Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

Kuna siku nilisoma story ya jamaa kubakwa mahabusu Hadi kufa...alikuwa anaitwa Hasara Omary..
Kila siku nilikuwa najiuliza kama jina lilichangia kumpa matatizo
Japo bado ni myth lakini si vyema kumpa mtoto majina ya aina hiyo. Sijawahi sikia mtu anaitawa ibilisi au yuda iskarioti
 
Tafiti zifanyike kama kuna uhusiano wa jina la mtoto na maisha anayokabili
 
Tafiti zifanyike kama kuna uhusiano wa jina la mtoto na maisha anayokabili
Hakuna haja ya utafiti. Yaani jina ndio kila kitu. Labda tu kuwe na utaratibu wa mtoto kuchagua jina analotaka baada ya kufikisha umri fulani.

Kwasababu tupo wengi tusiopenda majina tuliyopewa na wazazi wetu na ndio maana tunajipa majina mbadala (nickname). Kuna watu majina yao yamebeba tafsiri halisi ya maisha yao na ndivyo walivyo
 
Tafiti zitajibu maswali mengi na kutoa shuhuda zinazo thibitishwa na numbers, bado kuna haja ya kufanya tafiti
 
Nina jamaa yangu anaitwa Mgeni Kifo mtokambali

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo kumwita mtoto John, Emmanuel, Abdallah, Mohammed ni sawa.

Ila ukimwita Aishi, Tabu, Ubaya, Apendwae, Aizari, Msiba ,Nyamayao, Cha wote, Mzuri sio sahihi?

Mnajua hata maana na hayo majina mnayojifaharisha nayo?

Mimi katoto kangu ka kike nimekiita SALAMA na WA kiume Aishi akipatikana wa tatu ni TABU.
 
Huyo CHAWOTE ni mtihani
 
Wanyakyusa, Wapare na Wahaya wana majina yana maana nzuri mara nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…