Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

Majina ya wazaramu Yana message ...
Mara nyingi yalikuwa Yana define watu walivyo hasa ukweni ..
Binti akiolewa jinsi atakavyo pokelewa ukweni ndo atakavyo toa majina Kwa watoto wake....Sikudhani...manake hakudhani Hali iko kama alivyoikuta huko ukweni ..Siwatu...manake familia ya mume sio watu...labda wanamtesa...Sikitu manake hakuna shida atavumilia Tu n.k n.k Siwazuri...,Mateso n.k mostly huwa ni mama alieolewa ana define wakwe au majirani.....wazaramo wenyewe wanajua
Ina Maana yule Mtangazaji Siwatu Luanda, yawezekana alikuwa Mzaramu?
 
Akina sinaubaya, havijawa, bahati, ...
Ni vile tu wao wanatumia kiswahili. Wengine wanatumia zaidi ya 'kilugha'

Japo ukienda usukumani wapo akina cherehani, bakuli, sahani, majaba
Kuna jamaa nilisoma naye anaitwa Tangazo Mwanza.
 
Mwazani huwa ni kifupi cha mwana wa Ramadhani kama baba yake ni ramadhani au kazaliwa mwezi wa Ramadhani kama ilivyo Mwajuma, Mwanaaly, Mwashabani , Mwanaheri, Mwanaenzi, Mwarashi, Mwadawa, Mwamtumu, Mwahija nk.
Ingekua hivyo angeitwa Mwadhani, tafuta maana ya neno mwazani kwa kindengereko au kizaramo.
 
Amani iwe nanyi

Wakati tunakua, bado Dar es Salaam ilikua na wazaramu wengi na nilibahatika kusoma na watu wenye majina kama SIKITU, SIWATU, SIWAZURI, TABU, MATESO, HAVINITISHI, SIKUDHANI, KIDAWA, CHAUREMBO na majina mengi ya namna hiyo.

Sasa, sijui hekima ya wazee wa kizaramo ilikua ina kusudia nini?

Wakati mwingine, though it is a myth, jina linaweza kubeba au kusadifu aina ya maisha ya huyo mtoto baadae.

Watalaamu embu dadavueni
Siwajibu
 
kila kona kuna majina ya hovyo mpaka kutamka ni balaa kama Mboro,nkya ,Temu,Mrosso ndo nn eti😂 siwezi kumwita mwanangu majina ya hovyo .

sijui Tabu ,Maajabu, Sikujua ,chausiku majina mengi kama hayo kweny lugha ya kiswahili tu yana ukakasi ...

Moja ya mambo mema ya kumfanyia mwanao ni kumpa jina zuri..
 
Amani iwe nanyi

Wakati tunakua, bado Dar es Salaam ilikua na wazaramu wengi na nilibahatika kusoma na watu wenye majina kama SIKITU, SIWATU, SIWAZURI, TABU, MATESO, HAVINITISHI, SIKUDHANI, KIDAWA, CHAUREMBO na majina mengi ya namna hiyo.

Sasa, sijui hekima ya wazee wa kizaramo ilikua ina kusudia nini?

Wakati mwingine, though it is a myth, jina linaweza kubeba au kusadifu aina ya maisha ya huyo mtoto baadae.

Watalaamu embu dadavueni
Hayo majina huwa yana maana hawayatoi tu, mfano kama Mimi Dada yangu anaitwa Semeni ni kwa sababu baba yetu alikuwa mweusi sana lakini Dada yangu akatoka mweupe sana sasa maneno yakawa mengi sana ndipo akapewa jina la Semeni. Na Dada yangu mkubwa anaitwa Sikujua ni kwa sababu mama yetu alisumbuliwa sana na uzazi na maneno yakawa mengi maana walimkatia tamaa kabisa lakini baadae akapata mtoto akampa jina la Sikujua. Hivyo kwa Mimi naona hayo majina kwa wao yanathamani kutokana na matukio.
 
Back
Top Bottom