Kwanini mtandao wa X (Twitter) unapigwa vita nchini Tanzania?

Mimi nilitegemea hao viongozi wa dini wangeanza na wasanii wa bongo fleva. Wasanii kwa siku za karibuni ndiyo wamekua namba moja kwenye kuharibu maadili kupitia mashahiri na video za utupu zinazopigwa kila uchwao kwenye luninga huku watoto wakizitazama na kuimba. Wasanii wakubwa na maarufu ndiyo geti la maadili mabovu na wanajulikana tuanze nao hao kwanza ndiyo twende huko X.
 
Nakumbuka kwenye sakata la sukari,waziri Bashe alikuwa anajibu kwa maelezo mengi kule X,lakini alikutana na nondo za watu mpaka akaonekana muongo.

Waziri kama Ummy Mwalimu,huwa anapata shida sana kule X.

Kinacho hofiwa zaidi sio maadili,bali ni uoga wa watawala wetu juu ya mawazo kinzani na yao.
 
Wasanii wengi wanaharibu watoto akiwemo harmonize,diamond ,zuchu mbona hatuoni hizo kelelelele
 
Hawataki watu wenye akili wanataka tuwe wapumbavu tunashinda insta tunabishania ujinga wakina diamond na kibushuti cha mtwara
 
Ni kwa sababu "Nani kama mama" kashambuliwa huko na kuhusishwa na mambo machafu..

Inashangaza kuwa mtu mmoja tu kushambuliwa kwa matendo yake ya hovyo, ligeuke kuwa janga la watu wote.

Tatizo siyo mtandao wa Twitter X bali matendo machafu na ya hovyo ya viongozi wetu. Wajirekebishe na waache mambo hayo. Hiyo ndiyo salama yao. Ukifunga Twitter X, uchafu wao (wizi na kufisadi mali ya umma, ushoga wao, ulawiti wao, usagaji wao nk), utatafuta njia nyingine ya kutokea na jamii ya dunia yote itajua tu!

Huwezi kuficha ukweli kudhihirika!!
 
Nchi imefunga access za mitandao ya ngono. Hivyo hiyo imegeukq kuwa portal ya kubypass mpango huo ukiacha vpn.
Point watafute namba ya kufilterna kama ni policy ya Twitter kuhimiza ngono na ushoga basi iwekwe kando kwa sababu hizo.
Hujajibu swali

Picha na video za ngono zinakuja zenyewe au mtumiaji anazitafuta?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…