Umenena vema lakini hapana hapana hapana. Kuna ukweli fulani kuwa viongozi wetu kuna wezi ndiyo lakini sio wote, lakini kitu cha kushangaza ni kwamba mataifa yote ya Afrika chini ya jangwa la sahara yana hali sawa ya mambo na kiuchumi, mataifa yote ya Afrika kaskazini yana aina moja ya hali na uchumi, mataifa yote ya Asia yana aina moja ya hali na uchumi na mataifa yote ya Amerika kusini yana aina moja ya hali na uchumi. Hii kaka haiwezi kuwa imetokea kwa bahati tu (chance). Hali hii imetokea chini ya usimamizi wa Benki ya dunia, IMF, WTO, US Dollar, Swift, VISA, Pound, Euro, commonwealth, na mifumo mingine ya wale ambao walikuwa wameitawala dunia (wakiloni wetu) pamoja na Marekani. Ili Afrika itoke hapo ilipo ni lazima itoke kwenye mifumo yote ya Benki ya dunia, IMF, WTO, US Dollar, Swift, VISA, Pound, Euro, commonwealth, na mifumo mingine ya wale ambao walikuwa wameitawala dunia (wakiloni wetu) pamoja na Marekani.
Kaka haiwezekani nchi zote chini ya jangwa la Sahara zifanane kwa upumbavu kama hivi. Kuna nchi mpaka zimeshabadilisha viongozi wao na vyama vyao vya ukombozi kutoka madarakani lakini waaapi hali ni ileile na kupitiliza. Hii ina maana kuwa ipo common factor kwa hali hii. Kuna kundi powerful linaloiendesha dunia litakavyo. Viongozi wetu hawana cha kufanya wala la kufanya dhidi ya kundi hili ambalo liko tayari kuurudisha ukoloni upya kama likizidiwa nguvu. Nchi unazoziona zimewekewa vikwazo kama vile Urusi, NKorea, Cuba, Zimbabwe, Iran, Syria, Lybia, Iraq, Venezuela, na karibuni itakuwa Uganda na South Africa ni nchi ambazo viongozi wao walilighamua tatizo na kujaribu kuchukua hatua dhidi yao. Hili ndilo kundi ambalo Afrika chini ya jangwa inapaswa liliunge mkono kama wanataka hali tofauti ya mambo kwenye nchi zao.