Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Sio tangu ile connection ivuje?Tangu alipoanza kuchanganya siasa na dini heshima yake ya kiroho ilishuka kwa 99%
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio tangu ile connection ivuje?Tangu alipoanza kuchanganya siasa na dini heshima yake ya kiroho ilishuka kwa 99%
Upo sahihi.Nliendaga Tanga kanisani kwake na mgonjwa wangu pale tukataka kuelezea shida yetu tukaambiwa tutoe laki kadhaa , duh hatukuwa nazo ikabidi tuwe wapole.
Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Mkuu, ukiona huduma ya Kanisa inasimama zaidi ya miaka 10 ujue hiyo Huduma ni really!Itakua alipiga hela sana..siku hizi simuoni
wanapoteza upako kutokana na majivuno,uroho wa pesa,zinaa kwa kondoo wao,na kujiinua kama wao ndo kila ki2 badala ya MUNGU,na hii inatokea hasa wanapopata waumini wengi na huduma kuimarika!Ndio maana nimeuliza hili jambo kwa kutoa mifano halisi. Hivi inakuwaje hawa manabii wanapoteza nguvu zao za upako baada ya muda? Ni wapi wanapokosea?
Wacha weeh.Nabii Eliya aliishiwa upako hadi akamwomba Mungu ni bora amuue tu, Mungu alitaka kushusha upako wa Musa baada ya Israeli kuzingua, Musa akamwambia 'usitutoe hapa uso wako usipokwenda nasi' Mfalme Sauli na Daudi walikuwa wanashindwa vita upako wao ulipokuwa unapungua............kwa hiyo mifano ipo mingi.
Sisi tuliambiwa laki tano , tukabaki tunashangaa.Pole sana..tena anapenda 250,000 ili uweze kumuona
Nakuunga mkonoMimi nahisi wanapokuwa juu na kupata pesa nyingi,wanaanza kufuru na kuishi maisha ya anasa na uzinzi na vitu kama hivyo, ambvyo ni kinyume na mapenzi ya Mungu,kwahiyo hujikuta ile nguvu ya upako waliokuwa nayo inashuka na hatimaye wanapotea kabisa katika ramani...
Nimekupata vizuri mkuu. Kwa hiyo kumbe hawa akina Mwamposa uwepo wa upako wao ni wa muda tu? Mimi nashangaa sana mtu kupaa na kushuka kiupako hadi upako unakwisha kabisa mtu anakuwa chali kama Mzee wa Upako alivyoshuhudiwa amelewa chakali akimtukana jirani yake na kupelekea waumini wake wote kumkimbia kanisa lake limebaki tupu wanakaa popo na mijusi.Mitume na Manabii kazi yao haina kusitaafu wala kupumzika ni jukumu la milele mpaka Bwana atakapochukua Roho yake. Wote hao uliowataja nguvu zao za kiroho wamezitoa kwa yule mkuu wa kuzimu yule Joka mkuu audanganyaye ulimwengu. Kwa vile mikataba ya yule Joka mkuu ni ya muda/kipindi fulani ndiyo maana wanachuja lengo ile nguvu apewe mwingine katika mazingira mengine ili kumkomoa Bwana muumba kwa kuangamiza waja wake.
Chochote kitokacho kwa Joka mkuu hakiwezi kudumu milele iwe utajiri, umaarufu, uponyaji, unabii hata umaskini maana asili ya ile nguvu siyo ya milele, aliye wa milele ni Bwana muumba, chochote akitoacho yeye kitadumu maisha yako yote. Ndiyo maana utaona manabii na mitume wote wa Bwana, Upako wao ulikoma pale walipotwaliwa hakuna aliyepoteza mvuto akiwa bado yuko hai, hata wafalme waliopata Ukuu kwa jina la Bwana ukuu wao ulidumu maisha yao yote hata wale waliomkosea Bwana kama Sauli na Daudi hakuwaondolea ufalme wao wakiwa hai bali alisubili watwaliwe ndo baraka zake zikome.
Yuko Morogoro anamiliki Shiloh International Ministries na ana Radio inaitwa Shiloh FM inapatikana Morogoro ...Mkuu, ukiona huduma ya Kanisa inasimama zaidi ya miaka 10 ujue hiyo Huduma ni really!
Huyo Nabii fake Frank alikua ni Taperi kabisa 200% alitaka kumtaperi Dada mmoja ambaye namjua alipokuja Singida!!!
Waupako pombe ilimzidi nguvu. Wengine pia wadada wanawazidi nguvuGwajima sio mtume, na bado yupoyupo sana, Mwingira anamiliki shekeli za kutosha, makanisa kila Kona, benki, mashamba, kimsingi ana mihela, Kakobe serikali ilimtapeli mabilioni yake halafu wakampelekea mamluki wampindue!!! wa upako umesema magari yamesimama yote duh, hii sijui