Kwanini mtu wa Dar anachanganyikiwa ukimwambia unaenda kumtembelea?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sasa vyakula tunazalisha sie wenyewe, afu tusile tena?
Kunyumba kumenogaa. Tunakula kila aina ya msosi tuutakao.
 
Wee ni liongoo, Songea ipi hiyo?
Watu wanakula kila aina ya chakula huku, kuanzia ugali, wali, nyama, samaki, dagaa, maharagwe, etc.
Huoni hata aibu kudanganya, mxxxiiiieeew.
 
Ukipata muda pitia ripoti za lishe hata TNNS uko,,, sehemu nyingi wanazalisha chakula na kuuza kwaio wanakosa lishe bora inapelekea wanapata udumavu... πŸ˜‚
Hapana, hili nakataa. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wee ni liongoo, Songea ipi hiyo?
Watu wanakula kila aina ya chakula huku, kuanzia ugali, wali, nyama, samaki, dagaa, maharagwe, etc.
Huoni hata aibu kudanganya, mxxxiiiieeew.
navofaham kwa walio wengi wanakula ugali maharage na mbogamboga ivo ni bei ndogo na wanaweza kuwa navyo wamelima wenyewe ila dagaa nyama na uo wali kwa wengi ni anasa hata leo hii.

kuna familia chache zenye unafaa wa maisha ndo zinakula izo dagaa nyama na dagaa.

unaweza usiamini kuna familia nyingi zinakula mlo mmoja hata leo hii yani wakila saa nane leo hii basi kula tena ni kesho iyoiyo saa nane. na iyo sio kwa songea tu hata mikoa mengine iko ivo
 
Sijakataa, hili ni nchi nzima, sio Songea pekee, ndo nachopinga hapa.
 
Miaka zaidi ya 10 nilifanya uamuzi wa mgumu wa kuhama home (chuga) na kwenda Dsm kusaka fursa. Nilidhani itakuwa rahisi kupokelewa na ndugu yangu aliyekuwa tayari akiishi Dar. Nikamtaarifu kuwa nakuja Dar akasema poa. Nikiwa hotelini Korogwe akanitumia msg kuniuliza kuwa kwake nitakaa siku ngapi... lile swali lilinikera sana nikaapa kuwa sitaenda kwake bora nilale stendi. Sikumjibu kabisa msg yake.

Nikamcheki rafiki yangu akasema poa njoo.... nimefika Ilala Boma mida ya saa 1 jioni nikamkuta jamaa kituoni ananisubiri... jamaa akaniambia nilikujibu tu nisikukatishe tamaa ila kiukweli mimi naishi chumba kimoja na shemeji yako ambaye ni mjamzito. Miguu iliishiwa nguvu ila bado msimamo ukawa siendi kwa ndugu. Jamaa yangu akaniambia ataniombea hifadhi kwa moja wa marafiki zake....

tukaanza kwenda kwa huyo rafiki aliyesema.. kufika tukakutana na kijana kanyoa kiduku anavuta sigara kama garimoshi huku uongeaji wake ukimtambulisha kama mvuta bangi mwandamizi. Yule jamaa jina lake pia lilikuwa la kisanii.. mshkaji akasema huyu ndo jamaa atakayekupa hifadhi anapoishi.... nilivunga na kujiambia hii sasa sio poa... baada ya maongezi mafupi tukamuaga jamaa na kuelekea kutafuta msosi... ITAENDELEA..
 
Shida wengi ni fake life
 
Tatizo wakija mikoani hawasemi maisha halisi wanayoishi wakiwa dar,wanaji proud,kwahiyo ukimwambia unaenda dar lazima akukwepe maana atadhalilika
 
Walimu wanalipwa mishahara ya laki 1 moja na nusu mpaka mbili,unategemea wasichanganyikiwe wakisikia ugeni???
 
Sijasoma uzi wote uko juu

Hivi kuna aliegusia ishu ya wa mikoani kung'ata sana sembe kama viwazijeshi?

wew ukizubaa utakuta anko wako aliyeingia jana toka kule ligangabilili wilaya mpya ya itilima ndo anamalizia vipande vya mwisho vya ule mkate wa elf 2 uliouandaa kwa ajili ya familia nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…