Kweli.
Nimefika Oysterbay pale Karume na Haile Selassie nikakuta barabara zina mashimo kichizi. Mara Bakhressa kachukua sehemu ya Shule kwa Mchambawima kajenga nyumba pale.
OYsterbay vurugu tupu.
Mimi tangu mshua aanze kuwa anakuja US yearly nimekosa appetite kabisa ya kurudi hata likizo.
Nikisema miaka niliyopotea ni aibu.
It’s good to go back.
I do it at least twice a year.
Just got back a couple weeks ago.
Stayed there for 2 1/2 months.
Ukiacha familia, kuna mengi ya kufanya.
Mfano, safari hii nilienda mpaka Serengeti.
Mbuga hii ya Serengeti iko kwenye mikoa miwili: Mara na Simiyu.
Miaka yote hii sikuwahi kabisa kuwaza kwenda huko.
Ila safari hii kuna mtu akazungumzia kwenda Serengeti. Nikaona ni wazo zuri sana.
Kutoka Simiyu mpaka hapo mbugani wala haichukui muda kivile. Ni takriban lisaa limoja tu.
Unatoka Bariadi mjini unapitia Lamadi. Kutoka Lamadi mpaka Serengeti ni dakika chache tu.
Akilini mwangu sikuwahi kabisa kuwaza kwamba Serengeti si mbali kabisa na nyumbani. Kwamba unaweza kwenda leo na kurudi leo leo.
Next time nikienda tena Tanzania, nitaenda tena Serengeti maana mbuga ni kubwa. Sikuweza kuiona yote.
Nawe unaweza kutumia vivutio kama hivyo vikawa kama motisha ya wewe kurudi mara kwa mara.
Kama unakuwa hujaenda kwa muda mrefu, ni lazima uta experience culture shock.
Hicho ni kitu ambacho mimi sina kutokana na frequency yangu ya kwenda.