Kwanini mwanamke mwenye miaka 30+ asiolewe?

Kwanini mwanamke mwenye miaka 30+ asiolewe?

Ifike muda serikali ikemee hawa wajinga, kutwa tunahangaika na wagonjwa wa afya ya akili sababu ya watu kama hawa, neno lako moja linaweza kumuharibia mwingine maisha yake,
Shame!
usijivue shuka serikali ndio wananchi na ndio hao wanasaikolojia, mainjinia n.k
 
Kwanini watu mnapenda kuwahukumu watu kwenye mambo yanayohitaji maamuzi na utashi wa wengine kuweza kufanyika......

Ndoa ni maamuzi ya watu wawili ili kuweza kukamilika kwayo na sio maamuzi na utashi wa mtu mmoja......

Inawezekana upande mmoja ukawa tayari lakini upande mwingine usipate ushirikiano......

Unaweza kuwa unahitaji kuolewa au kuoa lakini kwa muda huo pasiwepo mwenye kukufaa kwa mujibu wa vigezo vyako vya misingi kwanini iwe dhambi kusubiri.......

Mambo kama haya ndio yanasukuma watu kufanya machaguo mabaya kwenye muunganiko muhimu kama wa NDOA na matokeo huwa ni wenye kujutia........

Katika hali ya kawaida kimaumbile mwanadamu aliyekamilika anamuhitajia mwanadamu mwenzie kwenye maisha yake lakini kwa bahati mbaya huwezi kuisoma nafsi ya mtu kuwa anakuongopea au mpo pamoja maana waongo, walaghai na watu wema huongea lugha moja......

Wapo waliokaa kwenye mahusiano yaliyochukua miaka mingi lakini ghafla wenzao wakaoa au kuolewa na wengine bila kujali muda waliowapotezea wenzao......


Wakati mwingine ndoa ni kama ridhiki tu ambayo mola anamuandikia mja wake.....

Hatuwezi wote tukaoa au kuolewa kwa wakati mmoja kwani watu tunatofautiana mitazamo hali za kimaisha na mazingira......

Haya masuala ya kutoa hukumu ya pamoja kwenye masuala nyeti na ya faragha yanawafanya kupatwa na misongo ya mawazo......

Hatuwezi kurudisha wakati nyuma lakini tunaweza kuziboresha nyakati zetu zilizopo kwa kuyapanga mema yajayo......

Sasa mtu amefikia miaka 30 hajaolewa ndio afanye nini....ajiue....??....ajirudishe utotoni.....??
 
Amewaona hao wanawake lakini?
d84143354770c96f482cee14029bceb1.gif
 
Kwa jinsi wanawake wakifikisha miaka 30 wanavyoonekana wamezeeka hapo mwanasaikolojia ana hoja ya msingi na concrete evidence ya kuitetea hoja yake
 
Back
Top Bottom