Kwanini mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika ufadhiliwe na Benki ya dunia?

60 Trillions? Cross check you figure
Mtu alieishi Marekani anafahamu kuwa Marekani kuna maskini wengi sana, watu wasio na makazi ni wengi sana pengine kuliko nchi yoyote, wanalala nje au kwenye magari mabovu na magari yao mazima. Yaani mchana ni gari na usiku ni nyumba. Kwanini serikali haitoi msaada kwa watu wao hawa wenye uhitaji badala yake wanatoa msaada Kwa waafrika sisi? Kwanini maji yawe mazito hivi kuliko damu? Ndugu zangu amkeni amkeni amkeni mfanye kazi, hakuna msaada hapa ni mitego kila kona.
 
Ni sawa tu mpaka siku waafrika tutakayopata akili
Viongozi Wana akili nyingi, na sio kwamba hawajui, bali wanatishiwa maisha yao Ile mbaya, wengine wameuawa, wengine wamepinduliwa na wengine wamewekewa vikwazo na wengine wanawindwa kama swala kwaajili ya misimamo Yao dhidi ya ujinga wao. Ukiona kiongozi wa Afrika anasakamwa sana mabeberu na vibaraka wao ujue kiongozi huyo Yuko sahihi, anaejitambua na anawabwekea. Lakini ukiona kiongozi wa Afrika Yuko salama hata kama nchini kwake hakuna demokrasia, Yuko madarakani kwa muda mrefu, ni mwizi na mbadhilifu wa mali za watu wake ujue kiongozi huyo amekubali matakwa yao, wanamuona bwege, mzoga, na punguani asiyejitambua. Huwa Wana msemo wao kuwa anaekubali kunyonywa mnyonye hadi afe.
 
Lengo la wamarekani kudhamini kupitia bank ya dunia mkutano huo wa dar es salaam wakati mmoja na mkutano wa urusi na afrika ni ili kuvuruga mkutano wa urusi na afrika. Uongozi wa samia kwa kutojua au kujua wametumika tu. Hizo gharama hatujui ni ufadhili au mkopo. Na kama ni mkopo ni kwa tanzania au AU.
 
Tarehe ya mkutano wa Russia-Africa ilifahamika tangu zamani, lakini mkutano wa DSM wa watu walewale wanaohitijika kwenda st. Petersburg ukapangwa tarehe hizohizo. Hii ni kuonyesha viongozi wetu wanakutana na mambo magumu sana kutoka kwa wakoloni wetu wa zamani. Tuwaombee kwakweli.

Tuhitaji set mpya kabisa ya mambo. Nchi zitakozokiwa karibu na BRICS huenda zikatoboa sana.
 
Africa hatuna viongozi. Je unajua Israel pia huhudhuria vikao vya African Union kama msikilizaji? Yaani that generation should be wiped out
 
Africa tunapenda "KITONGA"
 
Africa hatuna viongozi. Je unajua Israel pia huhudhuria vikao vya African Union kama msikilizaji? Yaani that generation should be wiped out
Baada ya miaka 60 ya kujitawala inayofanya vijana walikatae bara lao kwa umaskini unaozidi kuongezeka kila siku Afrika inahitaji mawazo mapya, njia mpya na silaha mpya kabisa. Kijana yuko tayari afike ulaya/marekani hata kwa mateso makali sana ili akakutane na dhahabu yake iliyoibiwa kutoka nchini kwake. Viongozi wetu kwa miaka 60 yote wanadanganywa kwa kupewa mikate yenye samadi katikati.
 
Bank si inafanya biashara?

Au ulikuwa unafikiri bank kazi yake kugawa sadaka?
 
Bank si inafanya biashara?

Au ulikuwa unafikiri bank kazi yake kugawa sadaka?
inategemea imekukopesha kufanya kitu gani kwa masharti gani. Bank haiwezi kukukopesha fedha za kuchimbia madini yako, kuongeza thamani mazao yako ya kilimo, mifugo wala misitu, benk haiwezi kukukopesha ujenge kiwanda cha kutengeneza mbolea wala matrekta kwa kilimo chako. Wazungu wanataka kuletee hata mbegu za chakula chenu kikuu
 
Kwanini miradi mingi ya afya ya nchi za afrika ifadhiliwe na hao hao World Bank?.
 
Wataweza vipi nao ni wanafiki? Nilipoona hadi wale wanaojiita wanamajumui wa kiafrica wanamkana Gadafi nikajisemea "lama sabachtan", yale maono aliyokuwa amayabeba Gadafi alikufa nayo pale katika ardhi ya kwao hawa wengine ni wahuni tu
Gadhafi usisahau alikuwa mshenzi tu kama washenzi wengine. Alimsaidia Uganda katika vita ya mwaka sabini na nane, tukawapiga waganda pamoja na majeshi yao ya kukodi ya Libya.
 
Kwanini miradi mingi ya afya ya nchi za afrika ifadhiliwe na hao hao World Bank?.
humo ndani kuna mitego mingi wanafanya. Nikwambie ukweli wazungu huwa wanafanya tafiti nyingi za dawa na vifaa tiba vyao kutumia waafrika bila idhini yao kwa kutumia mwamvuli wa kutoa misaada. Pale Marekani chuo kikuu cha afya cha kwanza kilijengwa pale Detroit kwasababu wa upatikanaji kwa wingi wa waafrika waliokuwa wanafariki (cadaver) kwa wingi kutokana na moshi, vumbi na sumu nyingi za viwandani. Wazungu hawataki waafrika kuwe na idadi kubwa ya watu, hivyo hawataweza kamwe kufadhili mradi utakaosababisha waafrika wawe wengi, na kati ya mambo yanayosaidia kupunguza idadi ya watu kwenye jamii ni matumizi ya uzazi wa mpango, watu kupoteza uwezo wao wa kuzaa, kufa na kuhama nchi. Mambo yote haya ya uzazi wa mpango, kutoteza uwezo wa kuzaa, kufa na kuhamisha watu ni agenda yao. Mfano, wanachochoa migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na kuwapa silaha za kuuliana, mnapouana mnapunguza idadi yenu, wanatoa Greencard ili watu wenye nguvu na maarifa wazihame nchi zao, nk
 
Hizi nyingi ni siasa za whatsapp, kumbuka kuwa mkono unaotoa ndio unobarikiwa. Hizi ni hadithi kwamba wazungu hawatupendi na wanataka watuue. Ni upuuzi mtupu wa watu wenye akili zile zile za kibaguzi sawa na zile za wazungu wenye hulka za kibaguzi.

Dada yangu ni mtaalam wa public health na kazi zote wanazofanya hao wazungu yeye ndiye mtendaji mkuu, haongelei kabisa hizo kasumba zinazosambaa sana mitandaoni.
 
Dada yako!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…