Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Sio kweli,katika sehemu ambazo zimepoteza ushawishi ni masaki.masaki kuna jina kubwa lakini uhalisia ni tofauti.majengo ya kizamanu na hayashtui.
Lakini mbezi bado ni ya moto,ina jina linaendana na uhalisia,kumetulia na kumekaa kishua.

Japo kwa sasa,sehemu ambayo inakoroma ni mbweni,kule kama una ugonjwa wa moyo sikushauri ufike.
😂
 
Habari wana jamii forum?

Kuanzia miaka ya elfu mbili kushuka chini, eneo la Mbezi beach lilikuwa ni kati ya maeneo machache ya jiji la Dar es salaam ambayo yalikuwa na umaarufu mkubwa kama vile ilivyokuwa Masaki, Osterbay, Sinza nk.

Hii ilipelekea watu wengi hasa wa mikoani wakisikia neno Mbezi, basi akili au mawazo yao yanaenda moja kwa moja kwenye Mbezi beach. Japo Mbezi ya Kimara ilikuwepo, lakini watu hawakuwa wakiifahamu kivile kama inavyofahamika leo.

Sasa hali imekuwa ni tofauti, Mbezi ya Kimara imetokea kuwa na umaarufu mkubwa hadi kupelekea Mbezi beach kusahaulika. Leo hii mfano ukiwa mikoani ukazungumzia neno Mbezi bila kuweka hilo neno beach mbele basi kila mtu akili na mawazo yake yataenda kwa Mbezi ya Kimara kama vile mbezi luis, mbezi mwisho, mbezi magufuli nk.

Je, ni nini chanzo cha umaarufu wa mbezi kuibuka ghafla tofauti na hapo zamani?

Nawasilisha
Naendelea kusoma comment
 
Ila mipango miji tu hawazingatia
Hapo unapopaona panaitwa goba Centre zamani palikuwa panaitwa muembe madole,na kulikuwa na usafiri wa landrover na ilikuwa moja inapiga route hadi tangi bovu
Watu huko zamani walikuwa wanauza maeneo mpaka 15,000 ,20000
Ila huko bado kuna kijiji fulani kimebakia cha asili watu hapo wakuda sana ,jina lake limentoka kdg

Ova
Kerege au
 
Mzee Paul b ashanipakia sana kwenye range lake,mzee wang naye alikuwaga
Na shamba huko kubwa
Sema alikuja liuzaga mzee naye alikuwa mhuni [emoji1] baharia tena
Sema nlikuwa napuyanga naye sana kwenye pilika zake

Ova
Ahaaaa saf San mzeee walau umekaa na wazeee ..,.. mzeee kipind Niko church boy tulikuwa tunaenda sana ibada kwake
 
Ile scandal twin tower na wengine wanasema mambo kuwachapia madem [emoji1]
Ila unaambiwa jamaa alikuwa mchapakazi kazini saa moja kamili ashaingia ofisini

Ila kwa huko ifakara hajafanya lolote kabisa

Ova
kwa nchi yetu ninavyo ijua hiyo twin tower asinge weza kula peke yake pesa ya serikali mtu mmoja hawezi kuichomoa peke yake.


hapo itakuwa hilo jambo la pili hilo la kuchapa madem za watu🤣🤣🤣🤣😭😭😭

kuna kigogo mmoja nasikia alisema atamshughulikia...na kweli ameweza🤣🤣🤣 maana alimpoteza kabisa kwenye Ramani... kisha Mungu akafanya yake​
 
Pale kwny round about kma unaenda kwa mama kuna gorofa moja hivi ni amaizing. Yani yule mwamba amejenga kitu cha ndoto yake. Eneo dogo ila hyo gorofa ilivo simamaaaa.....mbezi beach wnajfungia na mageti kabisa ulinzi shirikshi mbka mchana huiingii kzembeee.....goba kuna ile half london sijui kwa mtume wa majii, ni balaaa mzee unaambiwa wte vjana hakuna mzee, hyo midude sasaaa
Ukisikia pepo ya dunia ndio hiyo ya huyo jamaa wa round about kama unaelekea kwa mama.

Watu wanaishi ndugu yangu, wengi tunawashindikiza tu bila kujua tutafika lini 😂😂😂
 
Kuna yale mabanda pale karibia na efm kwa majizzo, hivi ni mradi wa mtu ule ama nini??? Mana pembeni ni mijengo ya maana ila yale mabanda duuuh, tena yamejengwa kwa mabati kabisaaa full kuanzia ukuta mbka paa...mbezi beach kuna sehemu znachekesha sana
Unaweza kuhisi mtu anaanzisha mradi wa kufuga kuku, kumbe mwenzako anapiga hesabu ya kupangisha watu na kila mwezi anavuta elf 25 kwa kila chumba 😂😂😂
 
Yani Mbweni mpaka Mbezi Beach karibu sawa na Mbezi Beach mpaka mjini.

Huku kunatakiwa kuanzishiwe mji wake, watu wawe wanaenda mjini mara moja kwa wiki.

Lakini hapo kwa umbali wa miji mikubwa si mbali sana, basi mji wetu tu
Barabara zenyewe njia za nyoka. Sehemu ya kutumia dakika 30 unatumia masaa mawili.

Ndiomaana Dar inaonekana kubwa hatari, na wakati ni ya kawaida tu haina ukubwa wowote ukilinganisha hata na mikoa midogo tu ya Tanzania.
 
Aisee
Wabongo watavuruga tu, hakuna mipango miji
Yaani siamini mpaka leo Masaki imevurugwa vile?
Mtu akibahatika kupata chaka la kuchoma mahindi, na parking mbili tatu za bodaboda basi heshima ya Mbweni itayeyuka kama donge la chumvi ndani ya maji.
 
Miradi yote hiyo ilikuwa inflated kwanza kipindi ambacho Avic inajengwa, siamini Kigamboni ilikuwa occupied kiasi cha kwenda kujenga mbali hivyo na hata ule mradi mwingine wa dege
Lakini bado karibu sana mjini kwa kutumia daraja...labda bongo idadi ya wenye hela sio kama nigeria au kenya
Ukiona wanaija na wakenya wanavyoshangaa youtube kwa jinsi kulivyopendeza na bei ya nyumba za huko Avic town na kumetelekezwa...
Wanasema ingekuwa kwao, bei ingekuwa mara tatu na zamani kungeshajaa wenye hela zao...
 
Na wale wa viduka vya hardware huku pembeni wanauza pombe.....
Kwisha habari yake....🤣🤣
Hao jamaa huwa hawakwepeki, muda si mrefu watalivamia hilo eneo.

Mwanzo watajifanya kuzuga kwa kufanya usafi kila jioni baada ya kumaliza kazi. Kisha wakishazoea eneo tu wataanza kuwa hawafagii na wakifagia taka wanatupia mitaroni. Basi kazi kwisha, Mbweni inageuka vingunguti ya kishua 😂😂😂
 
Back
Top Bottom