Ukiongelea tofauti ya idadi ya vitabu, moja kwa moja unakuwa unaongelea vitabu vya Tobiti, Yudithi, Hekima, Siraki, Baruku, 1 Wamakabayo na 2 Wamakabayo. Hivi ni vitabu vinavyopatikana katika Biblia ya Kikatoliki lakini havimo katika Biblia nyingi za Kiprotestanti.
Kanisa la mwanzo lilitumia sana tafsiri ya Kigiriki (Septuagint), iliyokuwa na vitabu 46 vya Agano la Kale. Karne ya 16, wakati wa Reformation, Waprotestanti walifuata zaidi orodha ya maandiko ya Kiebrania (Hebrew Canon), iliyokuwa na vitabu 39 vya Agano la Kale. Ukijumlisha na vitabu 27 vya Agano Jipya unapata vitabu 66.
Vitabu hivyo 7 vilikuwa na utata, na utata huo ni sababu kila upande uliviangalia, ukavipokea au kuvikataa kwa savabu zake, mfano
- wayahudi walivikataa sababu Havikuwepo katika orodha ya Kiebrania iliyokubaliwa na Wayahudi wengi.
- Waprotestant walivikataa sababu Baadhi ya mafundisho yake yalionekana kutounga mkono baadhi ya mafundisho ya Waprotestanti.
- Wakatoliki walivikubali sababu waliona vilitumika na Kanisa la kwanza kwa karne nyingi, hivyo vina mamlaka ya kiroho.
Kuhusu swali la nani ana mamlaka ya kuamua kitabu kipi kiwe sehemu ya Biblia, hapo ndipo mjadala mkubwa ulipo:
Wakatoliki husema Kanisa, kupitia mapokeo yake na mabaraza ya Kanisa (Church Councils), lilitambua rasmi vitabu vya Biblia.
Waprotestanti husema Kanisa halikuumba Biblia, bali lilitambua tu vitabu ambavyo tayari vilikuwa vimevuviwa na Mungu (inspired writings).
Kwa hiyo, mjadala si kuhusu vitabu saba pekee, bali pia kuhusu chanxo cha mamulaka ya mwisho katika Ukristo: Kanisa au Maandiko.