SimbaMpole123
JF-Expert Member
- Apr 23, 2023
- 5,501
- 4,956
1. Roho mtakatifu ni Nini? Na anabidi awe na mazingira gani? Au hapendi harufu ya dawa?Kuombea watu ili wapate afya ni agizo la Yesu Kristo kiongozi wa kanisa.
Aya Zipo.
Swala kuombea wagonjwa haliji tu haraka haraka au kwa mapenzi ya muombeaji.
Hamjiulizi tu, ni kwanini hakuna Nabii wala Mtume aliyewahi kwenda Hospitali kuombea Wagonjwa kwenye hivyo vitabu mnavyoviamini ?
Mnaosema hivyo ni kwamba hamyaamini Mambo ya Imani wala Dini.
Hali inayo pelekea kuwatukana watumishi wa Mungu kila kukicha, wawe wanaombea au hawaombei nyie kila siku kazi yenu ni kupinga, Hakuna Mungu, Dini ni utapeli, flani ni mwango Nk.
Watumishi wengi katika hali yoyote ile wanaisaidia jamii fulani kuacha matendo maovu na kuwapa nafuu ya kisaikolojia.
Ki Imani ya Kikristo kuombea hakuji kwa mapenzi ya Muombeaji Bali ruhusa ya Roho Mtakatifu.
Hivi mmejiuliza kuwa.
Je huko Hospitali kuna mazingira ya Uwepo wa Roho Mtakatifu?
Je Roho Mtakatifu amemruhusu Muombeaji akaombee watu Mahospitalini?
Je hao wanaotaka kuombewa wamefanya juhudi yoyote ya kuhitaji maombi toka Imani fulani na wakashindwa hadi wafuatwe walikolazwa?
Kwa Imani ya Kikristo Kiongozi wao Kristo mwenyewe alishawahi kuombea wagonjwa Mahospitalini?
Au Musa au Paulo au Elisha?
Kama sio ni kwanini musiwaulize wao kwanza ?
Kama hao watumishi hawaendi kuombea watu Mahospitalini Nendeni nyie mkawaombee huko Mahospitalini.
Kumbukeni kuwa hata akina Gwajima pamoja na ujinga wao mwingi lakini wamesaidia Maelfu ya watu kutenda wema, na kustawi na Kuokoka.
Hivyo kila mtumishi wa Mungu ana mchango mkubwa kwa jamii husika, hivyo anastahili heshima hata ndogo tu kwa hiyo kazi.
Nyie wapinga Dini na Imani endeleeni tu na Kauli zenu za kupinga Dini inatosha.
Na sio kuanza kusema wapi panahitaji maombezi na wapi hapahitaji.
Kazi ya kuombea wagonjwa sio ya kula chapati na Maharage na kushiba na kuanza kuongea ongea pumba.
2. Usitumie kigezo Cha hekaya za dini coz kila dini inazo na kila dini inawaponyaji according to Mungu wao so Kuna Mungu wangapi asa...na usiseme Mungu ni mmoja kisa dini mbili unazoziona mtaani kwenu dini zipo kibao na zote watu huhisi kuponywa..
Vitu vingine penda kufikiria achana na hisia za uwoga, ujinga na matumaini