Kwanini mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika ufadhiliwe na Benki ya dunia?

Kwanini mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika ufadhiliwe na Benki ya dunia?

hiyo ndio sababu kubwa ila viongozi wenye akili wameenda Urusi kwani tofauti ya mkutano wa Urusi na huu uliofadhiliwa na benki ya dunia, wa Urusi unapenda kuzungumzia changamoto za uchumi wa Afrika na na na ya kuzitatua lakini huu wa benki ya Dunia unafanya waafrika waamini bila misaada na mikopo ya benki ya Dunia hawawezi kujitegemea
Benk ya Dunia ilikuwepo na IPO lakini hali ya Afrika inazodi kuzorota kila mwaka. Ni heri ya hawa waliokwenda Moscow huenda wakaja na aina nyingine ya kufikiria na kutenda kuliko hii status quo.
 
Wataweza vipi nao ni wanafiki? Nilipoona hadi wale wanaojiita wanamajumui wa kiafrica wanamkana Gadafi nikajisemea "lama sabachtan", yale maono aliyokuwa amayabeba Gadafi alikufa nayo pale katika ardhi ya kwao hawa wengine ni wahuni tu
Viongozi wa Afrika wanatafunwa mmoja baada ya mwingine kama nyumbu wanavyotafunwa na simba kila mmoja kwa wakati wake. Wakati Simba wanaungana kumshambulia nyumbu mmoja kwa upande wa nyumbu sio hivyo, wanakimbiana badala ya kusaidiana kumjeruji Simba kwa pembe zao na kwato zao.
 
Unapoitaja World Bank, IMF na WTO ni sawa na kuitaja Marekani na Ulaya Magharibi. Kama mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika Tanzania umedhaminiwa na Benki ya dunia maana yake umedhaminiwa na nchi ya Marekani.

Kwanini AU na waafrika wenyewe wameshiñdwa kuudhamini mktano wao?

Are we serious?
Sasa kwani benki ya dunia biashara yake si ni kukopesha nchi mbalimbali zikiwemo hizi za Africa sasa ubaya nini kuwasponsor wateja wako.
 
Kama mnauza hadi nchi mtaweza kuchangia mkutano?
 
Sasa kwani benki ya dunia biashara yake si ni kukopesha nchi mbalimbali zikiwemo hizi za Africa sasa ubaya nini kuwasponsor wateja wako.
Viongozi wengi wa Afrika wanacheza nafasi ya udalali kwa maslahi na sifa zao binafsi na maslahi mapana ya mabeberu. Ukweli inauma na kuumiza sana. Ni heri kusogea polepole kwa uhakika na heshima kuliko kukimbia sana bila tahadhari, na kudharauriwa. Hakuna nchi hata moja ya Afrika ambayo imenufaika kwa kutumia misaada ya mabeberu. mabeberu wana agenda yao ileile iliyowasababisha waendeshe biashara ya utumwa na kutafuta makoloni. Sababu za kuendesha biashara ya utumwa na kutafuta makoloni zimebaki zilezile na zipo palepale, ni za kudumu. Hakuna kiongozi wa Afrika anapaswa kulisahau jambo hili na agenda hii kila siku 24/7 kwa siku 365.
 
Benk ya Dunia ilikuwepo na IPO lakini hali ya Afrika inazodi kuzorota kila mwaka. Ni heri ya hawa waliokwenda Moscow huenda wakaja na aina nyingine ya kufikiria na kutenda kuliko hii status quo.
Moscow labda waje na silaha tu.
Warusi kama raia ni maskini mnoo, matajiri nao ni tabaka la watu kama kikundi tu nao wana utajiri wa kukufuru .
 
Huyu ndiye anaekuwa sehemu ya mabadiliko ya dunia, wengiine wajemeni!!!!

AU bado ni ombaomba tu, Isitoshe wanachama wake wapo dhoofu kiuchumi
Tuna marais ambao hawakerwi na toothpicks kutoka China kwenye meza zao za chakula.
 
Benk ya Dunia ilikuwepo na IPO lakini hali ya Afrika inazodi kuzorota kila mwaka. Ni heri ya hawa waliokwenda Moscow huenda wakaja na aina nyingine ya kufikiria na kutenda kuliko hii status quo.
Umeanza kwa kuuliza swali zuri kabisa: kwa nini nchi za Afrika zisigharamie mkutano wao zenyewe badala ya kufadhiliwa na Benki ya Dunia? Yaani kwa nini zile tegemezi hata kwa mambo ya kimkakati kama hayo?

Sasa hiyo “heri” ya kwenda Urusi inatoka wapi tena? Yaani nchi zote za Afrika zisiwe na akili ya mikakati ya maendeleo yao hadi zipigwe boost na mwamba mmoja wa kizungu (Mrusi Putin); kweli? Mrusi aliyezidiwa akili hata na Mchina kwa mbali? Yaani unapona kuliwa na simba unashangilia kuliwa na dubu? eti afadhali!

Mkuu usijidanganye: tatizo la Waafrika haliko nje wala jawabu haliko nje. Liko ndani ya Afrika. Achana na Marekani, Ulaya na Urusi. Hivyo ni visingizio tu.

Shughulika na viongozi wako waliojaa ujinga, ubinafsi, uroho na ufisadi wa kila aina kwa nchi zao. Wamerundika pesa za nchi zao za wizi kwenye mabenki ya Marekani na Ulaya. Wanatajirisha makampuni ya kibepari duniani (multinationals) halafu, kinafiki, wanajifanya dugu moja na madikteta wa “kikomunisti”. Hakuna siri. Wanajiaibisha dunia nzima.
 
Of the total budget, 38% is to be assessed on Member States while 61% will be from partners. The operating budget will be fully funded by Member States while the programme budget will be funded 41% by Member States and 59% solicited from international partners.

Sasa hiyo 61% karibu 80% yake anatoa Marekani. Bajeti ya AU zaidi ya 61% wanatoa wafadhili kina World Bank na IMF na Marekani.

Nadhani sasa unaelewa.

Afrika kuna laana ya asili,
 
Kaka lengo ni kuwafanya viongozi wa Afrika wakose nafasi ya kuhudhuria safari ya kwenda Moscow

Huo ndio ukweli wenyewe, 100%. Viongozi wetu ni wajinga kiasi hiki?

Viongozi makini kama Museven hawezi kuhudhuria mkutano ambao anajuwa umefadhiliwa na mashoga.

Hao viongozi wa afrika walishikiwa bunduki kwamba wasiende huko mosscow?
 
Kaka lengo ni kuwafanya viongozi wa Afrika wakose nafasi ya kuhudhuria safari ya kwenda Moscow

Huo ndio ukweli wenyewe, 100%. Viongozi wetu ni wajinga kiasi hiki?

Viongozi makini kama Museven hawezi kuhudhuria mkutano ambao anajuwa umefadhiliwa na mashoga.

Sio wajinga sema umasikini mana wakimgomea bwana mkubwa watakula wapi?
 
Anaelipa ndiye anaechagua wimbo. Ukiona hivyo mkutano huu una manufaa kwa westerns than to Africans. I can guess why now
Wakiacha hao Wazungu, mtu mweusi anaweza kupotea hapa Duniani.

Chanjo za watoto wanalipia wao. Matibabu ya kifua kikuu na cancer wanalipia wao. Dawa za ukimwi wanalipia wao. Bajeti zetu kwa 40% zinategemea wao. Mikopo wanatoa wao. Utalii tunawategemea wao. Tekinolojia zote tunawategemea wao.

Mwafrika, una nini cha kujivunia? Ukisaidiwa ushukuru tu. Afrika haioni hata mwanga wa kuondoka kutoka mkiani katika maendeleo ya kila aina. Watawala wao wanazidi kuwatia gizani kwa kukosa upeo.
 
Ni hujuma ili viongozi wengi wa Afrika wasiende kukutana na Putin Urusi
Shida ya Afrika ni umaskini. Sasa uende kwa Putin ukafanye nini? Putin mwenyewe mambo yalipoharibika kabisa, aliwakimbilia na kuwapigia magoti hao wa nchi za Magharibi. Wakampa mabilioni ya pesa lakini kwa sharti la kuheshimu uhuru na matakwa ya states mbalimbali. Akatii sharti, akatoa uhuru wa wananchi kuamua. Ikawa ndiyo mwisho wa USSR.

Sahizi amerudi tena kwenye udikteta, lazima uchumi wake uparanganyike kama zamani. Mbeleni lazima warusi wapige magoti.
 
Jengo la Makao Makuu ya AU Ethiopia limejengwa kwa msaada wa China. Safari bado ndefu sana
 
waafrika wamekwama sana. hopeless kabisa! fikiria wewe ni mwanaume halafu jirani yako mwanaume anamnunulia mkeo pants. what would u think of this!

YESU ANAOKOA
 
Umeanza kwa kuuliza swali zuri kabisa: kwa nini nchi za Afrika zisigharamie mkutano wao zenyewe badala ya kufadhiliwa na Benki ya Dunia? Yaani kwa nini zile tegemezi hata kwa mambo ya kimkakati kama hayo?

Sasa hiyo “heri” ya kwenda Urusi inatoka wapi tena? Yaani nchi zote za Afrika zisiwe na akili ya mikakati ya maendeleo yao hadi zipigwe boost na mwamba mmoja wa kizungu (Mrusi Putin); kweli? Mrusi aliyezidiwa akili hata na Mchina kwa mbali? Yaani unapona kuliwa na simba unashangilia kuliwa na dubu? eti afadhali!

Mkuu usijidanganye: tatizo la Waafrika haliko nje wala jawabu haliko nje. Liko ndani ya Afrika. Achana na Marekani, Ulaya na Urusi. Hivyo ni visingizio tu.

Shughulika na viongozi wako waliojaa ujinga, ubinafsi, uroho na ufisadi wa kila aina kwa nchi zao. Wamerundika pesa za nchi zao za wizi kwenye mabenki ya Marekani na Ulaya. Wanatajirisha makampuni ya kibepari duniani (multinationals) halafu, kinafiki, wanajifanya dugu moja na madikteta wa “kikomunisti”. Hakuna siri. Wanajiaibisha dunia nzima.
Umenena vema lakini hapana hapana hapana. Kuna ukweli fulani kuwa viongozi wetu kuna wezi ndiyo lakini sio wote, lakini kitu cha kushangaza ni kwamba mataifa yote ya Afrika chini ya jangwa la sahara yana hali sawa ya mambo na kiuchumi, mataifa yote ya Afrika kaskazini yana aina moja ya hali na uchumi, mataifa yote ya Asia yana aina moja ya hali na uchumi na mataifa yote ya Amerika kusini yana aina moja ya hali na uchumi. Hii kaka haiwezi kuwa imetokea kwa bahati tu (chance). Hali hii imetokea chini ya usimamizi wa Benki ya dunia, IMF, WTO, US Dollar, Swift, VISA, Pound, Euro, commonwealth, na mifumo mingine ya wale ambao walikuwa wameitawala dunia (wakiloni wetu) pamoja na Marekani. Ili Afrika itoke hapo ilipo ni lazima itoke kwenye mifumo yote ya Benki ya dunia, IMF, WTO, US Dollar, Swift, VISA, Pound, Euro, commonwealth, na mifumo mingine ya wale ambao walikuwa wameitawala dunia (wakiloni wetu) pamoja na Marekani.

Kaka haiwezekani nchi zote chini ya jangwa la Sahara zifanane kwa upumbavu kama hivi. Kuna nchi mpaka zimeshabadilisha viongozi wao na vyama vyao vya ukombozi kutoka madarakani lakini waaapi hali ni ileile na kupitiliza. Hii ina maana kuwa ipo common factor kwa hali hii. Kuna kundi powerful linaloiendesha dunia litakavyo. Viongozi wetu hawana cha kufanya wala la kufanya dhidi ya kundi hili ambalo liko tayari kuurudisha ukoloni upya kama likizidiwa nguvu. Nchi unazoziona zimewekewa vikwazo kama vile Urusi, NKorea, Cuba, Zimbabwe, Iran, Syria, Lybia, Iraq, Venezuela, na karibuni itakuwa Uganda na South Africa ni nchi ambazo viongozi wao walilighamua tatizo na kujaribu kuchukua hatua dhidi yao. Hili ndilo kundi ambalo Afrika chini ya jangwa inapaswa liliunge mkono kama wanataka hali tofauti ya mambo kwenye nchi zao.
 
Afrika kuna laana ya asili,
Sio laana mkuu, hali hii imetengenezwa na wakoloni wetu wa zamani. Hata wakati wa ukoloni kulikuwa na mitaa ya duni ya waafrika weusi (compound), mitaa yenye ahueni ya waasia (uhindini) na mitaa mizuri ya Uzunguni. Hata leo hii wanahakikisha mitaa (nchi) hiyo inadumishwa. Nchi zote za weusi ni duni, nchi za waasia zina ahueni na nchi za wazungu ni bora na nzuri. Kuna mifumo inayohakikisha jambo hili linatekelezeka, na mifumo hiyo ni Benki ya dunia, IMF, WTO, US Dollar, Swift, VISA, Pound, Euro, commonwealth, na mifumo mingine ya wale ambao walikuwa wameitawala dunia (wakiloni wetu) pamoja na Marekani.

Yuko mtu ambae anapanga bei ya trekta lake na bei ya dhahabu yako, bei ya gari lake na bei ya korosho yako, utatoboa vipi hapo? Kinachomponza Urusi ni kuwazuia mipango yao hiyo ya kinyonyaji. Hatuna budi kumpa sapoti.
 
Viongozi wengi wa Afrika wanacheza nafasi ya udalali kwa maslahi na sifa zao binafsi na maslahi mapana ya mabeberu. Ukweli inauma na kuumiza sana. Ni heri kusogea polepole kwa uhakika na heshima kuliko kukimbia sana bila tahadhari, na kudharauriwa. Hakuna nchi hata moja ya Afrika ambayo imenufaika kwa kutumia misaada ya mabeberu. mabeberu wana agenda yao ileile iliyowasababisha waendeshe biashara ya utumwa na kutafuta makoloni. Sababu za kuendesha biashara ya utumwa na kutafuta makoloni zimebaki zilezile na zipo palepale, ni za kudumu. Hakuna kiongozi wa Afrika anapaswa kulisahau jambo hili na agenda hii kila siku 24/7 kwa siku 365.
Tatizo letu ni uvivu wa kutenda nchi za east asia na zile asean zilishakuwa makoloni zilishakuwa na mambo ya utumwa zilishakopa world bank ila nyingi kwa sasa zina uchumi imara na zipo vizuri sio tena masikini ,wakati wewe ukiona maji ni huduma unayangangia idara ziendeshwe na serikali wengine tunaona maji ni biashara sera zibadilike kampuni binfasi ziuze zisambaze maji mijini ,vijijini na mashambani haina haja ya kukopa kutekeleza miradi ya maji hii ni kubadili sera tu kama vile kwenye mitandao ya simu huu ni mfano tu wa eneo moja tu ,kiuhalisia tunahitaji ubepari wakitanzania ( capitalis in Tanzani context) utaoendana na utamaduni wetu na public ijitoe kwenye biashara ibakie kwenye sekta chache za huduma hapo nchi za Africa zitabadilika na itakuwa sehemu kubwa haiba sababu ya kwenda kukopa kopa nje na hivi ni kwa uchache tu otherwise NB: lile soko la hisa pale halina maana kama bado kila sekta inakuwa inamilikiwa na ummah.
 
Back
Top Bottom