Kwanini nchi za kiarabu zinapingana na Quran kwa kufuta ndoa za wake wengi?


Kwamba Alizaa na Hajir kwa bahat mbaya.Vip baada ya ibrahim(Baba wa iman) kujua ni bahat mbaya alichukua uamuz upi?
 
Hiyo reference ya mfalme atakayokuletea hapa , haitoki Google?

Kuna reference yoyote hapa duniani kwenye Internet ambayo haitoki Google?
Pole sana ndugu yangu., ulisoma chuo gani na kuaminishwa habari za google ndio habari halisi
 
Kwamba Alizaa na Hajir kwa bahat mbaya.Vip baada ya ibrahim(Baba wa iman) kujua ni bahat mbaya alichukua uamuz upi?
Mungu alimwamrisha hajir aondoke na mtoto wake wa nje nyumbani kwa Ibrahim baada ya kuanza kibri kwa Mama boss wake sarat
 
Watu wanachanganya faith (imani) kwa Allah na religion (dini) mfumo wa maisha.

Ustadhi anatuweka sawa kutofautisha Imani kwa Allah na kitu kinachoitwa dini ambacho ni mfumo wa maisha wa Turkey, Saudia, Tunisia, Mdengereko wa Tanzania n.k wenye tofauti mbalimbali

 
Pole sana ndugu yangu., ulisoma chuo gani na kuaminishwa habari za google ndio habari halisi
Jibu swali nililokuuliza.

Nimekuuliza, Kuna reference yoyote hapa duniani (kwenye Internet) ambayo haipatikani Google?

Inawezekana hata hujui Google ni nini... Google is just a search engine inayo-search across all Internet resources and contents

Hebu wewe hapo nipe reference ya kitu chochote kile kwenye Internet ambacho Google haina access nacho!!
 
Siku hizi kwenye hizo nchi ulizo sema ..hakuna waislamu bali wamebaki waisiharamu tu
 
Narudia tena google sio msahafu watu wa ngapi wamekuwa wakiishtaki google na wikipedia kwa kuweka taarifa za uongo zinazowahusu, sio kila kilicho kwenye google ni kweli, taka kujua kwanza ni nani aliyeasisi google search na kwa nini asiweke taarifa zinazogongana (uongo).

Na google ndio search engine namba 1 inayoiandikia uislamu mambo ambayo hayapo kwenye mafundisho na uhalisia wake, ni vile umelala na kuamka unaikuta google na kuamini kila unacho browse kwenye google

watu wangapi wanaibiwa kwa taarifa za uongo zitokanazo na google wanaingia na kufanya miamala kwenye links za uongo za wizi zitokanazo na google?
 
Ukijua mwisho wake na hao wanne utaelewa kama aliwamudu au la h [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mwisho wake ni watoto wake wa matumbo manne kuzawadiwa Utaifa teule la Mungu na la milele.Au kuna mwisho mwingine unaoujua wewe zaidi ya huu?.
 
Kwa kujitoa ufahamu tu,mpo vizuri.

Mwanzo 25:1-5

1Abrahamu alioa mke mwingine, jina lake Ketura.2Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.3Yokshani alimzaa Sheba na Dedani; wazawa wa Dedani walikuwa Waashuru, Waletushi na Waleumi. 4Watoto wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.
 
Kwa ufupi sana.

Uamuzi wa kuwa na mke mmoja au wengi ni uamuzi wa mtu binafsi wala hausiani na Mungu na wala sio dhambi au makosa kwa muumba.

Utamaduni wa kuoa mke mmoja ni utamaduni wa wazungu toka enzi na enzi kama ilivyokuwa kwa Afrika kuoa wake wengi.

Ajabu ni kwamba, waleta dini ya kikristo yaani wazungu walichomeka mila yao ya mke mmoja kuwa kanuni za kiimani kwa wakristo lakini soma biblia yote hakuna mahali utakuta inakatazwa kuoa wake wengi au mmoja.

Mwanamke amekatazwa kuzini kwasababu ya maumbile yake. Ndio maana kipindi cha Musa walipigwa mawe hadi kufa. Je kwanini mwanaume hakupigwa .awe?

Mwanaume amekatazwa kutamani mke wa mwenzake.

1 Timotheo 3:2
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;

1 Timotheo 3:12
Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.

My Take: Maoni Yangu.
Kwanini Paulo anaweka sharti la viongozi wawe ni waume wa mke mmoja pekee. Ina maana kuna wengine walikuwa na wake wengi. Walipoteza sifa za uongozi kanisani.

Kutoka 21.10-11
10 Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.
11 Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.

NB. Someni biblia wapendwa msibebeshee mizigo mizito
 
Kasome mathayo 19, Yesu Kristo kazungumzia mume na mke mmoja. Hapo Paulo aliweka hilo agizo akitumia mafundisho ya Yesu Kristo kwasababu maeneo yale walikuwepo watu waliokuwa na wake wengi.

Mungu angetaka mwanaume awe na wake wengi basi angeumba akina Eva wengi. Pia fahamu kwamba biblia imeandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu na sio opinion za wazungu kama unavyosema.

Kama Mungu angetaka wanawake waolewe wengi angewaumba wawe wengi kuliko wanaume (kwasasa duniani wanaume ni wengi kuliko wanawake) na pia angewafanya wasiwe na wivu.
 
Hapo amesema na kusisitiza kutomwacha mke na kuoa mwingine. Vipi kuhusu kuoa mwingine nabkuendelea nao wote?
 
Waislam wanafata Qur'an hawafati nchi, bali wanatui sheria za nchi ambazo hazikutowi katika Uislam wako, yaani sheria ambazo hazikulazimishi kufanya yaliokatazwa na Uislam.

Kumbuka kuwa ndoa siyo faradhi katika Uislam. Ukioa wawili, watatu, wanne, mmoja tu, au usioe kabisa haikutowi katika Uislam.
 
"Mathayo" na "Paulo" wapi na wapi, usiseme uongo.

Takwimu zipi ulizotumia kuwa duniani wanaume ni wengi kukiko wanawake? Weka ushahidi.
 
Naona wameona hiyo ni dhambi.
 

Unaposema Wanawake wapo Wengi mara nne ya wanaume Duniani unazungumzia Data zipi au ni maoni yako Binafsi au vile unavyotaka iwe?

Data za Dunia hazionyeshi hivyo.
 
Sasa hizo habari za vijiweni sijui umetoa wapi.
Data zipo hivi;

8,078,874,970Current population
4,076,238,312Current male population (50.5%)
4,002,636,658Current female population (49.5%)
51,766,973Births year to date
 
Sababu yake nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…