Kwanini Mzanzibar Shaka Hamdu Shaka ni Mkuu wa Wilaya bara, na Zanzibar hakuna Mtanganyika anayeongoza?

Kwanini Mzanzibar Shaka Hamdu Shaka ni Mkuu wa Wilaya bara, na Zanzibar hakuna Mtanganyika anayeongoza?

Tunataka Tanganyika yetu.Isitoshe Jana kakimbia huko CCM kirumba.
 
Kama Kuna mtu anaweza kumjibu Lissu Video hii hapa ajibu
View attachment 2978870
Ama kweli maisha mafupi. This is IRONIC. Lissu ni yule yule. Mwenyekiti wa kikao ndiye Rais wa sasa Awamu ya 6. Lissu anasema "tusiporekebisha ... mbele ni giza tupu; ... ni vita. Na watakaoianzisha ni hao hao wanaofumba macho"!

Leo vilio vimeongezeka kuhusu "mapinduzi" yanayofanywa na Zanzibar kuiteka "Tanganyika". Bahati njema Lissu ka-survive madhila kibao na kuja kuongoza ile hoja upya. Safari hii wasikilizaji wameongezeka ikiwa ni pamoja na wale "wafumba macho"! Mlengwa mkuu ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wakati Lissu anatoa cheche kwenye Bunge la Katiba.

Kitakachoimaliza nchi hii ni ujinga, unafiki, mtazamo finyu (short-sightedness) na uroho wa watu binafsi (individuals) kujipendekeza kwa watawala ili kuambulia chochote kwa lengo tu la kuwazidi Watanganyika wenzao ukwasi.

Kwa jinsi ninavyoiona nchi hii, kwa mfano, Mkenya (asiyejulikana) mwenye pesa zake, kiswahili kilichonyooka na vipaji kibao anaweza kuhonga uongozi wa serikali na CCM akapata uraia na nyadhfa nzito huko CCM. Baadaye akapata fursa ya kugombea uRais; akagombea na kushinda (automatic) akajikusanyia machawa kibao na kuanza kutekeleza ajenda zake. Possible.
 
Hili ni swali lenye lengo la kuhitimisha Mjadala wa kero za Muungano .

Tunataka kujua kama Micheweni, Kikwajuni, Chakechake au labda Kizimkazi kama ameonekana DC yeyote mwenye vinasaba vya Tanganyika.

Maana huku Tanganyika wapo Wazanzibar waliopewa hivyo vyeo, akiwemo Shaka Hamdu Shaka ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.

Kwa Heshima na Taadhima Naomba kuwasilisha.
 
Tujue kwanza katiba ya Zanzibar inasemaje kuhusu watu wenye sifa za kuteuliwa wakuu wa Wilaya huko Zanzibar.
 
Raisi wa Zanzibar wa sasa, Dr. Hussein Mwinyi ni raia wa wilaya ya Mkuranga na baba yake aliamuru akifa azikwe Mkuranga wakaona aibu(karma itawalipa). Ila point yako imeeleweka vizuri, huu muungano ni feki hata wao wanajua tu.
 
Back
Top Bottom