Kwanini mitume na manabii huishiwa upako baada ya muda? Je, hizi pako zao ni za kweli au za mchongo?

Mganga wao yule TB Joshua hayupo hawana tena pa kukimbilia. Mwamposa soon atakuwa chali ndio maana unaona anataka kufungua hospital na Zahanati anajua fika Maji na mAfuta ni wizi.
Ndio maana nimeuliza hili jambo kwa kutoa mifano halisi. Hivi inakuwaje hawa manabii wanapoteza nguvu zao za upako baada ya muda? Ni wapi wanapokosea?
 
Ukiona hivyo ni lazima ujiulize ''utume'' na ''unabii'' wao ulitoka wapi. Kama ulitoka kwa mwanadamu utapita lakini kama ulitoka kwa Roho Mtakatifu utadumu milele
Hili neno mkuu. Nimekupata vema.
 
Karibu sana mkuu; nakusubiri.
Nimerejea kwa kuchelewa
Watu wanapobarikiwa upako, karama ama kipawa kidogo na tunu mbalimbali za kiroho hujisahau na kujiona wamefika na kunguka dhambini wakiongozwa na tamaa za kidunia na vitu viharibikavyo na kujikuta kile kidogo walichotunukiwa huishiwa nguvu na kufa

Kubarikiwa upako nk ni jambo la kwanza lakini kuulea ukue na kumea matunda ya kiroho yenye matokeo ya kimwili ni jambo lngine

Watu si wavumilivu kulea
Vipawa vyao
Upako wao
Karama zao
Tunu za kiroho nk

Kuinuliwa kidogo tu ndani ya kanisa mtu hujiona ni mkamifu kuliko wengine na kukimbilia kuanzisha huduma binafsi.. Na huko kwenye huduma binafsi badala ya kujiendeleza kiroho hujisahau na kufanya mengine ya kidunia
 
Kwa nini wewe usiende kuwauliza wenyewe mkuu, wao waijua siri.
 
Asante kwa hizi inputs mkuu Mshana Jr ; umenena vyema na kiroho zaidi. Barikiwa.
 
Kwa maoni yangu naona Kila kitu au kila kiumbe kinaendeshwa na muda na kamwe hatuwezi kupingana na muda.

Sio kwa manabii na mitume tu hata mashekh, wanasiasa, wanamichezo even wafanyakazi wa kawaida pia wanamuda wakistaaf imeisha hiyo.

Ingawa kukaa sana kwenye masikio ya watu inategemea na nidhamu ya muhusika mfano huyu mwamposa ananidham sana na wito wake na atakaa muda kabla ya kuchuja.

Itoshe kusema kila jambo na wati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…