Nchi ya Uturuki, Tunisia na Iraq zimefuta kabisa ndoa za wake wengi huku Saudi Arabia ikiwa imeweka masharti makali kiasi kwamba hakuna watu wanaooa wake wengi.
Iran yenye watu milioni 88.5 ina ndoa za wake wengi zinazofikia laki moja tu. Algeria zinaelekea kupotea. Swali hapa ni kwanini hizi nchi zenye waislamu wengi hawataki kuoa wake wengi?
Kwa ufupi sana.
Uamuzi wa kuwa na mke mmoja au wengi ni uamuzi wa mtu binafsi wala hausiani na Mungu na wala sio dhambi au makosa kwa muumba.
Utamaduni wa kuoa mke mmoja ni utamaduni wa wazungu toka enzi na enzi kama ilivyokuwa kwa Afrika kuoa wake wengi.
Ajabu ni kwamba, waleta dini ya kikristo yaani wazungu walichomeka mila yao ya mke mmoja kuwa kanuni za kiimani kwa wakristo lakini soma biblia yote hakuna mahali utakuta inakatazwa kuoa wake wengi au mmoja.
Mwanamke amekatazwa kuzini kwasababu ya maumbile yake. Ndio maana kipindi cha Musa walipigwa mawe hadi kufa. Je kwanini mwanaume hakupigwa .awe?
Mwanaume amekatazwa kutamani mke wa mwenzake.
1 Timotheo 3:2
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
1 Timotheo 3:12
Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
My Take: Maoni Yangu.
Kwanini Paulo anaweka sharti la viongozi wawe ni waume wa mke mmoja pekee. Ina maana kuna wengine walikuwa na wake wengi. Walipoteza sifa za uongozi kanisani.
Kutoka 21.10-11
10 Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.
11 Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.
NB. Someni biblia wapendwa msibebeshee mizigo mizito