Mkuu chanzo cha uhai ni nini?
Kwa nini swali hili ni muhimu katika mjadala wa kuwapo Mungu?
Naweza kukuambia kwamba chanzo cha uhai si huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Kwa sababu ingekuwa hivyo, hao viumbe wake anaowapenda wasingekufa kikatili kama wanavyokufa sasa.
Naweza kuwa sijui chanzo cha uhai ni nini, lakini nikajua si Mungu.
Naweza kujua square root ya 2 si 10, bila kujua square root ya 2 ni nini.
Naweza kujua mtu mwenye miaka 30 leo hawezi kuwa na mama mzazi mwenye miezi 6 leo, bila ya kumjua mama mzazi wa huyo mtu.
Sasa, mimi nakwambia huyu mtu ana miaka 30 leo, hawezi kuwa na mama mzazi mwenye miezi 6 tu leo, it is against the laws of logic.
Wewe unaniuliza, sasa kama mama yake si huyu mwenye miezi 6, mama yake ni nani?
Mimi sihitaji kumjua mama yake huyu mtu mwenye miaka 30 ni nani ili kujua kwamba huyu wa miezi 6 hawezi kuwa mama mzazi wa mtu mwenye miaka 30.