Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Wengine ni matapeli,
Anakutamanisha na Bei rahisi ila gari iko mikoani ili ukikolea anakuambia tuma hela ya mafuta uletewe Dar.

Mkuu mtu unaanzaje kutuma pesa? Mimi gari naifuata mwenyewe na naikagua mwenyewe. Tunamalizana hapo nasepa nayo

Kutuma pesa kwa mtu usiemjua unataka lawama tu
 
Mwanza ni mji wa watu wenye hela, madini, samaki, etc. Hivyo mtu akitumia gari kidogo anataka apate lingine unakuta magari mengi yapo sokoni
 
Jibu sahihi kabisa,Dar/Arusha mtu alikupa tu no. Ya mwenye Gari/ kiwanja tu nae anajiweka kama dalali tayari anafukuzia posho hapo.Ndio hua Wanapakwa Mafuta tu.Pumbavu zao
 
Hahah hii ndio dawa Yao.Safi sana mkuu.
 
Dah aiseeh hapo kuipata gari straight kwa mmiliki ndio changamoto ilipo.

Unaeza kutusaidia mbinu gani tunaweza tumia kuwakepa madalali, kumpata mmiliki moja kwa moja?

Maana unaweza kuta unaliwa zaidi ya 4m na madalali
Binafsi huwa nikipata namba ya gari huwa sihangaiki na madalali bali naangalia usajili ni nani mmiliki ila changamoto huwa inakuwepo iwapo aliyeuza mwanzo hakubadilisha jina, ila huwa kafanikiwa kuunganishwa na huyo mwenye jina lililopo kwa kadi ya gari hilo.

NB: Hii si kwa kila mtu anaweza kufanya hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…