Kwanini mtu wa Dar anachanganyikiwa ukimwambia unaenda kumtembelea?

Yaaah mkuu...sema sasa wakija mikoan Wana pressurize tuende tukalione jiji

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Ukiachilia mbali ugumu wa maisha kwa baadhi ya watu, budget na mengineyo lkn kubwa zaidi ni ushirikina wa watu wa mikoani hasa ndgu wanaokujua, wasisikie fulani maisha yanamwendea vzr. Watafanya Kila mbinu ili wakuangushe sasa kwa sababu uko mbali nao ulozi wao haushiki vzr hivyo watafanya Kila mbinu wawe karibu na wewe that's why tunawakataaga tunajua mambo yenu mweusi😂.

Mfano Mimi mwaka Jana mwezi wa 12 Kuna ndgu ( mama na mwanae) walikuja kunisalimia lkn Kuna kitu nilikigundua kwao, wanakua kwenye mazungumzo mazito lkn nikitokea tu wote kimya kana kwamba walikuwa hawazungumzi chochote, basi machale yakanicheza nikasema ngoja niwategeshee tape recorder nijue kitu Gani wanakizingumza seriously lkn nikitokea wote wanakula buyu???

Inshort hakuna kiumbe mbaya Dunia hii kama ndgu. Kama wewe sio mzaliwa wa dar hakuna wa kukuchezea hapa dar labda ujichanganye vya watu. Watu wasiotaka utoboe ni ndgu zako hasa sisi tunaotoka kwenye Koo za kimasikini. Washirikina sanaaaaa
 
Itakuwa walitoka swax hao.....

By the way...uligundua walizungumza nn

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
UKawafukuza??
 
Ni kweli watu wengi wa Dar hatupendi wageni kwa sababu zifuatazo:-
1.Watu wengi hatuna muda wa kukaa nyumbani,kila siku tuko bize kutokana na nature ya jiji hili,hivyo mgeni ukija ni usumbufu kwa kuwa mgeni anatakiwa apewe muda wa kuwa nae.
2.Mikoani huwa tunajipa/mnatupa status ambazo ki uhalisia hatuna kwa hiyo ili kumentain hiyo status ni bora nisikupe nafasi ya kufika kwangu
3.Watu wengi ukiwakaribisha kwa mara ya kwanza nyumbani ndio mwanzo wa mazoea ya kuja kuja nyumbani hata kama hana mpango maalumu
4.Tukija kwenu sisi ndio walipaji wa bill na mkija huku sisi ndio tunawalipia tena.(kama utanihakikishia ukija kwangu utakuwa unatoa kama mimi ninvyokutoa ukiwa kwenu mkoani..basi karibu Dar)
5.Uchawi na kurudishana nyuma...watu wengi wa mikoani ni wachawi hivyo ili kujizuia na kimbola chao ni bora wasijue nyumbani.
 
kwa sababu maisha ni magumu mkuu that's a quite reason
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…