Nashukuru maana nimeelewa kwamba haufahamu chanzo cha uhai isipokuwa haukubaliani na kile ambacho wengine tunakikubali.
Asante.
Zaidi, suala la msingi zaidi si mimi nakubaliana na nini au sikubaliani na nini.
Siongelei habari zangu tu. Mimi kama mimi ni mtu tu, naweza kukosea.
Sipendi unijadili mimi, napenda ujadili umakini wa hoja. Kwa kuiangalia hoja, si kwa kuniangalia mimi.
Hizi hoja ninazozisema zilikuwapo kabla sijazaliwa, na zitaendelea kuwepo hata nikifa.
Kwa hivyo, naomba tujadili hoja, tusijadili mtu.
Naongelea fact, kwa mujibu wa kanuni za logical consistency.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ulimwengu ambao watu wake ambao inadaiwa anawapenda sana wanaweza kupata tabu sana, hawezi kuwepo, kwa sababu kuwepo Mungu huyo ni logical contradiction.
Mimi sijawahi kusema najua chanzo cha maisha, hiyo si hoja niliyoileta.
Mimi hoja yangu ni kwamba, Mungu hayupo, dhana ya uwepo wake ina logical contradiction sawasawa na kusema kuna mtoto wa miezi sita leo ambaye ni mama mzazi wa mtu wa miaka 30 leo.
Ni logical contradiction kama kusema kwamba katika Euclidean geometry kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara.
Ni logical contradiction kama kusema square root ya 2 ni 10.
Habari ya uhai umeanza vipi, katika mjadala wa kuwepo Mungu, ni logical non sequitur.