Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Tanzania yetu inaelekea wapi jamani.

Kuna mwanafunzi wa UDOM alikufa kiajabu ajabu na kuhusishwa na waziri ila ikazimwa tu. Na hili pia litazimwa.

Samia hebu ingilia kati basi. Uraisi sio picha zako kusambazwa mji mzima kusifiwa, uraisi ni kusimamia haki pia. Hii imezidi sasa.
 
Pole sana ndugu.
Mazingira ya utolewaji taarifa wa huo msiba unaleta utata kuhusu alivyopata umauti huyo bintiyo (MUNGU amrehemu).

Kesi hii ukitaka kuiendea mwenyewe unaweza pata matatizo maana inavysa ugali wa watu.

Nashauri uende kweye taasisi za haki za binadamu watakusaidia sana.

Walau itarejesha nidhamu na kuwawajibisha wahusika.
 
Pakuanzia ni hapo shuleni... wafungulie kesi wamiliki wa hiyo shule... baada ya hapo... hao wengine usiwafungulie kesi za mahakamani bali unaweza kumuandikia barua moja kwa moja OFISI YA RAIS.. barua hiyo pia iende Kwa Waziri wa Ulinzi.​

Unaweza kuwasiliana na polisi kitengo cha mawalisiano kupitia namba 0787668306

au ukawasiliana na kamishina mkuu wa malalamiko DODOMA kupitia namba 0737109300

ukiona haitoshi unaweza kuwasiliana na IGP. Wambura kupitia namba 0684111111​

nimeona njia uliyotumia haitoleta manufaa...

hayo ni mapambano walio anzisha hiyo vita wakiona huchukui hatua kwa mujibu wa sheria wataona wamekuweza. pole sana kwa kumpoteza binti yako...ama kwa hakika tuna Omboleza mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi...😭😭😭😭​
 
Uko sawa kwa maelezo yake huyu kuna linalofichwa, ajali kama ajali haifichwi hivi,kuna jambo na hapo anapouliza swali binti alitokaje shule kwa ruhusa ya nani hapo ndo penyewe,, apeleleze kwa wanafunzi wenzie lazima wapo wanaoijua story,
Kabisa kipo kinachofichwa na siyo ajali, ingekua ni ajali wala hata wasingebembelezwa wasingeisikia sauti ya DC wala OCD wangepokea taarifa kutoka shuleni tu
 
Pole sana ndugu.
Mazingira ya utolewaji taarifa wa huo msiba unaleta utata kuhusu alivyopata umauti huyo bintiyo (MUNGU amrehemu).

Kesi hii ukitaka kuiendea mwenyewe unaweza pata matatizo maana inavysa ugali wa watu.

Nashauri uende kweye taasisi za haki za binadamu watakusaidia sana.

Walau itarejesha nidhamu na kuwawajibisha wahusika.
chamsingi aondoe uoga. matatizo yapo tu hata asipo ifatilia atapata matatizo mengine....kwenye jambo jingine hivyo matatizo kwenye maisha yetu hayajawahi kuisha.

usimtishe yampasa apambanie haki ipatikane na ikiwezekana tumsaidie hili sio la kufumbiwa macho.​
 
Kaombe mahakama itoe kibali cha kufukua mwili wa marehemu ili ufanyiwe uchunguzi upya

Alafu kama ni ajali mbona hawakua na sababu ya kuficha maana ajali iliyosababisha kifo siyo kuua kwa kukusudia ni manslaughter
Shida unakuta alie sababisha ajali ni mtu mzito.

Au mtoto alikua anetoka kwenda mazingira ambayo hawataki yazungumziwe.
 
Pole sana mkuu kama mzazi inasikitisha sana, tatizo humu mmevamiwa na dot. Com,na vi tiss uchwara ambavyo vinajifanya ni semi God's, nchi imepoteza heshima na adabu yake, iam afraid hii case ina kila dalili itakua ni cold case soon, kama mzazi uamua mwenyewe how to revenge ushenzi na unyama huu, kumbuka kifo cha dada Akwilina, eti risasi imeenda juu na wakati wa kurudi ndio ikamuua ,huu ni uongo wa kinyama, kama upo nje ya royal families sahau haki yako, u need to push back mwenyewe, samahani kwa hili ila ndio ukweli wenyewe, unafiki sio mwema pole sana
hamna cha uroyal family wala nini awa watu ukiwafuata fuata haki unapata mimi nakwambia...ile meseji yake ya mwanzo wengi tulizani masikhala nikiwemo mimi.

amuandikie barua mh. Rais nakuhakikishia hili jambo litaleta mkanganyiko na watafunguliana mashitaka. kwenye hiyo barua iwe ya malalamiko tu isiwe ya madai...
 
Unajua kuna bitu vingine ni ujinga na sijui uoga.

Hamjui kifo cha mtoto kimetokea vipi na mmekuta ana jeraha kwanini hamkugomea kupokea mwili na kwanini kukamzika bila taarifa ya daktari?

Mambo mengine mnawajazia watu vichwani wakati mmeshachukua maamuzi tayari.
 
mkuu sifi leo... wewe pia umefanya uzembe mkubwa saana. hujawajibika ipasavyo Kama baba , na huu uzembe wako ndo umefanya uzalishe maswari mengi ya sintofahamu.

wewe Kama baba ndo ulaumiwe . wanaume ni lazima ubakishwe 50% ya utimamu wa maamuzi sahihi hata Kama upo kwenye tatizo kubwa kiasi gani.

zaidi pole kwa msiba.
 
Kuna uwezekano mkubwa hata ilo jeraha la mguuni ilikuwa ajali ya kutengenezewa/kusababishiwa kama sehemu ya kumlazimisha jambo fulani. Malaria inayompata mtoto akiwa shule ndo imlete OCD na DC na tena waanze kupiga simu kubembebeleza mtoto arudishwe nyumbani? Na hapohapo wamteke mama wa marehemu?

Kama baba ndugu sifi leo kuna wajibu wako hujautimiza. Na ni wakati huu unatambua kuwa kuna wajibu hukuutimiza,linakunyima utulivu wa nafsi.

Hujachelewa,fata ushauri wa wataalam hapo juu ikiwemo la kuomba kibali cha mahakama mwili ufukuliwe,uchunguzi ufanyike. Si ajabu hata walimbaka na ilo jeraha akawa hata alilipata wakati anajitetea ( najaribu kufikiri tu)
 
Mkuu ni kuulize mlikubali kuzika? Kama mlikubali kuzika bila uchunguzi basi umetupotezea muda sana na akili zetu tuliotoa ushauri! Nauliza tena mlikubali kuzika? Kama mmekubali basi case closed
 
Back
Top Bottom