Kwanini Mwamposa asiende kwenye mahosiptali kuombea wagonjwa na tukaona wanapona?

1. Roho mtakatifu ni Nini? Na anabidi awe na mazingira gani? Au hapendi harufu ya dawa?
2. Usitumie kigezo Cha hekaya za dini coz kila dini inazo na kila dini inawaponyaji according to Mungu wao so Kuna Mungu wangapi asa...na usiseme Mungu ni mmoja kisa dini mbili unazoziona mtaani kwenu dini zipo kibao na zote watu huhisi kuponywa..
Vitu vingine penda kufikiria achana na hisia za uwoga, ujinga na matumaini
 
Kwani hazifati...mbona unaongea upuuzi...mabank hayafati watu mtaani maofisini kujitangaza?... umezingua kichizi Bora ungetumia mfano wa daktari hapa umebugi
Rudia kusoma jumbe yangu vizuri kwa umakin
 
Pana Mungu na miungu u God and goodness.
Mungu ni mmoja The Creator.
Roho Mtakatifu ni uwepo wa Mungu ndani ya mtu ni Ile sauti ikuonyayo kuhusu mabaya,thus mwenye Roho Mtakatifu uogopa kufanya mabaya yaani hofu ya Mungu,kama hauna kwako dhambi ni kawaida tu
 
Penye ngano magugu hayakosi
 
Sawa
 
Kutakuwa na conflict of interest hospitali sio sehemu ya kupona TU pale Bali kuna biashara ya dawa inafanyika pale.
Unaweza pewa dawa ya kupoza Ili kesho uje tena na tena.
Muhimbili kuna kitengo cha utalfiti i.e: tiba asili ambapo atapewa kibali na wodi yake ili awaombe then madaktari wa utafiti wapitie wagonjwa wote upya kuwapima watoe majibu
 
Kwann hao wagonjwa wasiende kwa mwamposa kuponywa hadi wafatwe hospitalini.
Anayetoa na kusmba huduma ni mwamposa au mgongwa?

Hivi baada ya huyo yesu na muhamadi kuna WATUME na MANABII wengine waliozaliwa MBEYA?
Wajinga ndiyo waliwao!!
 
Kama hawataki kuyajua maandiko kwa nini wasiyajue kwa kulipishwa Hela,manabii wapo sawa kuwauzia uponyaji watu
Kwanini manabii wa Afrika/mbeya wasiombee UFISADI,UMASIKINI,UJINGA na MARADHI vinavyowasumbua waafrika vikaondoka?
 
Anaye hitaji maombi anaenda mwenyewe kuombewa huko kunako husika.
Benki zinawafuata wateja wake.

Hata watumishi wa Mungu pia wanawafuataga wateja wao pale inapobidi.
Kuna mikutano mingi ya Injiri inaandaliwa siku zote na wanaohitaji mahubiri wanashiriki kikamilifu.

Ukitaka mkopo Benki lazima wewe binafsi uende Benki kukamilisha maombi yako na Kamwe pale kwenye mafundisho Yao huwezi kuletewa pesa

Mambo ya Roho Mtakatifu wanayafahamu wahusika na wanayaamini.

Wanaohitaji maombezi wanayapata na wanaridhika. Hata huko Benki sio kila Mteja anaweza pata pesa.
Ni lazima vigezo vya kupata pesa vitimizwe.

Kuwakashifu watumishi wa Mungu ni kukosa maadili.

Wakashifuji wapo tu hata Yesu Mwenyewe alikashifiwa.

Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza, ni vema kuuliza kuliko kujifanya mjuaji.

Hakuna mtu aliyekuwa na nia ya maombezi akayakosa, na maombi hayalazimishwi.

Nenda sehemu husika, fuata vigezo utapata maombezi sahihi. Haya Mambo ni ya Kiimani na sio ya Kisayansi.

Na hata hiyo sayansi hadi leo imeshindwa kutimiza mahitaji ya Binadamu.

Haspitali zipo na kila siku vifo vinatokea huko Mahospitalini.

Je tuwakashifu Wataalamu wa afya kwa kusababisha vifo?

Ulimwengu una kanuni zake, na bado haujatoa majibu ya ustawi wa Binadamu, zaidi ya kuleta unafuu mchache kwa wachache.

Kama mtu haamini Mambo ya Dini hana sababu ya kusifu au kukebehi Mambo ya Dini.
 
Anayetoa na kusmba huduma ni mwamposa au mgongwa?

Hivi baada ya huyo yesu na muhamadi kuna WATUME na MANABII wengine waliozaliwa MBEYA?
Wajinga ndiyo waliwao!!
Mitume na manabii wapo hadi kesho,elewa kwanza nini maana ya mtume Nini maana ya nabii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…