Kwanini Mkuu wa Majeshi(JWTZ)anatokea Kamandi Moja tu, wakati tuna Kamandi Sita?

Kwanini Mkuu wa Majeshi(JWTZ)anatokea Kamandi Moja tu, wakati tuna Kamandi Sita?

Raia umpe nafasi ya kujadili jeshi ? Raia anajua nini kuhusu jeshi ? Kama mtu huna uelewa na kitu inakuwaje unataka nafasi ya kujadili usichokijua ? Mtu mwenye nafasi ya kujadili ni yule mwenye uelewa wa hicho kinachojadiliwa , kama huna uelewa huwezi kujadili hata kidogo
Jeshi linasimamiwa na raia, liko chini ya utawala wa kiraia.
 
Hili naweza jibu ,katika muundo wa jeshi letu kamandi ya nchi kavu ni jeshi mama ,askari yyte bila kujali kamandi yake lazima awe na basic infantry course ,kwaiyo ukishafika hizo position za juu mfano Chief of staff au CDF ceremonial dress ,number 3 ,combat etc utavaa za nchi kavu kama kiwakilishi cha jeshi la nchi kavu kuwa jeshi mama
Labda ungetoa mifano ya maofisa waliotoka kamandi ya anga au navy ambao iliwabidi kuvaa uniform za nchi kavu walipoteuliwa kuwa chief of staff au CDF.
 
Mimi tuko tofauti kidogo, kila mtu aspecialize kwake mapema kama majeshi ya wenzetu, unakuta mtu kafanya kozi ya infantry, vifaru , na navy lkn mwisho wa siku anatumia ujuzi mmoja tu, jeshi linakua linaingia gharama kubwa kuwafundisha vitu ambavyo hawavitumiaa.. kuhusu ikitokea umetekwa au pilot kuangukia porini, ukishakua mwanajeshi haijalishi ni airforce , navy au landforce lazima uweze kujua kutumia personal weapon , uwe na uwezo wa kutembea some Kms, uwe na uvumilivu wa kusurvive kwenye harsh environment,, haikuhitaji kuwa askari wa miguu kujua haya mambo.
Sahihi, wanajeshi wote duniani lazima wapate basic combat skills.
 
Ule utaratibu kwa upande wangu sio mzuri kwa sababu unamlazimisha Rais kumteua mkuu wa majeshi hata asiyemtaka.
Pia ni rahisi sana watu kufanyiaba hujuma.
Vilevile unaweza sababisha mtu mzuri kukosa nafasi kwa sababu sio zamu ya kamandi yao kutoa CDF.
Utaratibu wa kupokezana ndio mzuri zaidi, una hakikisha mkuu wa majeshi na wakuu wote wa kamandi wanapatikana kwa merit na ndio itaratibu unaotumiwa na nchi nyingi zilizoendelea na ambazo majeshi hayachanganywi sana na siasa.
 
Utaratibu wa kupokezana ndio mzuri zaidi, una hakikisha mkuu wa majeshi na wakuu wote wa kamandi wanapatikana kwa merit na ndio itaratibu unaotumiwa na nchi nyingi zilizoendelea na ambazo majeshi hayachanganywi sana na siasa.
Yeah, hapa kama kuna ukweli. Maana mpaka kuwa mkuu wa kamandi maana yake vigezo vya kuwa CS au CDF unavyo. Na nadhani katika chaguzi za CDF majina yanapendekezwa kutoka kwa hawa wakuu.
 
Hata kama ni common, lakini una viashiria vya uropokaji na hutoshi kuaminiwa. Your mind is very limited. Wenye akili wameelewa. Bahati mbaya sana humu mnatumia fake name, nina uhakika wakubwa wako wangekufahamu wangekuweka mbali na nyaraka. Labda uwe tu msimamizi wa jiko
Hakuna jambo lenye madhara hapo mbona hata Facebook nishawai mrekebisha yerico Nyerere kwenye post zake alisemaga jeshi letu lina kamandi tatu nikamkatalia na kumpa ufafanuzi wa kina na hao wakuu unaosema tukionana wanabaki kupongeza tu Kwa elimu sahihi nayotoa,, tatizo lako we hujui taarifa zipi zinafaa kuwekwa au kufafanuliwa mitandaoni au zipi hazifai manake hujui lolote kuhusu mambo kama haya ...wew kwako unaona kila kitu ni siri

Unachobaki ni kuleta ramli tu mara una viashiria vya uropokaji mara sijui nin ,ukiulizwa kosa liko wapi huna cha kusema, haya mambo hata kwenye majarida ya jeshi yapo ni free knowledge ambayo mtu yyte akijua ni muhimu manake pia inagusa history ya jeshi... Ungekuwa unajua Siri za jeshi ni zipi na zinahusisha nin usingekuwa unaishi Kwa kuogopa na basi ungekaa kimya na kunipongeza navyotoa ufafanuzi kuliko kudhiirisha level ya ujinga wako kama unavyofanya....
 
Ule utaratibu kwa upande wangu sio mzuri kwa sababu unamlazimisha Rais kumteua mkuu wa majeshi hata asiyemtaka.
Pia ni rahisi sana watu kufanyiaba hujuma.
Vilevile unaweza sababisha mtu mzuri kukosa nafasi kwa sababu sio zamu ya kamandi yao kutoa CDF.
Kwani uchaguzi wa CDF unaangalia tu mtu unayemtaka? Kuna mengi mno kupata mkuu wa majeshi siyo kama ambavyo unataka kusema. Sijaandika kukurupuka
 
Kwanza kwa Tanzania, ni vigezo gani hutumika ktk kumteua mtu Mwanajeshi kuwa Mkuu wa Majeshi(CDF)?? Je, uchawa haupo kabisa kwenye vigezo vya kuweza kuteuliwa kuwa CDF hapa Tz?

Jaribu tu kufikiria, kama Paul Makonda na umbumbumbu wake pamoja na uhalifu wake alionao ameweza kuteuliwa kushika nyadhifa kubwa kubwa hapa Tanzania Huku wakiachwa watu wengine wengi ambao ni Wasomi, waadilifu na weledi, Je, inashindikana nini kumteua CDF kwa kufuata utaratibu kama huo ambao unaulalamikia????
Kwenye mambo ya usalama hakuna uchawa bali kule ni vigezo stahiki ndio vinavyofanya mtu achaguliwe
 
Utaratibu wa kupokezana ndio mzuri zaidi, una hakikisha mkuu wa majeshi na wakuu wote wa kamandi wanapatikana kwa merit na ndio itaratibu unaotumiwa na nchi nyingi zilizoendelea na ambazo majeshi hayachanganywi sana na siasa.
Vigezo sio kupokezana tu kama mnapokezana jeneza kwenye msafara viko vingi.Kenya nako Kuna shida.Kuna generali siku za karibuni tu alipelekwa Kongo kwenda kuongoza operation ya Majeshi ya Kenya kupambana na M23 akakimbia vita analalamika kuwa wanataka M23 kumuua akarudi Kenya .Sasa alivyoenda vitani alifikiria Nini kule anaenda kucheza mziki au?

Mkuu wa Majeshi huchaguliwa pia Kwa kuangalia uwezo wake kivita je alishawahi ongoza operation ngapi za kivita na zikafanikiwa? Kwenye eneo lake? Kuna vyeo aweza panda Kwa kikawaida tu kuwa umefanya kazi miaka hii na kuhudhuria Kozi au elimu shika.Cheo .Mkuu wa majeshi CV yake kivita lazima ionyeshe mafanikio ndani na nje ya nchi anayaweza ? Umetumwa kupambana na M23 ,operation za Jeshi sijui Dafur Nk .Historia Yako kivita ikoje eneo lako la ubobezi liwe anga,ardhini,military intelligence,baharini nk kivita ukoje? Mfano nilisoma mahali Kuna makamanda wa kamandi walishawahi twangana ngumi na mwenzie wa kamandi ya anga na majini baada ya kikosi Cha majini kufanya vibaya vita ya Uganda na Tanzania kikosi kilazamishwa na majeshi ya Idd Amin Cha majini sababu ya utendaji mbovu vitani wa kamandi ya majini ziwa Victoria walipokuwa wakivuka kukabili majeshi ya Uganda yaliyovamis Tanzania na kumpa kazi ngumu ya ziada kamanda wa Anga kufanya kazi extra kuokoa jahazi

Yule kamanda wa kamandi ya majini ilibidi aondolewe vitani arudishwe kambini.Suala Sio tu ukuu wa kamandi

Pia Kuna swala la umri Unakuta mkuu mwingine wa kamandi umri unemtupa mkono anafikia ku kustaafu

Wengine Kwa kuona uzito wa hiyo kazi hugoma.Mkuu wa Majeshi Hana muda wa kulala akiwa mdogo mno sababu ni mkuu wa Majeshi yote yawe polisi,JWtZ,Usalama wa Taifa nk na wote hueakilisha ripoti kwake Kila siku na muda wowote kukiwa na swala lazima atafute Kwa maamuzi na maelekezo yake
Ndiko.maana sio rahisi Kumkuta mkuu wa Majeshi wa Tanzania mnene ila wale wa chini yake waweza Kuta wako wanene wengi tu
 
Hiv mgambo nayo n kamandi kwanza maana ya kamandi ya jeshi tuna elimu kweli
Screenshot_20240421_085954_Chrome.jpg
 
Mfano mwaka 2012 chuo cha NDC kilivyozinduliwa mkuu wake wa kwanza alitokea airforce Charles Lawrence makakala lakini alikuja kupanda cheo na kuwa luteni jenerali lakini sare zake Bado alikuwa anavaa za airforce,ila angeteuliwa kuwa Chief of staff au CDF angebadili sare na kuvaa za land force ambazo ndo kamandi mama ,aliyekuwa Mlinzi wa kikwete kamali kimario baadaye brigedia jenerali yule kamandi yake ni airforce lakini pale alikuwa akivaa barret za land force akiwa nyuma ya raisi,pia brigedia jenerali mkeremi aliyeañza Kwa kikwete 2014 Hadi Kwa magufulini 2018 ni airforce na nilijua baada ya kukutana naye akiwa na cheo cha brigedia jenerali so hapo inamaanisha basic course zake alizobobea kiutendaji vita ni za anga,japo Kwa sasa ni mkuu wa usalama na utambuzi jeshini na sare anavaa za land force
Mkeremi ni head wa MI na vipi kuhusu Maj. Gen Gaguti?
 
Back
Top Bottom