Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

Amani iwe nanyi

Wakati tunakua, bado Dar es Salaam ilikua na wazaramu wengi na nilibahatika kusoma na watu wenye majina kama SIKITU, SIWATU, SIWAZURI, TABU, MATESO, HAVINITISHI, SIKUDHANI, KIDAWA, CHAUREMBO na majina mengi ya namna hiyo.

Sasa, sijui hekima ya wazee wa kizaramo ilikua ina kusudia nini?

Wakati mwingine, though it is a myth, jina linaweza kubeba au kusadifu aina ya maisha ya huyo mtoto baadae.

Watalaamu embu dadavueni
Unawashangaa wazaramo vipi wanyakyusa na mikabila mingine ya bara au kwa vile yanatamkwa kikabila? Huenda kwa Kiswahili kuna watu wanaitwa Mavi.
 
Mwazani huwa ni kifupi cha mwana wa Ramadhani kama baba yake ni ramadhani au kazaliwa mwezi wa Ramadhani kama ilivyo Mwajuma, Mwanaaly, Mwashabani , Mwanaheri, Mwanaenzi, nk.
Ila ukanda wa Pwani na kusini wanamajina ya ajabu Sana[emoji3]
 
Amani iwe nanyi

Wakati tunakua, bado Dar es Salaam ilikua na wazaramu wengi na nilibahatika kusoma na watu wenye majina kama SIKITU, SIWATU, SIWAZURI, TABU, MATESO, HAVINITISHI, SIKUDHANI, KIDAWA, CHAUREMBO na majina mengi ya namna hiyo.

Sasa, sijui hekima ya wazee wa kizaramo ilikua ina kusudia nini?

Wakati mwingine, though it is a myth, jina linaweza kubeba au kusadifu aina ya maisha ya huyo mtoto baadae.

Watalaamu embu dadavueni
Ipo hivi kama Mapambano,Zawadi,Furaha, Shida ,HAVINTISHI,CHAUSIKU, NK Basi hivyo hivyo Ulaya HAPPY,GIFT,LIVINGSTON, GODBLESS, Shida ya Bongo tumebeba uharabu na Uzungu utafikiri Kama Kwetu hatuna majina lakini ukifutilia ni Ulimbukeni wa kufuata Mila za Watu. Ebu fikiri ELLYBARICK, AMBELE,MWITA, SHUJAA, MAPINDUZI,BARAKA . AFRICA ilibarikiwa hekima Sana kabla hata ya Wageni.
Wazaramo Walitaka kila Jina liwe na maana na ndiyo wajuavyo Wazungu na Waarabu Sasa leo ni vutuko Mtoto anaitwa MACWHITE Wakati rangi yake Mtitu tii.
 
Wangoni ndo funika wana majina ya wanyama mtu kuitwa komba ,Ngedere, kenge ua Mbega ni kawaida.
 
Ni fikirishi sana, nadhani hawawazi madhara yake kwa huyo mtoto, mfano ukimwita SHIDA mtoto si anaweza pigika maisha yake yote?
Muite wa kwako tajiri au pesa ukitarajia kwamba jina ndio linaamua hatma ya mtu[emoji44][emoji44]
 
Hakuna haja ya utafiti. Yaani jina ndio kila kitu. Labda tu kuwe na utaratibu wa mtoto kuchagua jina analotaka baada ya kufikisha umri fulani.

Kwasababu tupo wengi tusiopenda majina tuliyopewa na wazazi wetu na ndio maana tunajipa majina mbadala (nickname). Kuna watu majina yao yamebeba tafsiri halisi ya maisha yao na ndivyo walivyo
Kwa Nini effects ziwe kwenye majina mabaya tu? Mfano ukimwita mwanao tajiri atakua tajiri Kwa sababu ya jina? Au ukimwita pesa msomi upendo furaha basi atakuwa na hizo sifa Kwa sababu ya jina?
 
IPO hasa kama binti alieolewa kakutana na mambo ya kishirikina ukweni lakini na yeye anajiamini Yuko fiti...ndo anawajibu "Havintishi'
Mara nyingi ni magomvi na migongano ya hapa na pale baina ya ndugu na wanafamilia ndio huleta hayo mambo na hata kwenye shughuli za ngoma huko ndio vijembe vinapigwa haswa hadi wakati mwingine watu hushindwa kuvumiliana na kuishia kupigana kabisa.
 
Back
Top Bottom