Kwanini ninamdharau sana mtu aliepata mafanikio kupitia connection

Kwanini ninamdharau sana mtu aliepata mafanikio kupitia connection

Kwa miaka hii nimekuwa nikikutana na watu waliopata mafanikio au maendeleo yoyote Yale kupitia connection huwa Nina mdharau sana, na muda mwingine huwa naudharau hata ushauri wake,..akiwa anaongea huwa najisemea kimoyomoyo "huyu ataniambia nini!"

Labda mimi sijawaelewa vizuri ninyi vijana. Unamaanisha network (nyie mnaita connection) au michongo, ambayo mimi naita uhuni.
Lakini kwa upande wa network is everything. Watu hupeana dili kulingana na wanavyo kufahamu. Wanavyokuamini kwamba hutawaangusha. Hata ulaya na marekani huwezi pata kazi/dili bila mtu kuku refer. Yaani from no where una lend kwenye dili
 
Kuwa na connection pia ni asset mkuu, hata wewe ukiwa na kampuni yako zikija CV mbili zinafanana, itakua rahisi zaidi kuajiri mtu unayemfahamu au uliyepewa taarifa zake na mtu wa karibu kuliko mtu baki kabisa.

Hatufundishi soft skills, na hayo ndiyo matokeo yake. Network, communication skills, adabu/nidhamu (interpersonal skills), emotional intelligence, entrepreneurship, problem solving etc ni assets na zinahitqjika na kila mmoja bila kujali taaluma yake
Wengi wanadhani ukijua law, physics, udaktari nk inatosha. Kumbe hiyo ni core au hard skills. Wanahitaji kuwa na elimu ziada, yaani soft skills
 
Anashindwa kujua kuwa ili uweze kufanikiwa Mungu( kwa wale wa Imani) huwa analeta watu wa Hatma yako( connection) ili waweze kukuvusha kukupeleka kwenye baraka zako! Baada ya hao watu kutokea basi watakufundisha na kukuacha ujisimamie mwenyewe kwa uwezo wa Mungu.
Nimekupata mkuu eg. Mungu alimletea Ridhiwani mtu anayeitwa JK
 
Connection zipo za aina nyingi mkuu,
Kuna zinazotengenezwa kutokana na juhudi za mtu mwenyewe,hadi anakutana na watu husika.

Na kuna zile za baba mweny kampuni,mjomba yupo wizarani.
Sasa apoo unazungumziaa zipi??.
 
Ambao wamepambana na kufika walipo kwa msaada wa Mungu hawawezi kukuelewa.

Kuna kupambana mpaka unafika point unakata tamaa ya maisha, chakula hakuna, hujui unalala vipi na utaamkaje, mwisho unakuja kuona neema ya Mungu inakugsa.
Hata hizo connection Mungu hutoa. Punguzeni wivu. Hakuna ufahari kwenye kusota.
 
Back
Top Bottom