Kwanini ndugu zetu wazaramu wanawapa watoto majina fikirishi?

Ina Maana yule Mtangazaji Siwatu Luanda, yawezekana alikuwa Mzaramu?
 
Akina sinaubaya, havijawa, bahati, ...
Ni vile tu wao wanatumia kiswahili. Wengine wanatumia zaidi ya 'kilugha'

Japo ukienda usukumani wapo akina cherehani, bakuli, sahani, majaba
Kuna jamaa nilisoma naye anaitwa Tangazo Mwanza.
 
Mwazani huwa ni kifupi cha mwana wa Ramadhani kama baba yake ni ramadhani au kazaliwa mwezi wa Ramadhani kama ilivyo Mwajuma, Mwanaaly, Mwashabani , Mwanaheri, Mwanaenzi, Mwarashi, Mwadawa, Mwamtumu, Mwahija nk.
Ingekua hivyo angeitwa Mwadhani, tafuta maana ya neno mwazani kwa kindengereko au kizaramo.
 
Siwajibu
 
kila kona kuna majina ya hovyo mpaka kutamka ni balaa kama Mboro,nkya ,Temu,Mrosso ndo nn eti😂 siwezi kumwita mwanangu majina ya hovyo .

sijui Tabu ,Maajabu, Sikujua ,chausiku majina mengi kama hayo kweny lugha ya kiswahili tu yana ukakasi ...

Moja ya mambo mema ya kumfanyia mwanao ni kumpa jina zuri..
 
Hayo majina huwa yana maana hawayatoi tu, mfano kama Mimi Dada yangu anaitwa Semeni ni kwa sababu baba yetu alikuwa mweusi sana lakini Dada yangu akatoka mweupe sana sasa maneno yakawa mengi sana ndipo akapewa jina la Semeni. Na Dada yangu mkubwa anaitwa Sikujua ni kwa sababu mama yetu alisumbuliwa sana na uzazi na maneno yakawa mengi maana walimkatia tamaa kabisa lakini baadae akapata mtoto akampa jina la Sikujua. Hivyo kwa Mimi naona hayo majina kwa wao yanathamani kutokana na matukio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…