Na wasiwasi na upeo wako wa kufikiri, natoa haja yangu unarudia kile kile, mimi nimesapoti utoaji wa hiyo Bikra kabla mtu hajaoa? Itabidi unilipe sasa maana nishachoka kuelekeza kitu kile kile
Oohh kumbe umeona kero ya kumuelezea mtu jambo halafu bado anarudia kitu kile kile na hata hivyo si ulisema kwamba hata mwanaume akikutoa bikira usimlaumu eti kisa hakukubaka, yani mwanaume kushawishi siyo kosa ila mwanamke kukubali ndio kosa labda niulize kwani ni kina nani wenye shida na hizo bikira za wanawake, mimi nilikuelezea kule juu kwamba mfano itokee kizazi chote cha wasiojitunza kimefutika kikaanza kizazi cha wanaojitunza tu halafu wanaume wakakosa wanawake wa kufanya nao kabla ya ndoa je unadhani wanaume watakubali kuvumilia hadi ndoa
Lakini ulivyo na uwezo mdogo wa kufikiri na kupambanua hoja ukasema eti nisiandike kitu ambacho hakina uhalisia na hakiwezi kutokea, nikakuambia kwamba hicho nilichoandika kinareflect uhalisia kwa sababu kama ungekuwa na uwezo wa kufikiria mbali, basi ungejua kwamba hata sasa hivi tukisema wanawake wote wenye bikira waanze kujitunza hadi ndoa maana yake kizazi cha wanawake ambao hawakujitunza kitaenda kitaisha
Kitabaki kizazi cha waliojitunza na hapo ndipo wanaume wa kizazi hiko watakapojikuta wanakutana na kigingi cha no sex before marriage, and mind you hapo binti kuolewa ni hadi amalize kusoma na apate shughuli ya kumuingizia kipato sababu huko tunakoelekea hakuna mwanaume atataka kuoa golikipa, na kwa mwanaume nako same thing kuoa ni mpaka amalize kusoma na apate shughuli ya kumuingizia kipato piga hesabu hapo siyo chini ya miaka 25 hadi 30 kutegemeana na level ya elimu na hali ya mtu ya maisha
Zamani iliwezekana watu kujitunza hadi ndoa sababu ndoa zilifungwa mapema binti akivunja ungo tu anaozeshwa kijana naye akishabalehe tu anapewa mashamba na mifugo kisha anapewa mke wanaanza maisha ya ndoa, ila siku hizi vijana hawataki kuoa mapema wanasingizia watakosa uhuru mara sijui mahari kubwa mara sijui mpaka wajipate na blah blah kibao, kumbe wanataka warukeruke kwanza wachezee watoto wa watu halafu mwisho wa siku wakitaka kuoa waanze kuleta unafiki wa kusema eti wanawake hawajitunzi hivyo ndio wanajifanya kuanza kutaka kuoa bikira
Sasa kwa wanaume hawa ambao wanadai wakishabalehe tu hawawezi kukaa hata mwaka bila kufanya ngono sababu ni nature unadhani wataweza kuvumilia hadi umri wa kuoa miaka 25 hadi 30 huko, maana kumbuka hapo wanawake wote wameamua wajitunze hadi ndoa kama mnavyotaka ili mkija kuoa mzikute bikira yani tufanye kila unayemtongoza ni bikira anakuambia hatoi hadi umuoe, maana yake na ninyi itabidi mkubali kujitunza na muingie kwenye ndoa mkiwa mabikira sasa swali langu ni kwamba je wanaume mtakuwa tayari kwa hilo
Sababu shida imeonekana iko upande wenu zaidi mwanamke yeye ana uwezo wa kukaa hata miaka bila kufanya ngono na asipate madhara, kwa sababu ana uwezo mkubwa sana wa kuzuia hisia za ngono labda awe anajiendekeza tu ila ninyi huwa mnasema wenyewe kwamba kukaa hata mwaka tu mtihani, mwanamke yeye ukiona amekubali kirahisi kufanya ngono ujue ameshawishiwa na kitu kingine kama pesa au mali lakini si kwamba eti hisia zimembana kiasi hiko
Kwanza kwa kawaida mwanamke hupenda kufanya na mwanaume anayempenda tu tofauti na hapo ndio kama nilivyokuambia ni lazima kuwe na kitu cha kumshawishi, kwahiyo kwa mwanamke ni rahisi sana kujitunza hadi ndoa ikiwa hajashawishiwa kwa chochote ila kwa mwanaume wote tunajua hali halisi, ndio maana nikakuuliza siku wanawake wote mabikira wakisema waanze kuweka ngumu wajitunze hadi ndoa kama mnavyotaka je na wanaume mtakubali na mtaweza kuvumilia hadi ndoa bila kuwashawishi wanawake wakubali kufanya ngono kabla ya ndoa elewa hoja