Natamani sana kujibu kwa Lugha rahisi ,ila changamoto kubwa ni kuwa Upo Ignorant kwenye Dini ya Uislamu....Ila Nitajibu kiurahisi ili ieleweke kama Ifuatavyo.....Uislamu haufundishi kumwaga Damu Aidha kwa vita ,au yale mambo yaliyofanyika ya kigaidi kama yaliyofanywa na kina Osama Bin Laden,au vikundi mbalimbali vya kigaidi ikiwemo ISIS ,Hamas Israel,Al Shabab na vyenginevyo ambavyo wengi huviusisha na Mwenendo wa Uislamu...Osama Bin Laden, na Makundi mengine ya kigaidi ,ni magaidi kama Magaidi wengine ambao wanafanya Ugaidi wao wakijificha nyuma ya pazia la Uislamu ,Mara nyingi Makundi haya ya kigaidi na Magaidi hawa wanafanya mauaji na kusababisha kadhia mbalimbali ikiwemo kulipua Majengo, wakisingizia Wanafanya hivyo kwasababu ni "Jihad"....Maana ya Jihadi ni kupigania Dini ya mwenyezimungu ,Jihadi kubwa katika Uislamu ,ni Jihadi ya Nafsi ,ambayo hii ni Jihadi mtu anayoifanya kwa ajili ya kuzuia nafsi yake isitende matendo maovu, kama kuiba, kuzini ,Kuua nk....Jihadi ndogo ni Jihadi ya kivita ambayo ikilazimika na kukiwa hakuna njia ya kuepusha mmoja anapambania dini yake kwa njia ya Kutumia nguvu(Vitani) pindi inapobidi mfano Vita vingi vilivyopiganwa waislamu walichokozwa na waliwekwa to the point of no return ni aidha wapigane au Dini yao iuliwe moja kwa moja na wapoteze kila kitu ikiwemo Uhai wao(Vita vyote ukisoma "Historia ya Uislamu " utaelewa na sababu zake")...Aina hii ya jihadi ni vita ya uso kwa uso ,jeshi na jeshi, sio kulipua majengo,sio kukamata watu na kuchinja ,sio kujilipua kwenye ndege,sio kulipua magorofa lahasha......Hayo ni matendo ya watu ambao ni magaidi ,na gaidi anaweza kuwa Muislamu au dini nyengine, na akifanya hivyo au wakifanya hivyo ,hata kama wote ni waislamu haimaanishi kuwa Uislamu unafundisha Ugaidi....Tuendelee ,Katika hiyo Jihadi ya Vita ,kuna sheria zipo wakati wa kupigana na baada ya kupigana miongoni mwa sheria ni Kukatazwa Kuharibu au kukata miti au njia yoyote ya kuharibu mazingira,Wanawake hawaruhusiwi Kuuliwa au kufanyiwa uhalifu wowote ,Na pindi adui atakapojisalimisha ,harushusiwi kuuliwa ....Hizo ni baadhi ya Sheria zilizopo katika vita ya Jihadi....Kwa Muhtasari huo ningependa kuhitimisha kukufungua ,kukuambia kuwa Hao Magaidi ambao ni waislam au pengine sio waislam ila wanajificha nyuma ya Mgongo wa Uislamu(Mfano hawa ISIS ni Organization inasemekana inakuwa run by American Government ,it's a propaganda, yeah lakini there must be something in it)..Kwakuhitimisha Hao magaidi mnaowaita waislamu ,though huenda ni waislam ,matendo yao wanafanya kwa Matakwa yao wenyewe ,ila Uislam haufundishi kumwaga Damu wengi wanasingizia ,"JIHADI" ,Lakini baada ya kukuelezea kwa Ufupi maana ya Jihad Utajua kuwa wako Ignorant ,hawajaelewa au wameelewa Ila Ni wanafanya Makusudi wakijificha nyuma ya Kivuli cha Uislamu.Wanafanya Hivyo na wataendelea kufanya hivyo because wanakitu cha kusingizia na Kujustify Ukatili wao ,wakidai wanafanya wachofanya In the Name of Allah and Jihad..."Na watawaaminisha Watu kama wewe kuwa Islam Teaches evil na Muslims are proud killing and bombing innocents, (Hata Atheists hawawezi fanya hiki kitu)"Nchi nyingi zenye mlengo wa uislamu au majimbo mengi ya nchi yenye mlengo wa uislamu uwa ni kitovu cha ugaidi na maeneo hayo usifika kwa kuzalisha makundi mengi ya Kigaidi.
Sisemi tu kwa sababu nasema bali nasema kwa sababu zipo nadharia nyingi zinazoonesha kuwa ni kweli maeneo hayo ukumbwa na matukio ya kigaidi ama Vita.
Hata Tanzania miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na tetesi za matukio ya kigaidi maeneo ya Kibiti na jirani na maeneo hayo ambayo kwa wingi ukaliwa na watu wa Dini ya uislamu kitendo kilichopelekea Jeshi la Tanzania kuwekeza nguvu huko Kibiti na kutokomeza ugaidi huo ambao ulikuwa umeanza kumea katika maeneo hayo ya pwani ya Tanzania. Hata kijana mmoja wa kitanzania mwenye mlengo wa Dini ya kiislamu aliwahi kukamatwa Kenya akitumikia kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab.
Ukiachilia mbali hayo, Duniani ukitamka neno ugaidi alafu ukasema tutajie dini yenye kuhusishwa na ugaidi moja kwa moja hata mtoto atakutajia Uislamu. Na hii ni kwa sababu Watu wote wanaokamatwa katika matukio hayo basi ujinasibu kama wanapigania Dini ama maslahi yao ya kidini. Ukiachilia mbali kupigania Dini au Maslahi ya Kidini. Nchi hizo hizo au maeneo hayo hayo yamekuwa yakikumbwa na Mapinduzi ya kijeshi na watu hao wakitaka kusimika dola la kiislamu.
Alikadharika maeneo hayo uwa yanakumbwa na vurugu za kivita za mara kwa mara.
Hapa Afrika ukitoa Congo DRC tu ambayo haina waislamu wengi, nchi nyingi zilizobaki zenye vita za mara kwa mara maeneo hayo yenye vita ukaliwa na waislamu kwa idadi kubwa.
Ukanda wote wa Sahel, yani kusini mwa mpaka wa jangwa la Sahara, nchi kama Sudan, Niger, Mali, Burkinafaso, Chad na nyinginezo na nchi zinazokumbwa na vikundi vya kigaidi mara kwa mara. Na ni nchi zenye uislamu mwingi na kama unavyoona zinapakana na nchi za waarabu wa kiafrika ambazo kwa asilimia 90 raia wa nchi hizo ni waislamu.
View attachment 2943395
Nigeria pia ni miongoni mwa nchi inayokumbwa na matukio ya kigaidi sana hususani Maeneo ya kaskazini ya nchi hiyo ambayo ukaliwa na waislamu wengi. Nchini Nigeria wakristo wengi wanapatikana Kusini katika majiji kama Lagos, na Abuja, na waislamu wengi upatikana maeneo ya Kaskazini mwa nchi ambayo mara nyingi majimbo ya Maeneo hayo uongozwa kwa Sheria za kiislamu, pia nadhani juzi kati katika mfungo wa ramadhani watu wa maeneo hayo walikamatwa kwa kutokufunga Mfungo wa Ramadhani na waliadhibiwa. Maeneo hayo hayo ndio kituo cha Kundi la Boko Haram na vikundi vingine vya namna hiyo.
Tukiama barani Afrika tukaamia bara la Asia ukanda ya Middle East (Mashariki ya Kati) ambapo ndiko uislamu umeanzia huko ndiko kuna vikundi vingi vya kigaidi, na karibia kila nchi ina vikundi vyake. Nadhani wengi mnavifahamu vikundi kama Hamas kilichoishambulia Israel na kuteka na kuua watu katika tamasha la mziki, na kupeleka vita ambayo imeigharimu ardhi ya Palestina ukanda wa Gaza. Vilevile haikupita miezi mingi kuna kikundi kutoka Yemen nacho kinaitwa Hauthi kikaanza kulipa mashambulizi kwa kupiga meli zinazopita ukanda wa bahari ya sham bila kujali kuwa anaepigwa ni raia wa nchi gani.
Ukiachilia mzozo huo wa Israel na maadui zake, hakuna asiyejua kundi la kigaidi lenye mlengo wa kiislamu lililotikisa Dunia kwa matukio ya kutisha kwa kuchinja, kupiga risasi au kujitoa Mhanga. Hii ya kujitoa mhanga ikapelekea Waislamu hasa waliojifunika mwili mzima kuogopwa sana kuhisi labda wamebeba mabomu ya kujitoa mhanga. Chini ya Osama Bin Laden, kundi hili liliisumbua Dunia hasa Marekani kwa kuipa Jeraha lisilosahaulika la Septemba 11.
Kwa kifupi huko Middle East (Mashariki ya Kati) kuna vikundi vingi sana vya kigaidi, vingine vinakuwaga vimelala tu, vinakuwa (Inactive) lakini viko tayari kwa mashambulizi. Na vikundi hivi ndivyo vinafanya Dola za kiislamu zinaendelea kusimama na sheria kali za kiislamu zifatwe, mfano moja wapo ni Kundi la Taliban kutokea pale Afghanistan ambalo baada ya kushika dola tu likaweka sheria kali za kiislamu ikiwemo wanafunzi kusoma madarasa kwa kuzingatia jinsia mpaka chuo kikuu yani mtoto wa kike na wakiume kila mtu darasa lake.
Kundi jingine la Kigaidi ni kundi la ISIS yani Islamic State. Kundi hili juzi kati limekiri kupiga Tukio pale Russia kwa kumimina Risasi katika Mall moja pale Moscow kwenye tamasha la mziki na kuua watu zaidi ya 150 na kuchoma jengo kwa vilipuzi. Lakini Rais wa Russia Vladimir Putin hajawaacha salama, kawadaka watu kadhaa ambao wanahusika na tukio hilo ambao wengi wao wanasema wamekodiwa kutokea nchi ya Uturuki ambayo ni yenye mlengo wa kiislamu.
Kwa ufupi makundi haya ni mengi sana na yana uhusiano wa moja kwa moja, kwa sababu mengi yanakuwa na link au uhusiano.
Kwani ndugu zetu waislamu mnapokuwa mnafundishwa Dini uwa mnapewa maelezo gani yanayowatia baadhi yenu mioyo ya kikatili, kutaka kumwaga Damu?
UKITAKA KUULEWA UISLAMU NI LAZIMA USOME NA NDIO UJUDGE ,UISLAMU HAUFUNDISHWI KWA KUJUDGE CHARACTERS ZA WATU LAHASHA ,UTALETA WRONG CONCLUSIONS...."Kasome FIQH ya Usilamu ,au sheria Katika Dini ya Uislamu au Kasome Historia ya Uislamu".......Islam means Peace ..Maadui wanapambana kuvuruga hii Peace...By the way ISLAM is the Fastest growing religion in the world currently Despite hivyo vitu vyote Ulivyongea ,Vinavyotokea na Vilivyotokea...UKITAKA KUELEWA ZAIDI PLEASE UKASOME USIANGALIE MATUKIO YANAYOTOKEA NCHI ZA KIISLAMU..