humu ndani wataishia kukutukana hutapewa jibu la maana.

Hao wamarekani siku zote wanaangalia maslahi yao yapo vipi, hizi habari za demokrasia ni geresha tu za kuwapatia wanasiasa wao hoja za kuwajibu waandishi wao wa habari.
 
Kwa hiyo viongozi ndio wanaocooperate kiuchumi na China?
Kwani lazima hao wauaji ndio wawe viongozi??

Unaniuliza kama vile mimi ndio Marekani.

Una watawala ambao wana MAKOVU yenye USAHA, Marekani anatumia hayo MAKOVU kuwatenga, kama wewe unaona kwako hayo makovu hayana shida, wao hawayataki.

Sasa kama.m wewe unaona NCHI=SAMIA na Genge lake (Vimeungana na havitofautiki), hilo siyo la Marekani.

Ni tatizo lako.
 
Tiananmen square incidence ilikuwa 1989, kwa nini baada ya hapo Marekani na nchi za Magharibi waliendelea kufanya FDI China?
Wachina wanaichukuliaje nchi yao?

Hata Nyerere hakuwapa Wazungu wanachotaka, ila walimheshimu kwasababu aliheshimiwa na watu wake. Vita ya Kagera kila mtu alishiriki.

Leo TZ, watawala wako busy kuteka watu na kuua mpaka wajawazito na watoto, kupora haki kupitia mahakama, WIZI, UFISADI.

Hivi unadhani leo nchi ikivamiwa, labda UVCCM na ABDUL ndio wataenda kupigana.
 
Hakuna demokrasia bila kuwa na mfumo wa vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mihimili ya dola, mahakama huru na uchaguzi huru.

Mfumo wa mashauriano uko hata Saudi Arabia, Qatar, Oman, Kuwait na UAE ambapo wafalme wanafanya maamuzi kwa kushauriana na Baraza la majlis ila huo sio mfumo wa kidemokrasia.

Pia hakuna demokrasia ya Kichina au ya tafsiri ya Kichina, hakuna demokrasia ya tafsiri ya Kitanzania. Demokrasia ni moja tu na tafsiri yake ni moja kote duniani na demokrasia ni zao la Magharibi. Kusema kuna demokrasia ya Kichina ni sawa na kusema Ukristo wa China au Ubudha wa magharibi.

China ina mfumo wake wa kujitawala usio wa demokrasia, kuhusu huo mfumo kuleta au kutoleta maendeleo ni mjadala mwingine.
 
Umeuelewa huo mswada?? Kitu cha Kwanza cha US ni kuhusu Tanzania ni kuundermine democratic institutions, sasa wewe unakubaliana nao au unapingana nao hapo ndio nitakuja kwenye Hilo jingine
Mleta mada sio mgeni hapa jamvini kwa namna alivyo shabiki wa China.
 
Demokrasia siyo lazima vyama vingi.

Demokrasia lazima iambatane na UWAJIBIKAJI KWA WATU, WATU KUCHAGUANA WENYEWE, MSINGI WA HAKI na MERITOCRACY
 
Mpaka sasa swali langu halijajibiwa, inasemwa kuwa Tanzania inaundermine demokrasia

Basi kwa nini Marekani iingilie economic cooperation kati ya Tanzania na China?

Kuna uhusiano gani kati ya mambo hayo mawili?
Kwa sababu China ndio mnufaika mkubwa wa utawala usio wa kidemokrasia wa Tanzania.
 
Kama ambavyo China haingilii mataifa mengine wakati watawala wa nchi hizo wanaua watu wake, ndivyo hivyo hivyo hawataingilia matatizo yako, siku MABEBERU wakianza kukushona.
 
Kwa sababu China ndio mnufaika mkubwa wa utawala usio wa kidemokrasia wa Tanzania.
Wao Marekani hawajawekeza Tanzania?

Mbona hapo Tanzania wapo na mnafanya nao economic cooperation na wananufaika

Basi Marekani ilitakiwa iweke mfano kwa kuwa mstari wa mbele kuondoa ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania
 
Swali: Ni lazima mataifa yote duniani yafuate mfumo wa Demokrasia ya Magharibi?

Kila taifa lina haki ya kufuata mfumo wake wa kisiasa na utawala

Mwisho wa siku kinachoamua ni mfumo upi unaleta maendeleo, amani na prosperity

China wamejipata kwenye socialism with Chinese characteristics
 
Demokrasia yetu ikoje?

Mbona unakwepa UKWELI?

Utaratibu wetu wenyewe, tumekubaliana vipi?

Tunaheshimu utaratibu huo?

Huu upumbavu wa kushindwa kutoa majibu, na kutafuta watu wa kulaumu haujawahi kutatua tatizo lolote
 
Mfumo wetu wa kisiasa na utawala Tanzania ni upi?
 
Sio kila anayetekwa serikali inahusika. Kijana kakatwa kichwa mwezi uliopita, serikali inahusika?.

Propaganda zinaichafua sana nchi hii kwa pesa zinazolipwa kwa waandishi wa habari, wanafanya ufisadi halafu kinafiki wanauandika kwenye vyombo vyao vya habari.
 
Sio kila anayetekwa serikali inahusika. Kijana kakatwa kichwa mwezi uliopita, serikali inahusika?.
Kama hawahusiki, wanafanya nini sasa?

Kama kuna genge linakuja nchini linateka watu na kuwaua, maana yake wanaosema serikali ya CCM ni zero wako.m SAHIHI kwa 600%.
Propaganda zinaichafua sana nchi hii kwa pesa zinazolipwa kwa waandishi wa habari, wanafanya ufisadi halafu kinafiki wanauandika kwenye vyombo vyao vya habari.
Propaganda wana fanya CCM ndio maana haziendi.mbali.

Ukweli unaishi MILELE.

Waandishi gani wa Habari, hao wa TZ ambao Mhariri mkuu ni TCRA na BASHITE???
 
Mnajazana ujinga humu mitandani hata mnapokwenda kufanya vurugu huko mtaani halafu mkapigwa shaba vifo vyenu vinakuwa na msingi wa ujinga mwingi.

Hakuna genge lolote linalotoka nje ya nchi kuja kufanya uharamia hapa Tanzania. Hakuna huo ushahidi kwamba wanajeshi walituliza ghasia tarehe 29 October ni raia wa kigeni, vijana wa hapa hapa bongo walimaliza ule upuuzi.

Watu wanauana wao wenyewe kwa sababu zao wenyewe unataka serikali iziue wasiuane?. Kivipi wakati kuuana kwao hutokana na sababu zao binafsi?
 
Mnajazana ujinga humu mitandani hata mnapokwenda kufanya vurugu huko mtaani halafu mkapigwa shaba vifo vyenu vinakuwa na msingi wa ujinga mwingi.
Bahati nzuri wote mnakiri kuwa nyie ndio MMEUA watu, mpaka wanawake wenye MIMBA.

Tutajua mtokeo yake siku chache zijqzo.
Hakuna genge lolote linalotoka nje ya nchi kuja kufanya uharamia hapa Tanzania. Hakuna huo ushahidi kwamba wanajeshi walituliza ghasia tarehe 29 October ni raia wa kigeni, vijana wa hapa hapa bongo walimaliza ule upuuzi.
Ushahidi huwezi kuutoa wewe. Itafamika tu, hata miaka 50 ijayo.
Watu wanauana wao wenyewe kwa sababu zao wenyewe unataka serikali iziue wasiuane?. Kivipi wakati kuuana kwao hutokana na sababu zao binafsi?
Huu ni uthibitiaho mwingine, tuna zigo la mavi ya nguruwe Ikulu
 
Kulalamika ni jadi na asili ya mtanzania, akipewa yeye nafasi vichekesho vitupu.

Hao waliouliwa wangeingia ikulu tungekuwa tunajiliza kwa kina ICC kuhusiana na vifo vyao?.

Mlitaka kufanya mapinduzi ya kihuni mkadhibitiwa kihuni pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…