Kwanini Mkuu wa Majeshi(JWTZ)anatokea Kamandi Moja tu, wakati tuna Kamandi Sita?

Ushasema kapandishwa cheo na kuhamishiwa MMJ. MMJ ndio kamandi yake.
 
Sawa
 
Utaratibu wa Tz hautofautiani sana na huo wa Kenya.

Jwtz lina sura za Kamandi 3 za msingi, ie: Land Force, Navy na Air Force.

Namna ulivyoeleza JA, (JKT) na MMJ vyote vipo ndani ya Land Force, ingawa kiutendaji zinajitegemea.

Ukuu wa Majeshi huchaguliwa afisa yeyote mwenye sifa kutoka katika kamamdi hizo.

Ingawa Wakuu wengi wa Majeshi wametokea katika kamandi ya Land Force, lakiniJwtz liliwahi kushikwa na Mkuu wake wa Majeshi toka Kamandi ya Air Force (Rtd Gen. Robert Mboma).

Na Afisa kutoka Kamandi yoyote, anapoteuliwa kushika wadhifa wa Mkuu wa majeshi, automatick huhamishiwa Makao makuu ya jeshi(MMJ) ndipo ofisi yake ilipo.
 
Afisa wa jeshi kwenda kufanya kazi zingine za kiserikali za uteuzi kama ulizotaja hapo juu haimuondoi kwenye kamandi yake.
 
Swali zuri sana, ipo hivi, jeshi letu kimfumo na kiutendaji lipo tofauti kidogo, nadhani hili swali limeulizwa kutokana na mfumo wa Kenya ulivyo ktk kuchagua ma CDF wao, wanaotokana na KAMANDI. Sisi kimfumo ma CDF hawatokani na KAMANDI bali hutokana na kwanza wanaangalia ma senior officers kama wapo na wanakidhi vigezo dhidi ya wengine no matter vyeo vyao vinalingana hata kaka wapo 10 ambao wapo sellected, Ila huchujwa kulingana na vigezo vyao. Hapa nazuungumzia hawa ma senior officer haijalishi wapo kamandi gani iwe navy, airforce, makao makuu n.k yeyote atakae kuwa na vigezo sitahiki atapitishwa kwenye mchujo kwa sifa zao. Majina kadhaa baada ya mchujo wa awali, hupelekwa kwa rais kujadiliwa ili kujadiliwa na jopo ka kamati ya rais ikiwemo CDF anaemaliza muda wake ili kujadili na kulipitisha kina moja tu. Mchakato wa awali huanzia makao makuu ya jeshi then rais hupelekewa majina ambayo wakuu wote huyajadili kwa sifa na kuyapitisha. Ipo hivi jwtz halifuati mfumo wa kuchagua CDF kwa kufuata zamu za kamandi, kwenye kamandi ni nafasi za usimamizi hivyo senior officer yeyote anaweza kuteuliwa kuwa mkuu wa kamandi yoyote ile na inaweza ikatokea akahamishwa kamandi na kwenda operation nyingine yoyote. Ila kwenye kamandi kuna specialization. Askari wanaweza kuspecilize kwenye fani flani ya kamandi na akadumu kwa kipindi kirefu akiwa humo. Mfano airforce wapo marubani ambao ni special case ambayo ipo ktk specialization huwezi ukamwamisha askari huyu wa airforce kwenda jkt kusimamia nyanya haipo hivyo. Au umtoe askari ambaye ni senior diver wa navy umpeleke kwenye vifaru ilhali huko wapo wenye fani hiyo ambao tayari wamespecilize. Zipo kozi ambazo askari wote lazima wazipitie ambazo ni flat rate mfano infantria lazima kwenye kozi ya kijeshi upitie huko kabla ya kwenda kwenye kamandi zingine zote. Kitu pekee ambacho kipo kimfumo huwezi kukwepa kozi ya infatria ni lazima sababu ndio mfumo wa mafunzo ulivyo. Banda ya hapo ndipo utaweza kuspecilize kwenye mifumo ya kamandi. Kwa hiyo KAMANDI wakuu huteuliwa tuu kusimamia na wanaweza kuamishwa kulingana na uhitaji wa usimamizi, leo hii mfano mkuu wa kamandi ya navy anaweza akahamishiwa airforce then huko huko alipo anaweza kuteuliwa kuwa CDF kama vigezo vyake vitakuwa vimemeet requirements zote. Asanteni.
 
Kwani uchaguzi wa CDF unaangalia tu mtu unayemtaka? Kuna mengi mno kupata mkuu wa majeshi siyo kama ambavyo unataka kusema. Sijaandika kukurupuka
Sikumaanisha kumtaka kwa maana ya kwamba hata kama hana vigezo.
Nimemaanisha pamoja na kuwa na vigezo ni vema kumpata mtu ambaye hatakua na misuguano na Rais aliyeko madarakani.
 
Mkuu, vigezo vya 'seniority' vilizingatiwaje namna ya kumpata Cdf Gen Twalipo na Gen Mkunda?

Embu tupe dokezo nini kiliwafanya kupandishwa ghafla na kurukia uCdf wakati ma Senior wao walikuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…