Kwanini mgogoro wa Loliondo haukuibuka wakati Magufuli yupo hai? Hawa OBC ni akina nani? Kwanini Loliondo Gate? Mbona wanasiasa wa Oman?

Job Ndugai alishasema toka mwanzo, kwamba nchi itapigwa mnada hii, tukamsulubu, haya oneni sasa. Tunauzwa mchana kweupe kama mbuzi
 
Tanzania sio yetu, tupo tu ilimradi siku ziende
 
Wewe watu wote aliowachukua
shetani unawajua??Acheni maswali ya kijinga jibu hoja
kama Magufuri aliua au
hakuua,mambo ya nitajie watu
watano ukweli anaujua
Magufuri mwenyewe pamoja
na wapambe wake Makonda
na Sabaya,
Sasa ninyi mnaosema kauwa watu wengi mmejuaje ikiwa hata watu wachache tu aliyowauwa hamuwajui? Haiingii akilini labda kama unataka tu kuwa na imani kuwa Magufuli kauwa watu wengi kama kujifurahisha nafsi.

Wengine tumesikia hadi walikimbia nchi kuogopa kuuliwa ila ajabu watu mnashindwa hata watu watano tu waliyouliwa na Magu!
 
Utasubiri viongozi wa vyama mbalimbali wakusemee kero ambazo zipo kiaka nena rudi hazina utatuzi we kweli poyoyo kizazi weak sana hichi, acha watu waingie front labda serikali itasikia,
 
Mume wenu yuko motoni kama vipi kunyweni sumu mumfuate
 
Kama ww unavyoweka sifa mbele kuwa ni mzalendo namba moja, mimi ndio ninavyoweka chuki mbele kuwa alikuwa dhalimu ndani ya nchi hii.
Kumbe unaweka chuki bila sababu? Nonsense huna akili, acha zako.
 
Walishangilia nchi inafunguliwa, sasa hivi tena wanalialia. Hao wamasai ni sukagang wanahujumu juhudi za mama.
 
Wamasai Kuhamishwa Ngorongoro ni jambo la kimaendeo na ni lazima serikali isimamie maendeleo ya watu wake. Hakuna serikali Duniani inayowaacha watu waishi bila utaratibu. Dunia ni Kijiji na haikwepeki. Ni kuwadanganya Wamasai kuwa pale walipo katikati ya Simba Watakuja kupata maendeleo zaidi ya kuzaana na kuwa wengi kuliko mifugo yao.

Kosa la serikali ni kushindwa kuwekeza kwenye Suala la kuwahamisha wamasai. Ilikua ni rahisi sana kuwahamisha.

Kuna makundi ya wasomi wanaonufaika sana na maisha ya ajabu wanayoishi wamasai Karne hii. Makundi hayo ya wamaharalati ,Wao wanaishi New York, Kenya , Arusha Mjini, Dar es salaam. n.k. Wanawahamasisha Wamasai waendelee kuishi kama wanyama wakati nchi hii ni kubwa na Ina maeneo Mengi yanye malisho ya kutosha na fursa nyingine Kwa binadam. Kwa Nini watu waachwe waishi kama wanyama wakati wanatafuta ,maendeleo.

Serikali ichague Moja ama kuiacha Ngorongoro ipotezwe na BINADAM wanye akili ya kuishi na watu wengine maeneo mengine au iwahamishe Wamasai wakaishi maeneo mengine na watu wengine na waendelee na ,mifugo yao.

Hatuwezi kuwahamisha wanyama wakaja Handeni au rufiji wakati binadamu wanaweza wakahamishwa bila kupoteza chochote. Hivi Mtu akihamishiwa Eneo lingine zuri zaidi Tena akiwa na familia yake tatizo liko wapi? Wanahamishwa na mifugo yao na Mali zao na familia zao wanachogoma ni Nini ?

Serikali kama ipo sirious na Suala la kuwahamisha wamasai basi ianze kwanza kuwashughulikia wanaowazuia watu kuhama. Pili ihakikishe Eneo Hilo haliuzwi Kwa wageni.
Vinginevyo kama wanabip na kutishwa na mziki wa Wamasai basi iache Hifadhi hiyo iwe manispaa ya mji na wanyama wapotee mana hata Dar es salaam kabla ya kuja Wakoloni lilikua pori na wanyama kama nguruwe pori na fisi na Majoka yalikua yakikaa.

Watu kimara waliondolewa Kwa kubomolewa Nyumba zao bila hata kuonyeshwa pa Kwenda lakini watu waliheshimu Suala maendeleo Leo watu wanafurahia mabarabara. Ule uhodari na uthubutu wa JPM uliwafanya watu watulie na kiangalia usimamizi wa zoezi lile.

Nilitegemea mpaka Sasa nione malori ya Jeshi yakiwabeba Wamasai na kuwapeleka Mkinga, Handeni, Kilindi, Ifakara, rufiji, Lindi,Mtwara n.k. na kukabidhiwa maeneo yaliyojengwa tayari na ardhi Iliyopimwa Kwa kila familia.

Huwezi kuwahamisha watu Kwa faida ya umma halafu unashindwa kuwaonyesha pa Kwenda palipoandaliwa.
Serikali iandae maeneo ili iwapeleke na kuwapa ili ,maisha yaendelee.
 
 

Attachments

  • IMG-20220612-WA0078.jpg
    87.4 KB · Views: 3
  • IMG-20220612-WA0076.jpg
    74.4 KB · Views: 4
  • VID-20220612-WA0066.mp4
    4.6 MB
  • IMG-20220612-WA0064.jpg
    133.2 KB · Views: 3
  • IMG-20220612-WA0069.jpg
    77.8 KB · Views: 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…