Kwanini mwanamke wa Kiislam kuwa Rais ni kukiuka nguzo za Uislamu?

Kwanini mwanamke wa Kiislam kuwa Rais ni kukiuka nguzo za Uislamu?

Swali la uelewa,

Kwa nini mama wa kiislamu kuwa rais ni kukiuka mafunzo ya Mtume Muhamadi?

Huu ni uelewa tu, kwa hiyo tujengeane uwezo bila jazba wala kashfa

c.c FaizaFoxy
Ngoja tukusaidie Uislamu una nguzo tano

Nazo ni hizi, tena zinafuatwa kwa mpangilio wake, yani ya kwanza ndio ya lazima kuliko zote na tatu za mwisho mara nyingi kuna watu wanaweza wakashindwa kuzifanya kwa sababu zinazokubalika

(1) Kuamini Mungu ni mmoja, na Muhammad ni mjumbe wake

(2) Kusali sala tano

(3) Kufunga mwezi wa ramadhani

(4)Kutoa zaka

(5) Kwenda kuhiji kwa yule mwenye uwezo
 
Sasa ndg zetu Kama ndo hivyo kuna Katazo La Namna hiyo..... nini kifanyike? Semeni Wenyewe Waislamu.
Hilo linategemea kwenye kunyambua maandiko na kwenye kuangalia historia ya Waislamu, ambapo kihistoria wapo wanawake waliowahi kuongoza vizuri tu na pia wapo wasomi wakiislamu ambao huja na mafundisho yao kuwa qurani imeruhusu wanawake kuongoza,

Ni moja ya topiki zinazojadiliwa sana na wanazuoni wa kiislamu
 
ila muddy Hana shukrani kabisa...bi Khadija kamkuta jalalan kampa Hela,kamlea,kampa biashara...ila jamaa alipotoboa Tu Na kuanza kupata wafuasi akàanza kumuongezea wake mpaka 11.
Halafu kwenye kitabu chake Quran kawapondea kinoma wanawake
Soma vizuri historia uelewe, Mtume Muhammad (s.a.w) hakuona mke mwengine hadi pale Bi Khadija alipofariki, acha kupotosha, pia mtume Muhammad (s.a.w) alioa wake wengi kwasababu za kihistoria kwamba ilionekana suluhu wa kufanya wanawake wajane na mayatima wawe na watu wa kuwatunza na kuwalisha ilikuwa ni kuolewa ndio mtume (s.a.w) alioa wake zake kadhaa kwa sababu hiyo kuwa walikuwa wajane ama mayatima
 
SHIDA YA HII DINI DUNIA IMEINGIZWA CHAKA NA SHETANI.

ONA MCHANGANYIKO MWINGI WA MAFUNDISHO YA KISHETANI NA KIPAGANI.

Si Rahisi kuingia MBINGUNI kwa Hawa ndugu zetu.
 
Soma vizuri historia uelewe, Mtume Muhammad (s.a.w) hakuona mke mwengine hadi pale Bi Khadija alipofariki, acha kupotosha, pia mtume Muhammad (s.a.w) alioa wake wengi kwasababu za kihistoria kwamba ilionekana suluhu wa kufanya wanawake wajane na mayatima wawe na watu wa kuwatunza na kuwalisha ilikuwa ni kuolewa ndio mtume (s.a.w) alioa wake zake kadhaa kwa sababu hiyo kuwa walikuwa wajane ama mayatima
Nisamehe mkuu nilikosa mimi.
La ilah ila Allah, Muhammad rasul Allah
 
Swali la uelewa,

Kwa nini mama wa kiislamu kuwa rais ni kukiuka mafunzo ya Mtume Muhamadi?

Huu ni uelewa tu, kwa hiyo tujengeane uwezo bila jazba wala kashfa

c.c FaizaFoxy
Kuna maandiko katika vitabu/hadithi zinazohusika moja kwa moja na Imani hiyo, mathalani, kuna maelezo yanayofahamika/kusomeka hivi:-

"Haitengemai ile jamii ambayo jambo lao la juu kabisa la uongozi WAMEMWACHIA MWANAMKE"".

[Emphasis is added]

NB: Mimi siyo mtaalamu wa maandiko matakatifu, ila naamini wataalamu wa maandiko matakatifu kutoka upande husika watajitokeza na kuliweka sawa andiko langu hili.
 
Back
Top Bottom