Kwanini mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika ufadhiliwe na Benki ya dunia?

endapo unasema ukweli na takwimu zako ni sahihi, sasa hiyo BRICS inayopigiwa upatu itatuvusha au porojo tu za kisiasa.
 
Moscow labda waje na silaha tu.
Warusi kama raia ni maskini mnoo, matajiri nao ni tabaka la watu kama kikundi tu nao wana utajiri wa kukufuru .
Aisee acha wivu basi...marekani angeweza kuwadindia nchi 30+ kama urusi anavyodindisha hadi mda huu? Cuba tuu ilimtoa kamasi kwa warning ya Urusi had aka-sign mkataba wa kutambua mipaka ya NATO dhidi ya Urusi, leo hii amevunja mikataba yoote na kumzunguka Urusi kwa nia ileile ovu..rushwa, uuaji kwa kusambaza madawa ya kulevya, kufadhili silaha na vikosi vya kimapigano kwa majirani wa wanaokataa sera zake za kinyonyaji, nakuhakikishia siku nchi za Africa zikigomea sera mbovu za mabeberu zitapigwa vikwazo hadi wananchi tufe kwa kwashakoo..
 
It was done to enslave Africans with money and debt
 
Alaaniwe mwalimu wako aliekufundisha western propaganda.

Adui wa maendeleo ya afrika ni ukoloni uliopita + ukoloni mamboleo....

Baba yake na babu yangu alikua ni chief aliepewa upendeleo sana na wakoloni, akawakandamiza aliowatawala ili afaidi mema aliyopewa na wakoloni..ukikataa unakufa madarakani au vita inakutafuna unakufa...

Shame on your teachers...
 
Well said mkuu[emoji482][emoji482][emoji482]
 
Uko sahihi sana, serikali legelege kuhodhi utoaji wa huduma muhimu ni kati ya chanzo Cha hali hii. Hata hapa nchini ona, TTCL imekufa lakini mitandao binafsi ya simu inaendelea, UDA imekufa lakini daladala zipo, TBC inasuasua lakini media nyingine zinachanja mbuga, nk. Nchi za Asia ni ama walikaribisha uwekezaji au walisimamia kikamilifu uendeshaji na usimamizi wa huduma, waliua hadharani yeyote yule mbadhilifu. Sisi hatukukarinisha uwekezaji binafsi na hatusimamii utoaji huduma. Ni pango la wezi, Wala rushwa na wabadhilifu wa Mali za umma.
 
Nakubaliana ila siafiki kwenye msemo wa serikali lege lege mi naamini kwenye nchi zinazoendelea kunahitajika uwekezaji kutoka nje bila kuumizana au kuuana hadharani na mfano mzuri umeusema huu wa ttcl na makampuni binafsi ambayo huhitaji kukopa ili kuimarisha upatikanaji wa maendeleo ni kupata wawekezaji walete fedha na teknolojia huku fedha za umma zikafanya mengine ambapo pia ukiacha simu na pia kwenye habari (magazeti,redio na tv) tumefanya vizuri kwa kuwa sekta inamilikiwa kwa kiwango kikubwa na sekta binafsi baada ya kubadili sera zetu na ajira na kodi zinapatikana vivyo hivyo kwenye maji tukibadili sera iwe ruhusa watu au kampuni binafsi kuzalisha na kusambaza maji ishindane na za umma automatically wananchi watapata huduma stahiki na serikali kupata kodi stahiki na mwekezaji stahiki yake na nchi kupiga maendeleo kwenda mbele na hii ikifanyika kwa utulivu kwa kushirikisha sekta mbalimbali ambazo ni kero kwa watu basi nchi inakuwa inapaa kiuchumi sisi hatuhitaji kwenda kucopy nje zaidi ya kujifunza ya hapa na hasa kupitia sekta zile tumeziruhusu ziwe na uwekezaji jinsi zilivyokuwa na manufaa hususani simu na habari.
 
Ukitoa shida za mfumo kandamizi wa WB, IMF, WTO, USD, swiftly, VISA, commonwealth, na westerns kuyaatamia ex- colonies Yao hata baada ya kupata uhuru, shida kuu ya ndani ni viongozi wa Afrika kujiwekea kinga ya kutokushitakiwa hata wakifanya nini kibaya. Mfumo huu wa kinga unazalisha wezi, wala rushwa na wabadhilifu wa mali za wananchi na matumizi mabaya ya mikopo na misaada. Misaada mingi ya Magharibi Imeficha hila, mitego na Nia ovu ndani yake. Ndio maana misaada mingi kutoka nchi za magharibi sio Ile ya kujenga viwanda mama, kutoa teknolojia, wala kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo, ufungaji, uvuvi, misitu na madini. Misaada Yao mikubwa ni kwenye kupunguza idadi ya watu, kutunza misitu na mbuga za wanyama.
 
Huwa siwajibu wapuuzi kama wewe.
Kwa hiyo wameenda kujifunza vita?
Huelewi hata nilichoandika unahorojoka ti hapa.
 
Aisei, huu ndio muda wa kumkataa shetani na kazi zake zote. Huu ni muda wa Afrika kuchagua njia nyingine kama wakitaka wapate matokeo yaliyotofauti na haya ya sasa. Afrika ianze kwa kuondoa vikwazo vya kutembeleana na kuuziana bidhaa wenyewewe kwa weenyewe kwa kutumia utaratibu wa kiafrika kwa kutumia sarafu za kiafrika. Afrika ijitoe kwenye kivuli cha wakoloni/watesi wake wa zamani. Afrika haihitaji vitu kama commonwealth, IMF, World bank, WTO, wala kutumia pesa za kigeni kununua bidhaa nchi nyingine. Afrika inahitaji aina nyingine ya silaha za kivita ambazo zitamudu kujilinda dhidi ya uvamizi wa wakoloni wetu wa zamani watakapotaka kurudi tena kututawala. Afrika inahitaji elimu na lugha inayojibu maswali yetu.
 
Ulitaka ufadhili wewe?
 
Nimekuelewa kimsingi wanatumia principle ya kuzuia matatizo kabla hayajafika kwao yaani ni misaada ambayo tunaona kama misaada ila kiuhalisia tunasaidiana mfano ukisaidia kwenye kupiga vita mabadiliko ya tabia nchi au kifua kikuu inamaana hivi vikitokea kwa wingi kwenye nchi zinazoendelea basi vitawarudia na wao yaani vitafika kwao ni sawa tu usipozima moto nyumba ya jirani itakayofuata ni ya kwako ,technically ni misaada ya kusaidiana wanaweza kuleta mabadiliko na maendeleo sio serikali zao na misaada yake bali ni kampuni zao hasa zikija kufanya investment wataleta tech n, skills na money tena tukiweza kushawishi kampuni zenye products za kuexpo kurudisha kwao then tutawin.
 
Eeewaaa!! Wewe ndo umeleewa kile hasa ninachokisema. Wakoloni hawakujenga reli, barabara, shule, hospitali, kumbi za sinema, umeme, makanisa, bandari, kutunza misitu na mbuga za wanyama kwakuwa walitupenda sana, lahsha, vyote hivyo vilikuwa kwa faida Yao (directly and indirectly) wao. Walishasema kuwa wao hawana Cha bure (no free lunch) hata kimoja, wewe unataka wasemeje tena hadi uelewe?,

Ukiona wanasema wakujengea wao barabara ujue miongoni mwa mafundi wajenzi wao Kuna mashushu wao wenye kazi maalumu nchini kwako au nchi jirani, humo humo mna wataalam wa miamba, madini wanaochunguza wapi madini yaliko, humohumo una watu wamekuja kuchukua mali zao ambazo walizoacha/walizoficha wakati wa ukoloni, nk. Sio bure, sio huruma, sio msaada.
 
Hao AU wanafadhiliwa na whites ili mambo yaende. We unaona muafrika ana jipya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…