Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

haina feeling sababu technology yetu ndio ilipoishia kwa sasa, with Ai na tech kukua tunaelekea huko, sasa hivi sio siri tena DNA zetu zina binary like language, sisi tupo programed sio na herufi mbili kama Binary ila herufi 4 ama 3 etc watu wa Biology wanajua zaidi. so concept ni ile ile.
Sijakuelewa concept kwamba ukiumba kitu au kitu kikiwa chako una mandate ya kukifanya utakavyo hata ku-inflict pain ?!!!

Ukifanya hayo huku duniani tutakuita sadist.....
hio ni concept tu nakupa haimaanishi Akili ya creator ni kama yetu,
Creating something to inflict pain in my book is better not to create it in the first place...., kwahio kama ninafuga kuku na kuwalisha ili niwagombanishe kwenye kamari ni bora nisingewafuga as far as they are concerned....
 
Unamaanisha nini ukisema nadharia? Kitu kikiwa nadharia kina exist au la?
Hakiexist mpaka kithibitishwe na kuondolewa kwenye nadharia. Mfano, kuna nadharia kuwa kuna samaki aina ya nguva n.k
 
Wapo ambao hawajasikia ingawa wengi wamesikia na kukaza fuvu. Shetani anamfahamu Kristo.
Twende Logically....
Statement; Hakuna ambaye amemfahamu Kristo na Hakuguswa
Swali: Shetani Hakumfahamu
Jibu: Ndio
Swali: Kwahio aliguswa ? Au ni kipi anakijua sisi tusichokijua.... Au Statement yako ni null and void ? Au kuguswa kunamaanisha nini hasa....
 
Swali lako ni rahisi sana. Kama unadhani lifeforce inatokana na pace maker basi nenda kachukue maiti uiwekee pace maker uone kama itaanza kuishi.
Unajua vitu vinavyoitwa cell, organs, tissue, body systems n.k ?

Unaweza ukakata baadhi ya majani ya mti lakini bado uka-survive ila ukiyakata yote muda wote huenda mti ukashindwa kujitengenezea chakula hivyo kufa ila kama bado kuna uhai living cells ukachipua tena kabla haujawa brain dead kazi ya moyo ni ku-pump damu na hii kazi inaweza kufanya na artifial pumps chakula unaweza kulishwa nutrients kwa drips na only what makes you (brain ndio bado ina utata its still a struggle) wakiweza kutengeneza brain au kuhamisha brain (ufahamu wangu kwenda kwako) hapo tutaweza kuishi milele ingawa tatizo hata cells za ubongo zikizeeka zikaacha ku-regenerate na kufa ndio pale unakuta mtu/mzee anapumia ila yupo tu kama vegetable....

Mambo tuliyokuwa tunaona ya ajabu hapo zamani sasa hivi yanafanyika kuna mtu anakatika mkono wanamuwekea mkono wa bandia na bado anaweza kushika na ku-grab vitu kwa kutumia fikra tu... (zamani ungeona hayo jamaa aliyofanya hayo tungemuita mponyaji na kumuita messiah)
 
NB: Kama kuna anayeweza kunielewesha haya logically kwa kanuni za imani yake naomba tujadili (na sio kutumia kanuni za multiplication kwenye paraghraph moja na ya Pili kutumia kanuni za Addition) yaani inconsistency!


Wewe unaomba ufundishwe halafu hapohapo unaomba ufundishweje!!!😏, wewe ni mwanafunzi gani??!!
 
Wewe unaomba ufundishwe halafu hapohapo unaomba ufundishweje!!!😏, wewe ni mwanafunzi gani??!!
Naam nifundishwe with consistency sio leo jtatu naambiwa hili kesho lile, keshokutwa jingine tena mwisho wa siku tunachanganyana na sio kufundishana tena bali ni kuona vipi previous statement zinaweza kuwa justified, na ikishindikana jibu ni akili yetu Yeye muumba muweza Yote anajua atendalo.... (Hii fimbo ilitumika sana kipindi fulani kuwa-nyoosha watumwa ili waendelee kuridhika na kuwatumikia mabwana)
 
Twende Logically....
Statement; Hakuna ambaye amemfahamu Kristo na Hakuguswa
Swali: Shetani Hakumfahamu
Jibu: Ndio
Swali: Kwahio aliguswa ? Au ni kipi anakijua sisi tusichokijua.... Au Statement yako ni null and void ? Au kuguswa kunamaanisha nini hasa....
Haya mambo nimekueleza kule mwanzoni, ulikuwa unasoma ili ubishane bila kuelewa?? Nilikuambia shetani alikuwa kwenye spirit world ambayo ni perfect na alifanya dhambi bila kuwa influenced na chochote hivyo hana fursa ya kusamehewa.
 
Hakiexist mpaka kithibitishwe na kuondolewa kwenye nadharia. Mfano, kuna nadharia kuwa kuna samaki aina ya nguva n.k
Basi kama unasema mawazo sio halisia in their own form itakuwa heri ubakie kwenye five senses halafu sisi tutaendelea kuamini kwenye uwepo wa vitu beyond the tangible world. Fainali inakuja mara baada ya kuuacha mwili na kuingia upande wa pili. Kila mtu atajibu mwenyewe.
 
Hili suala tulijadili kwa Logic!

Iwapo tunaambiwa kusamehe mara sabini mara saba, inakuwaje hawa wasimalize tofauti zao sababu naona hivi vita vyao sisi nyasi tunaumia.

Okay unaweza kusema kwamba Shetani hajarepent (kuomba msamaha) ndio maana hajapewa msamaha, lakini je inamaanisha Mungu anapenda kuombwa ombwa na kunyenyekewa kiasi kwamba hatoi msamaha mpaka aombwe.

Na je, Hadithi za Mwana Mpotevu, Je inamaanisha siku Shetani akirudi na kupiga magoti atasamehewa ? Au kuna Muda wa kuomba msamaha ukipita ndio basi.

Au baada ya kukaa Motoni kwa karne kadhaa huenda ukapita msamaha kama wa wafungwa na kila mtu akawa huru na sio hawa tu ambao walijinyima bata huku duniani?

NB: Kama kuna anayeweza kunielewesha haya logically kwa kanuni za imani yake naomba tujadili (na sio kutumia kanuni za multiplication kwenye paraghraph moja na ya Pili kutumia kanuni za Addition) yaani inconsistency!
Halafu pia kwanini Mungu hadi sasa hajaamua kumsinyasinya shetani ili tuishi kama alivyokusudia??
Ina maana kakubali kuwa miaka yote hii tuishi na matatizo alosababisha shetani wakati angeweza kumshughulikia na kufanya sisi tuishi kwa amani na salama

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Biblia imesema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. Dunia iliumbwa pamoja na ulimwengu billions of years ago. Zile siku unazoona kwenye kitabu cha mwanzo zinahesabiwa baada ya tukio la dunia kuwa ukiwa na utupu.

Na kwenye theolojia inaelezeka kwamba tukio la ukiwa tena utupu lilikuja baada ya shetani kumwasi Mungu. Ukisoma kitabu cha Ezekiel sura ya 28 unaona shetani kabla hajaasi alikuwa na ofisi hapa duniani. Alipoasi ndio Mungu aliharibu dunia pamoja na ofisi aliyokuwa anaitumia hapa duniani.

Sasa baada ya kipindi fulani ndio Mungu akarudi kuanza kuweka new life kwenye dunia hii na hapo ndio zile siku za kitabu cha mwanzo zinatajwa.
Wapi hapo kwenye bible naweza nikasoma pameandikwa dunia iliumbea pamoja na ulimwengu billions of years ago?
 
of course choice yako ni vitu ulivyopangiwa, nje ya universe kuna material na vitu ambavyo hujawahi kuvisikia, kuviona wala kuvitest na mpaka kufa hutaviona, choice yako ni vitu ambavyo vipo duniani tu, ambavyo Mungu amepanga hio ni sahihi. hivyo vingine utaviona after kifo.

na hivyo alivyopanga kuna ambavyo ameruhusu na ambavyo amekataza, umepewa free will kufanya vyote, ukifanya ulivyoruhusiwa ni plus ukifanya ulivyokatazwa ni negative choice ni yako
Unachanganya concept na maswali aliyokuuliza muuliza mada...

Kuna kujua outcome kutokana na possible outcomes (hata kwenye mpira kuna draw; win au loose) kila mtu anajua....

Kujua outcome kwamba itakuwa moja bila na ni wewe ndio uliwapanga marefa na kuwapa vidonge vya nguvu baadhi ya wachezaji na baadhi kuwapa vidonge vya uzingizi ni kwamba the match is fixed (pre-arranged) and no matter mtu A atafanya nini lazima outcome itakuwa kama ilivyokuwa fixed..., na kama mchezaji wenu bora atavunjwa mguu lazima ni wewe ulimweka culprit ili amvunje mkuu ili neno litimie....

Either that au kila kitu ni happenstances na huwezi kujua nini kitakuwa nini na hata kilichotokea sasa ukikirudia tena huenda outcomes zitakuwa tofauti unless otherwise unaplan every move na sio free will ya every moving part....

Kama kuna vifo vingi Tanzania vya watoto sababu ni wazembe sidhani kama ni wewe ndio uliwapangia wawe wazembe..., au sidhani kama uliona kwamba hii dunia sasa imezidi ngoja nimtengeze hitler ili afanye yake ili neno litimie kwamba mamilioni wafe kipindi hiki sababu kitabu changu kiweze kubalance kama nilivyotabiri watakufa watu kadhaa (na kama sio wewe unaoleta hivyo vifo ni shetani) basi na wewe uliumba wengine ili wafe ili shetani afanye alichofanya at that instance.... yaani watoto kadhaa wabakwe (sababu tu free will ya mbakaji itimie)
 
Basi kama unasema mawazo sio halisia in their own form itakuwa heri ubakie kwenye five senses halafu sisi tutaendelea kuamini kwenye uwepo wa vitu beyond the tangible world. Fainali inakuja mara baada ya kuuacha mwili na kuingia upande wa pili. Kila mtu atajibu mwenyewe.
Hizi ni hisia zako zinazoendeshwa na woga wa yajayo baada ya kifo. Kwani upande wa pili ww unauthibitisha vp kuwa utaadhibu wasio waoga kama wewe? Kuna aliye adhibiwa ukamshuhudia? By the way waoga nasikia hawataiona mbingu. Ni kweli?
 
Halafu pia kwanini Mungu hadi sasa hajaamua kumsinyasinya shetani ili tuishi kama alivyokusudia??
Ina maana kakubali kuwa miaka yote hii tuishi na matatizo alosababisha shetani wakati angeweza kumshughulikia na kufanya sisi tuishi kwa amani na salama

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Niambiwa eti shetani alimuomba ampe maisha marefu ili aweze kudeal na binadamu na Mungu akasema Sawa tu endelea.... Kuna wadau wameniambia hivyo...., Who am I to Argue with People's Faith (Nachoweza kufanya ni kuvunja vunja logic zao kwa imani yao)
 
Hivi ni Wapi huu mjadala umegeuka kuwa Sisi ndio sahihi wao sio sahihi..., na kuwahukumu waislamu kwa matendo ya waislamu na sio kitabu chao nadhani ni kukosea sana...

Mtu anaweza kutumia kitabu chako akaona kuna Daudi kupenda wake za watu ni justification ya kufanya uzinzi, ndio maana hivi vitabu vya Imani inabidi uvimeze with a pinch of salt....
Simuhukumu mtu.
Ila nahukumu adhabu za Binadamu kuchinja binadamu wengie eti kwa kisingizio cha kutenda dhambi fulani wakati nao pia wanatenda dhambi pia tena inawezekana kupita wao.

Yesu alipoletewa mwanamke mzinzi ili auliwe alisema jambo moja tu.

Anayeona hajawahi kutenda dhambi awe wa kwanza kumpiga mawe huyu mwanamke.
Wote walikimbia kwa kusutwa na nafsi zao.

Kama mtu katenda dhambi mwache huyo Mungu wake atajua cha kumfanya.
 
Nafsi na roho hauzithibitishi kwa physical senses kama ambavyo huwezi kuthibitisha emotions japo zipo.
Nani kakuambia emotioms hazithibitishiki?

Role ya Amygdala ni nini

Na nani kakuambia emotions haziko physical?

Na finally ni nai kakuambia hivyo havithibotishiki mpaka utumie kama mlango wa kuingizia habari zako za uzushi (roho&nafsi) kuwa vipo?
 
Wapi hapo kwenye bible naweza nikasoma pameandikwa dunia iliumbea pamoja na ulimwengu billions of years ago?
Mstari wa kwanza wa kitabu cha Mwanzo upo clear, mbingu na nchi ziliumbwa hapo mwanzo na sio siku ya kwanza.
 
Hizi ni hisia zako zinazoendeshwa na woga wa yajayo baada ya kifo. Kwani upande wa pili ww unauthibitisha vp kuwa utaadhibu wasio waoga kama wewe? Kuna aliye adhibiwa ukamshuhudia? By the way waoga nasikia hawataiona mbingu. Ni kweli?
Mimi sina hofu, nakupa tahadhari ambayo ilitamkwa na Yesu Kristo mwenyewe juu ya hatari za kwenda kuzimu.
 
Back
Top Bottom