Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

Km kweli haya unayoongea basi hicho kifo ni zaidi ya ajali kuna mengi nyuma ya pazia.
anyway

Hapa kuna jambo zito sana hatulijui.

Mtoto kakutwa na matatizo akiwa shule,shule imemualika DC na OCD wakaja kuwa wapokezi wa mama mzazi wa mwanafunzi,kibabe tu anaporwa simu.

Labda mdogo wetu aliishaanza kuwa mtumishi wa idara yenu hii ya kiwaki.nimewaza tu sina uhakika maswali ni mengi.
 
Mkuu so utafute msaada wa sheria kwa wanasheria?

Wapo wa bure pale USM, zipo NGO kibao zinatoa huduma hiyo bure.

Watumie wanasheria kuomba kibali Cha mahakama ufanyike uchunguzi.

Damu ya mtu haimwagiki kirahisi hivyo.
 
Huu utamaduni wa kufumbia macho uovo/Utendaji mbovu ndio unaiangamiza jamii.

Wazazi hamjamtendea haki kabisa binti yenu. Ilitakiwa Mgome kabisa kupokea maiti, au atleast mgome kuzika mpaka mpate taarifa za kutosha.

Kwanza tuliosoma shule za boarding tunajua mwanafunzi akifia shuleni. Ni lazima aagwe na wanafunzi wote then maiti inasafirishwa na shule kutokea shuleni ndo inaenda nyumbani.

Hili la kusafirishwa na polisi ni geni kwangu inadhihirisha kuna story imerukwa.

Kama wazazi jitahidi mumtendee haki binti yenu. Huwezi jua kapitia mangapi mpaka umauti ulivo mkuta.

Kama kuna wanasheria humu tuendelee kumpa msaada mtoa mada.
 
Ukiwa kama baba wa mtoto naomba nikiri wazi kwamba hukutekeleza majukumu Yako vilivyo Toka umepata taarifa za msiba na mpaka dogo anazikwa, how comes mnamzika mpendwa wenu namna hiyo bila kujua nini kimemsibu? Labda kama Kuna taarifa unatuficha ila kama hivyo ulivyoandika ni kweli basi hata familia ya dogo mna matatizo.
 
Tanzania yetu inaelekea wapi jamani.

Kuna mwanafunzi wa UDOM alikufa kiajabu ajabu na kuhusishwa na waziri ila ikazimwa tu. Na hili pia litazimwa.

Samia hebu ingilia kati basi. Uraisi sio picha zako kusambazwa mji mzima kusifiwa, uraisi ni kusimamia haki pia. Hii imezidi sasa.
Nchi ngumu hii. viongozi hovyo, raia nao hovyo. Hivi ina maana hamjui tatizo liko wapi? Unamwambia Samia aingilie kati wakati yeye ndiye chanzo cha tatizo? Hamuewi wapi?
 
Dawa yao ni kufungua kesi mahakamani iliuchunguzi ufanyike, pole sn mkuu
Ni kupoteza muda bure. Kuna cases nyingi za watu kufariki katika mazingira kama zimefunguliwa lakini hazifiki kokote. Tatizo ni mfumo wetu wa uongozi na dawa yake ni kila raia kudai mabadiliko. Leo ni yule, kesho ni mimi, na keshokutwa ni wewe. Kila mtu ataonja madhara yake kwa wakati wake.
 
Huu utamaduni wa kufumbia macho uovo/Utendaji mbovu ndio unaiangamiza jamii.

Wazazi hamjamtendea haki kabisa binti yenu. Ilitakiwa Mgome kabisa kupokea maiti, au atleast mgome kuzika mpaka mpate taarifa za kutosha.
ngapi mpaka umauti ulivo mkuta.

Kama kuna wanasheria humu tuendelee kumpa msaada mtoa mada.
Raia ya Bongo hakuna tofauti na nyumbu. Halafu unakuta mtu anarudia tena huko huko tena anaomba asaidie. Yaani watu wanalipwa kwa hiyo kazi lakini mpaka waombwe.
 
Ni kupoteza muda bure. Kuna cases nyingi za watu kufariki katika mazingira kama zimefunguliwa lakini hazifiki kokote. Tatizo ni mfumo wetu wa uongozi na dawa yake ni kila raia kudai mabadiliko. Leo ni yule, kesho ni mimi, na keshokutwa ni wewe. Kila mtu ataonja madhara yake kwa wakati wake.
Kuna wale watu wa haki za binadamu nadhani wapo vizuri kiasi
 
Back
Top Bottom