Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Kwanza unapaswa ukubuke kuwa hakuna claim iliyowahi kuletwa na Mungu

Si yako wala ya wengine iliyowahi kuletwa na Mungu

Ila kuna maandishi yanayodaiwa kuwa ni claim kutoka kwa Mungu, maandishi ambayo yameelezwa sehemu nyingi tofauti tofauti ambayo yote kwa pamoja hayajawahi kukubaliana.

Mfano wako wa treni unataka kuutumia kwenye hoja gani?

Unataka kuhusisha mfano wa treni na ulimwengu kuwa watu tumejikuta tupo ndani?
Yap mfano wa treni = Dunia
 
Umepata wapi mawazo haya potofu? Mungu anayo foreknowledge ya mambo yote na anayo plan ambayo kila anayeifuata anakuwa na hatma nzuri.

Huwezi kusema hapangi wakati kila kitu amekiweka yeye na anajua kila kitakachotokea...

Kama anajua kabisa mimi nina code ya hasira na kisirani na alitengeneza watu anaojua watakuja kumuua mama yangu hence kupelekea mimi kuishi maisha ya hasira na kisasi huwezi kusema hakupanga ila alijua wakati kete zote alizipanga yeye na kila kinachofanyika kwa maneno mengine ni destiny (it is written) AKA kazi ya Mungu haina Makosa...
 
Okay Je unajua hio compensation itakuwa nini au kitu gani...

Kwahio kutakuwa na matabaka yaani wenye compensation kubwa zaidi ya wengine yaani Classes tofauti tofauti ?
Kwa Imani yetu ndio kuna Matabaka ya Compensation.

Edit
Compensation ni Pepo hio Paradise, maisha baada ya kufa ambayo ni ya milele.

Kuna Hadithi ya mtume kwamba level ya chini kabisa ya pepo ni eneo mara 10 ya dunia ya sasa in terms of size.
 
Swali lako ni logical phallacy maana unahitaji kujibiwa swala la imani kwa kutumia logic how? Hebu tumia logic ku prove kwamba binadamu ana nafsi?
Moja nimeomba maelezo logically sio Proof..., Kwamba kwa kutumia premises za imani ya mtu husika anipe jibu la swali langu, ila kwenye ile premise yake (whichever she/he believes) iwe consistent na logical sound....

Mfano kwenye Movie Game of Thrones tume-set premise ya dunia ambayo ina dragons na viumbe ambao hawafi kwa normal means na wanaona future yaani ni time travelers lakini hawawezi kuvuka maji na wanakufa wakichomwa moto (Okay tumekubaliana na hio premises tuna-invest time yetu kuangalia hii tamthiliya for a good number of episodes)

Sasa mwisho wa siku wale wasioweza kuvuka maji kwenye kujikinga hawakuwekewa maji; moto ambayo ndio the main defense haukutumiwa vya kutosha, (yaani dragons ambao ndio main defense ikawa minor (badala ya kutumia cannon balls za moto za kutosha watu wanakwenda mano amano (jambo ambalo wakifa na wenyewe wanakuwa zombies) !!!! na yule anayeoona kila kitu akawa taken by surprise kuhusu kifo chake akauliwa

Hence kwenye premises tuliyowekeana kwenye hii story mwisho wa siku ilikuwa naina logic yoyote (yaani kama umeweka premises ya statement fulani kwamba ni hivi haiwezekani ubadilishe kanuni for your convinience) conclusion ni kwamba unachosema hakiwezi kuwa kweli by using your own statements
 
Kwa Imani yetu ndio kuna Matabaka ya Compensation.
Na unahitaji kufanya nini ili uwe don wa kule peponi yaani na the lowest of the low watafanya nini ? Na sio sio more efficient kuliko sisi kufanyishana kazi wale walioko motoni ndio wawe wafanyakazi wetu, na kama we can anything magically why work at all kwenye isiwe bata baada ya bata ?!!!
Edit
Compensation ni Pepo hio Paradise, maisha baada ya kufa ambayo ni ya milele.

Kuna Hadithi ya mtume kwamba level ya chini kabisa ya pepo ni eneo mara 10 ya dunia ya sasa in terms of size.
Na kwa watu ambao monetary / materialistic world haitusumbui unatuweka wapi kama Yesu mwenyewe alikuwa na Punda wakati angekuja na farasi huoni kwamba hapa rules of the games zitabadilika kwanini tusi-practise kuendesha farasi tokea huku kitaa....
 
Mimi pia huwa najiuliza hilo swali kwanini Mungu alimuumba shetani na kumpa freewill ingawaje alijua (sio kwamba aliprogram) kwamba atakuja kuasi. Hapo kwa maoni yangu kuna hekima ya Mungu iliyopo juu sana ambayo bado hatujaifahamu.

Kwahiyo kimsingi Mungu anafahamu yatakayotokea mbeleni lakini sio necessarily kwamba yanayotokea ni mambo aliyoyapanga.
Ngoja nikupe mfano mdogo wewe ukiweka sumu ndani kwako (na sio kwamba mbolea ambayo inaweza kuua lakini pia inarutubisha mazao!!! / Hapana sumu ambayo its only thing ni kuua) huoni kwamba ni kama kutega mtego wa panya ? Na mbaya zaidi kama unajua kabisa mwanao huwa mdokozi na atakula ile sumu, unaweza kuniambia haukupanga kumuua ?

Kumbuka katika hizi happenstances hizi kete zote zipo kwenye mchezo mmoja yaani matokio yanarelate...., kwahio kuna wengine ambao wapo kwenye game ili kusababisha wengine wapotee.., Ukikubali kwamba Mungu anajua kila kitu kitakachotokea na kila kitu amekiweka yeye basi tukubaliane tu logically ni kwamba alipanga yatakayotokea na wengine ufanye nini au usifanye nini your destiny is written and your doomed... (na nyie mnaohubiri hamfanyi kumuokoa mtu yoyote yule bali kujiandikia ticket nzuri kwamba nilikuwa mtu mwema ili mkale bata huko mbeleni) Kwahio sio necessarily watu wazuri bali mna hidden agenda na mnawatumia waumini kama ticket ya kwenda peponi
 
Hili suala tulijadili kwa Logic!

Iwapo tunaambiwa kusamehe mara sabini mara saba, inakuwaje hawa wasimalize tofauti zao sababu naona hivi vita vyao sisi nyasi tunaumia.

Okay unaweza kusema kwamba Shetani hajarepent (kuomba msamaha) ndio maana hajapewa msamaha, lakini je inamaanisha Mungu anapenda kuombwa ombwa na kunyenyekewa kiasi kwamba hatoi msamaha mpaka aombwe.

Na je, Hadithi za Mwana Mpotevu, Je inamaanisha siku Shetani akirudi na kupiga magoti atasamehewa ? Au kuna Muda wa kuomba msamaha ukipita ndio basi.

Au baada ya kukaa Motoni kwa karne kadhaa huenda ukapita msamaha kama wa wafungwa na kila mtu akawa huru na sio hawa tu ambao walijinyima bata huku duniani?

NB: Kama kuna anayeweza kunielewesha haya logically kwa kanuni za imani yake naomba tujadili (na sio kutumia kanuni za multiplication kwenye paraghraph moja na ya Pili kutumia kanuni za Addition) yaani inconsistency!
Swali lako ni fikirishi! Ngoja nijaribu hivi.
Kwenye spritual life, Kuna timing mkuu.Hata wewe ukifa kabla hujatubu dhambi zako,hauna tena chance ya ku-negotiate(japo kuna baadhi ya dini zinasema inawezekana kumuombea marehemu toba,sijui maandiko wanayotumia).Ila kwa jinsi ya maandiko matakatifu (biblia takatifu) usipoweza kutengeneza mahusiano yako na Mungu ungali hai,hakuna chance tena ya kufanya hivyo mara baada ya kufa . So it is too late kwa Shetani kuomba toba.kitendo cha shetani kufukuzwa,ilikuwa ni spritual death kwa shetani.Ndiyo maana anachosubiri ni hukumu tuu.

Pia tukumbuke kwamba Mungu na Shetani hizi ni Kingdom mbili tofauti zenye mamlaka kamili(Ijapokuwa Mungu ni mkuu) bado shetani anweza fanya copies ya mambo ya Mungu kudanganya watu.Again,fahamu mpaka sasa Shetani mwenyewe anajiona hana kile cha kumfanya aombe msamaha kwa sababu ana mamlaka kiasi anaona mambo yake yako on-track na pia ana watu wafuasi kibao nyuma yake.So akiweka chini siraha watu wake watabaki wapi by now? ikiwa tuu kuiunganisha simba na yanga kuwa yanga ni ngumu kuliko hili,au angalia kinachoendelea sasa Urusi na Ukrane kama haiko rahisi kwa ukrane kuachia nchi si zaidi sana kwa shetani?.Au ulikuwa unamanisha Mungu aseme sawa bwana shetani,mimi nimeamua kuwa chini yako sasa?

Mwisho kabisa,Mungu ametoa uhuru wa kuchagua unachoona kinafaa,ila ametoa angalizo juu ya mwisho wa kila njia utakayoamua kuiendea.

Ubarikiwe
 
Mkuu hausomi kabisa post zangu anyway i will wait
Kuona post moja baada ya nyingine ni kazi kwahio takuwa nazijibu as I go along ila na mara nyingine najitahidi kupitia post kwa post kama jibu mtu ashakujibu na lipo sawa na mawazo yangu nadhani itakuwa poa katika huu mjadala.., Anyway ngoja tuendelee
 
Na unahitaji kufanya nini ili uwe don wa kule peponi yaani na the lowest of the low watafanya nini ? Na sio sio more efficient kuliko sisi kufanyishana kazi wale walioko motoni ndio wawe wafanyakazi wetu, na kama we can anything magically why work at all kwenye isiwe bata baada ya bata ?!!!

Na kwa watu ambao monetary / materialistic world haitusumbui unatuweka wapi kama Yesu mwenyewe alikuwa na Punda wakati angekuja na farasi huoni kwamba hapa rules of the games zitabadilika kwanini tusi-practise kuendesha farasi tokea huku kitaa....
Mitume walikuwa tofauti na kila mtume ameleta mafundisho tofauti na wote wameonesha njia mbalimbali.

So yesu anaweza kuwa na Punda ila Suleiman akawa ni Tajiri kushinda mtu yoyote, nothing wrong kuwa Materialistic na kutafuta vizuri.

Sisi Uisilamu tumekatazwa kuwa Watawa ama kuabudu muda wote, unatakiwa ujimix na vitu tofauti tofauti.

Na ili uwe Don peponi inabidi ufuate guidelines za huyo alieitengeneza hio pepo.
 
Ukishaukubali uhalisia wa vitu abstract beyond the five senses basi hauna sababu ya kupinga uwepo wa ulimwengu wa roho.
And how do you make this weird connection!!!! Kwahio nikubaliane na chochote kile cha kufikirika pia ?, Kwanini Nikubali Uwepo Wa Mungu wa Abraham na sio wa Mwanamalundi au Mizimu ya Babu zangu au Krishna wa kule India au chochote kile ?
 
Mitume walikuwa tofauti na kila mtume ameleta mafundisho tofauti na wote wameonesha njia mbalimbali.
Kwahio njia zipo mbalimbali ili twende sambamba nadhani tungejikita kwenye Imani yako na sio imani nyingine ili tuondoe mkanganyiko huu
So yesu anaweza kuwa na Punda ila Suleiman akawa ni Tajiri kushinda mtu yoyote, nothing wrong kuwa Materialistic na kutafuta vizuri.
Sijasema kuwa materialistic ni mbaya ila nimekwambia kuna watu sio materialistic kwahio hio reward ya hekari sijui ngapi au percent ngapi kwao ikawa ni usumbufu wala hawahitaji hivyo vitu (kuna watu wanapenda kuishi simple na kwao inaumiza kuona matabaka kwanini mimi niwe na kumi wakati mwingine ana nusu ? (in short different strokes for different folks)
Sisi Uisilamu tumekatazwa kuwa Watawa ama kuabudu muda wote, unatakiwa ujimix na vitu tofauti tofauti.
Hata kama hupendi hivyo vitu ?, Nadhani kama pia mola ndio amekuumba na tabia ya kutopenda kujimix au umezungukwa na wanafiki basi sio kosa lako usipopenda kujimix... (ingawa mimi nasema hizi ni tabia za mtu anazozipata baada ya kuzaliwa kutokana na mazingira) binadamu anazaliwa akiwa a blank slate (Tabula Rasa)

Na je wale wanaoamini reward yao itakuwa mabikra sijui wangapi (hawa mabikra wamefanya kosa gani hadi destiny yao iwe kiburudisho cha wengine)?
Na ili uwe Don peponi inabidi ufuate guidelines za huyo alieitengeneza hio pepo.
 
Nani alikwambia Shetani (Shetty) anataka suluhu??🤣🤣🤣

Kimaandiko Shetani alishahukumiwa kitambo ni suala la muda tu Mungu kuja kutekeleza hukumu yake ya kumuondoa huyu kiumbe mtata Shetty

Hivyo hakuna nafasi ya wao kukaa meza moja kupatana

Na ndio maana kwa sasa akijua ana kipindi kifupi anazidi kutaka kuwaangusha watumishi wa Mungu.

Na anachochea kila aina ya uovu na ushenzi ili siku ya hukumu aondoke na wengi
Wakati Mungu anamtengeneza na baadae Shetty akawa rafiki yake, alijua kwamba kuna siku Shetty atafanya aliyoyafanya ?

Na Mungu alivyotoa msamaha kwa mwanadamu na kuleta mwanae wa pekee (kama wewe ni wa imani hio) alijua kwamba baadae atatoa msamaha au huwa anahukumu tofauti tofauti za muda mfupi baadae anasamehe na nyingine ndio imetoka ?

Pili alivyoleta gharika kusafisha ulimwengu wale walionda na gharika tutakuwa nao Peponi au nao ndio hivyo tena moto ushawamaliza (hata wale watoto makinda)
 
Kwahiyo kipimo chako kinapima nini ikiwa hakitayang'amua mawazo specifically?
Hivi mawazo specifically ni nini ? Unaweza kunipa mfano unajua hapa watu huenda tukawa tunabishana kutokana na utofauti wa lugha au anachomaanisha mwingine huenda mimi naongelea stafeli wewe kumbe upo kwenye biringanya !!!
 
Kanuni za logical consistency zinaonesha uwepo wa Mungu bila kuacha mashaka yoyote. Ulimwengu wote unaendeshwa kwenye kanuni za ulandano ndio maana tunao uhakika ikifika usiku lazima pia asubuhi itakuja.. nk

Hapa umeongea kama vile Mungu ni jamaa fulani mdogondogo. Hapana. Mungu ni mkuu na anao uwezo wa kufanya chochote na kwa namna yoyote anayojisikia bila kuhojiwa na yeyote. Mungu aliamua kuweka freewill na ndio chanzo cha mabaya kudhihirika.

Kwanini haujishughulishi kujua chanzo cha uhai? Au niseme kwanini hautushirikishi chanzo unachofikiria wewe wakati unapinga vile tunavyokupa?

Hapa sio kweli. Zaidi ya asilimia 95 ya wanadamu ulimwenguni pote wanaamini katika aina moja au nyingine ya miungu na imani hizo zimejitahidi kuhusisha mungu wake na uwepo wa uhai.

Itashangaza kama utajadili Mungu bila kujadili chanzo cha uhai maana concept nzima ya mungu inahusiana na uwepo wa uhai beyond the physical world.
Naona umeamua kuunganisha tu maneno ili yafanye sentensi and then paragraphs..., ukiulizwa kwanini jibu because I said So!!!!

Kuna wengine walisema Muafrika ni inferior kwa watu weupe kwahio tumfanye awe mtumwa.., sijui na wenyewe tungeamini tu sababu wamesema tungekuwa wapi sasa hivi...

Dunia ingeendeshwa kwa kanuni unazotaka leo tungekuwa bado tuna Noblemen na Slaves na huenda Taifa Teule Israel (according to imani yako) ndio wangekuwa wanatutumikisha na sisi tunawatumikia...

Ama Kweli Okwonkwo will be turning in his grave (according to Imani ya Character wa Chinua Achebe)
 
Okay...

Kwa minajili hio unaweza kusema baba afanye chochote kwa mwanae sababu alimzaa au wewe unaweza tu ukafuga samaki ili uwape sumu ufurahie wanavyokosa oxygen (sababu tu uliwapa chakula na kuwatotoresha) ingawa sisi wa pembeni tutakuita sadist

Ndio maana sitaki na nikaona nikuulize kwanini wasiyamalize ili shetani aache hii recruitment ?, sababu choices zilizopo huenda bado zinakufunga.., kama hutaki A wala B na hakuna C (non existent in the first place) hapo umepewa a raw deal....
achana na shetani, tuanze na wewe kwanini usimalize tofauti yako na Mungu..?
 
Kwahio njia zipo mbalimbali ili twende sambamba nadhani tungejikita kwenye Imani yako na sio imani nyingine ili tuondoe mkanganyiko huu
Imani yangu ni kuamini mitume yote, so ipo kwenye imani yangu bado
Sijasema kuwa materialistic ni mbaya ila nimekwambia kuna watu sio materialistic kwahio hio reward ya hekari sijui ngapi au percent ngapi kwao ikawa ni usumbufu wala hawahitaji hivyo vitu (kuna watu wanapenda kuishi simple na kwao inaumiza kuona matabaka kwanini mimi niwe na kumi wakati mwingine ana nusu ? (in short different strokes for different folks)
Tukiwa peponi kuna vitu vitaondolewa kwenye Miili yetu, so unachopenda hapa na utakachopenda kule sio lazima viwe sawa.
Hata kama hupendi hivyo vitu ?, Nadhani kama pia mola ndio amekuumba na tabia ya kutopenda kujimix au umezungukwa na wanafiki basi sio kosa lako usipopenda kujimix... (ingawa mimi nasema hizi ni tabia za mtu anazozipata baada ya kuzaliwa kutokana na mazingira) binadamu anazaliwa akiwa a blank slate (Tabula Rasa)

Na je wale wanaoamini reward yao itakuwa mabikra sijui wangapi (hawa mabikra wamefanya kosa gani hadi destiny yao iwe kiburudisho cha wengine)?
Unamaanisha Houri sio? Hili ni suala ambalo linataka elimu kidogo, sababu hadithi nyingi zinakuwa classified kama Dhaif zinazoelezea.

Ila pia Houri sio mabinti wa hapa duniani, ni another type of creation ambayo ni special kwa ajili ya pepo tu.
 
Back
Top Bottom