Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣😂😂Anakuja Nao Yeye MwenyeweKakobe alikua anaombea vilema wanapona lakin siyo vilema unao waona mtaani vilema wote huwa ni wageni wanakuja nae
Jambo wadau?
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu na kuisha kabisa. Nabaki najiuliza maswali kadhaa yasiyokuwa na majibu:
Yaani najiuliza maswali mengi bila majibu. Ndipo nikaamua kuanzisha huu uzi kwa kuwa humu JF kuna wabobevu wa masuala ya theology akina Mshana Jr wanaweza kutusaidia kujibu baadhi ya maswali haya.
- Kwanini pako za hawa manabii zinapanda na kushuka ghafla kiasi hiki?
- Je, hizi pako ni za kweli au ni za mchongo?
- Kama ni za kweli kwanini zinaisha na kama ni za mchongo kwanini zikiisha wasirudi tena kuchukua nyingine kule wanakozitoa?
Hebu jaribu kufikiria nguvu za upako alizokuwa nazo Askofu Kakobe enzi zile anafungua kanisa lake la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) halafu ulinganishe na hali aliyo nayo sasa hivi utagundua kuna kitu hakiko sawa. Si huyu tu bali walikuwepo Mitume na Manabii wengi hapa nchini wakiwemo Mzee wa Upako, Mch Antony Lusekelo ukiangalia jinsi alivyokuwa akikusanya mtiti na mabasi yake kila kona ya nchi halafu leo ukienda kule kanisani kwake unakuta mabasi yote yamepaki unabaki unashangaa. Hapa lazima kuna tatizo sio bure.
Ukitoka kwa hawa wawili njoo kwa Mtume Mwingira na Mtume Gwajima ujiulize zile nguvu walizokuwa nazo zamani zilipotelea wapi hadi sasa wamebaki na waumini wa kuungaunga. Tatizo ni nini hasa?
Manabii na mitume waliovuma siku za nyuma na kupotea kimuujiza ni wengi lakini nimetoa mifano ya hawa wachache kama msingi wa kujenga hoja yangu. Sasa hivi Mtume Mwamposa ndiye yupo juu lakini naye atakuja kuporomoka baada ya muda mfupi.
Njooni wajuzi wote tujadiliane hili jambo mpaka tupate jawabu la pamoja.
Nawasilisha.
Hata nyakati hizo walikuwa wanakuja na kupita wao sio Mungu kwamba wadumu milele
Alikuwepo Eliya akaja Elisha na kuendelea
Gwajima sio mtume, na bado yupoyupo sana, Mwingira anamiliki shekeli za kutosha, makanisa kila Kona, benki, mashamba, kimsingi ana mihela, Kakobe serikali ilimtapeli mabilioni yake halafu wakampelekea mamluki wampindue!!! wa upako umesema magari yamesimama yote duh, hii sijui
Ndio maana nimeuliza hili jambo kwa kutoa mifano halisi. Hivi inakuwaje hawa manabii wanapoteza nguvu zao za upako baada ya muda? Ni wapi wanapokosea?
Wote uliowataja wana miaka umri zaid ya 65 nguvu za mwili zimepungua ndo maana kunakustaafu huduma
Kwa maoni yangu naona Kila kitu au kila kiumbe kinaendeshwa na muda na kamwe hatuwezi kupingana na muda.
Sio kwa manabii na mitume tu hata mashekh, wanasiasa, wanamichezo even wafanyakazi wa kawaida pia wanamuda wakistaaf imeisha hiyo.
Ingawa kukaa sana kwenye masikio ya watu inategemea na nidhamu ya muhusika mfano huyu mwamposa ananidham sana na wito wake na atakaa muda kabla ya kuchuja.
Itoshe kusema kila jambo na wati wake.
HAKUNA MTUME MJINI NI UONGO.
HAWAJUI MAANA YA MTUME.
MTUME HANA KANISA KAZI YAKE NI KUANZISHA KANISA NA KUMWACHIA MCHUNGAJI NA MWALIMU.
Mtume ni mfyeka pori yaani mpeleka dini/imani pasipokuwa na imani.
Yaani kuwaendea watu ambao hawajafikiwa na imani au ambao bado hawajapokea imani.
Ndio maana hakuna kanisa la Paulo.Very true. Mfano mzuri mtume Paulo, alifungua kazi hadi uarabuni.
Kakobe alikua anaombea vilema wanapona lakin siyo vilema unao waona mtaani vilema wote huwa ni wageni wanakuja nae
Ata huyu anaevuma Sana akienda mkoa fulani wanaopona pale wote kutoka wilaya za huo mkoa akienda Kijijini wanaopona ni wamjiniDu! Huyu alikuwa balaa aisee! Kumbe vilema wote walikuwa wa mchongo? 😀 😀 😀 😀
Jambo wadau?
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha na maneno mengi. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia upako wa manabii na mitume jinsi wanavyoanza huduma zao kwa pako za hali ya juu sana lakini baada ya muda zile pako huanza kufifia taratibu na kuisha kabisa. Nabaki najiuliza maswali kadhaa yasiyokuwa na majibu:
Nawasilisha.
Mtume Paul alifanya Kazi ya uinjilisti zaidi kuliko Kazi ya utumeNdio maana hakuna kanisa la Paulo.
Kazi yake ilikuwa kuhubiri na kufungua kanisa na kuweka mzee wa kanisa...leo tunawaita wachungaji
Wakishapata pesa SAsa upako tena wa nini tena.Ndio maana nimeuliza hili jambo kwa kutoa mifano halisi. Hivi inakuwaje hawa manabii wanapoteza nguvu zao za upako baada ya muda? Ni wapi wanapokosea?