Kwanini mtu wa Dar anachanganyikiwa ukimwambia unaenda kumtembelea?

Kwanini mtu wa Dar anachanganyikiwa ukimwambia unaenda kumtembelea?

Yaah mkuu...hata huyo cocastic ....ana udumavu wa akili .... kwasababu hyo ya malnutrition effect

Wanazalisha sana .....lakini wanakula mlo wa aina Moja[emoji23][emoji23]
Tofauti na mbeya huku
∆asubuhi ...Chai maziwa + parachichi[emoji1649]
∆ Mchana ..... kitmoto + mboga za majani + banana

∆usiku .....wali + mtindi + mboga za majani+ parachichi [emoji1649]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
😂😂😂😂😂
Sasa vyakula tunazalisha sie wenyewe, afu tusile tena?
Kunyumba kumenogaa. Tunakula kila aina ya msosi tuutakao.
 
Uko sahihi mkuu.....mfano kule songea wanazalisha sana mahindi Sasa mtoto asubuhi anakunywa uji wa mahindi ( carbohydrates)

Mchana anapikiwa ugali ( carbohydrates)

Usiku anachemshiwa mahindi ( carbohydrates)[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa mwezi mzma cycle hiiyo hiyo ya msosi wa aina Moja ....that's y vitoto vinakua na matumbo makubwa ( malnutrition, ..... kwashiorkor [emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Wee ni liongoo, Songea ipi hiyo?
Watu wanakula kila aina ya chakula huku, kuanzia ugali, wali, nyama, samaki, dagaa, maharagwe, etc.
Huoni hata aibu kudanganya, mxxxiiiieeew.
 
Ukipata muda pitia ripoti za lishe hata TNNS uko,,, sehemu nyingi wanazalisha chakula na kuuza kwaio wanakosa lishe bora inapelekea wanapata udumavu... 😂
Hapana, hili nakataa. 😂😂😂😂
 
Wee ni liongoo, Songea ipi hiyo?
Watu wanakula kila aina ya chakula huku, kuanzia ugali, wali, nyama, samaki, dagaa, maharagwe, etc.
Huoni hata aibu kudanganya, mxxxiiiieeew.
navofaham kwa walio wengi wanakula ugali maharage na mbogamboga ivo ni bei ndogo na wanaweza kuwa navyo wamelima wenyewe ila dagaa nyama na uo wali kwa wengi ni anasa hata leo hii.

kuna familia chache zenye unafaa wa maisha ndo zinakula izo dagaa nyama na dagaa.

unaweza usiamini kuna familia nyingi zinakula mlo mmoja hata leo hii yani wakila saa nane leo hii basi kula tena ni kesho iyoiyo saa nane. na iyo sio kwa songea tu hata mikoa mengine iko ivo
 
Sijakataa, hili ni nchi nzima, sio Songea pekee, ndo nachopinga hapa.
 
Miaka zaidi ya 10 nilifanya uamuzi wa mgumu wa kuhama home (chuga) na kwenda Dsm kusaka fursa. Nilidhani itakuwa rahisi kupokelewa na ndugu yangu aliyekuwa tayari akiishi Dar. Nikamtaarifu kuwa nakuja Dar akasema poa. Nikiwa hotelini Korogwe akanitumia msg kuniuliza kuwa kwake nitakaa siku ngapi... lile swali lilinikera sana nikaapa kuwa sitaenda kwake bora nilale stendi. Sikumjibu kabisa msg yake.

Nikamcheki rafiki yangu akasema poa njoo.... nimefika Ilala Boma mida ya saa 1 jioni nikamkuta jamaa kituoni ananisubiri... jamaa akaniambia nilikujibu tu nisikukatishe tamaa ila kiukweli mimi naishi chumba kimoja na shemeji yako ambaye ni mjamzito. Miguu iliishiwa nguvu ila bado msimamo ukawa siendi kwa ndugu. Jamaa yangu akaniambia ataniombea hifadhi kwa moja wa marafiki zake....

tukaanza kwenda kwa huyo rafiki aliyesema.. kufika tukakutana na kijana kanyoa kiduku anavuta sigara kama garimoshi huku uongeaji wake ukimtambulisha kama mvuta bangi mwandamizi. Yule jamaa jina lake pia lilikuwa la kisanii.. mshkaji akasema huyu ndo jamaa atakayekupa hifadhi anapoishi.... nilivunga na kujiambia hii sasa sio poa... baada ya maongezi mafupi tukamuaga jamaa na kuelekea kutafuta msosi... ITAENDELEA..
 
Wakati mwingine huwa sielewi shida ya watu wa Dar nini Kuna siku Rafiki yangu nilimwambia nakuja Dar akaniambie niletee zawadi za huko Tukuyu.

Nikanunua mkungu wa Ndizi debe la Viazi na Nyanya ndoo nilinunua Doma mbele ya mikumi kama nilitumia 60,000 kumpelekea Rafiki yangu nilikua na private Car ila nakaribia kufika nikamwambia anielekeze Nia yangu nimepekee tu hivyo vitu Mimi niende kwangu akaniambia katoka kaenda Tanga[emoji23][emoji23]

Nikawa nampigia hapokei mara Simu haipatikani baada ya siku tatu vile vitu vikaanza kuaharibika nikampigia picha nikamtumia na nikagawa kwa majirani zangu nikiwa naenda akisema niletee Michele au mafuta namwambia acha Uzushi wajinga sana hawa jamaa sijui alifikiri Mimi nataka kufikia kwake.

Je, huwa tatizo ni nini
#####HATUCHEZI###

View attachment 3338863

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Shida wengi ni fake life
 
Tatizo wakija mikoani hawasemi maisha halisi wanayoishi wakiwa dar,wanaji proud,kwahiyo ukimwambia unaenda dar lazima akukwepe maana atadhalilika
 
Wakati mwingine huwa sielewi shida ya watu wa Dar nini Kuna siku Rafiki yangu nilimwambia nakuja Dar akaniambie niletee zawadi za huko Tukuyu.

Nikanunua mkungu wa Ndizi debe la Viazi na Nyanya ndoo nilinunua Doma mbele ya mikumi kama nilitumia 60,000 kumpelekea Rafiki yangu nilikua na private Car ila nakaribia kufika nikamwambia anielekeze Nia yangu nimepekee tu hivyo vitu Mimi niende kwangu akaniambia katoka kaenda Tanga[emoji23][emoji23]

Nikawa nampigia hapokei mara Simu haipatikani baada ya siku tatu vile vitu vikaanza kuaharibika nikampigia picha nikamtumia na nikagawa kwa majirani zangu nikiwa naenda akisema niletee Michele au mafuta namwambia acha Uzushi wajinga sana hawa jamaa sijui alifikiri Mimi nataka kufikia kwake.

Je, huwa tatizo ni nini
#####HATUCHEZI###

View attachment 3338863

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Walimu wanalipwa mishahara ya laki 1 moja na nusu mpaka mbili,unategemea wasichanganyikiwe wakisikia ugeni???
 
Sijasoma uzi wote uko juu

Hivi kuna aliegusia ishu ya wa mikoani kung'ata sana sembe kama viwazijeshi?

wew ukizubaa utakuta anko wako aliyeingia jana toka kule ligangabilili wilaya mpya ya itilima ndo anamalizia vipande vya mwisho vya ule mkate wa elf 2 uliouandaa kwa ajili ya familia nzima.
 
Back
Top Bottom