Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

You are right,shule iliyokuwa inatoa upinzani kidoogo kwa tambaza wakati huo kwa mambo ya fujo ilikuwa kinondoni,ila kwa masomo ilikuwa Azania.Azania walikuwa wazuri kwa O level wakati Tambaza walikuwa wazuri kwa A level,na fujo za Tambaza ilikuwa ni O level Na zaidi form two na form one,na pia watu wa fujo hasa walikuwa wachache ila shule nzima na hasa O level walikuwa na umoja sana ndicho kilikuwa kinawabeba kwenye vurugu,ukimgusa tambaza mmoja ni kama umeigusa shule nzima,A level tambaza walikuwa watulivu sana na wengi wao walikuwa ni wale waliotoka Azania O level Ile Azania ya Mzee Kisamo na Mzee Meja ambayo ukichomekea shati unapewa adhabu,uniform ni kaptula ya kaki na shati bila kuchomekea,hapo one za point saba kwa O level ilikuwa kitu cha kawaida na Tambaza ya Kalumuna na baadae Mushi one za point 3 kwa A level ilikuwa kitu cha kawaida.Dah siku zimekwenda!
 
Lazima tulete nyodo. Watu hatujazaliwa nyie mko secondary leo tupo wote JF tunachati. Kuna sehemu mtakuwa mmekosea lazima naelewa nw kwanini wengi humu hamuipendi CCM.
Nahisi wewe hujitambui na una ulimbukeni flani,Jf siyo sehemu ya kuchat,ukitaka kuchat bakia whatsApp au face book,halafu kuwa na mtu kwenye jukwaa flani haimaanishi sasa mnalingana na mtu huyo kwa kila kitu,mfano unaweza kukaa jukwaa moja pale uwanja wa Taifa na waziri mkuu mkiangalia mpira haimaanishi sasa wewe na waziri mkuu mnalingana,likewise humu JF kuna watu wa mbavu mbalimbali humu kama mawaziri,maprof nk usije ukajipa moyo mnalingana,ingawa hata sie wachimba chumvi pia tumo,uzuri wa JF status ya mtu sio issue,tunajali mawazo yako,na ndio mana slogan ni HOME OF GREAT THINKER......
 
Mnasumbuka kumjibu wa nini ? Wakati mambo hayo yanatokea yeye alikuwa anachunga ngombe kijijini kwao Biharamulo
 
 
Daahh wengi humu jg hawamjui puza na jamaa jina alilipata kwny tshrt ni kweli?
 
Nilikuwa hostel ya Azania miaka ya 91-93 ... A level.... wakati huo tulikuwa wachache sana A level ila O level wengi sana.....na Azania walikuwa wazuri kwenye mpira... ilikuwa Tambaza wakija cheza mechi pale Azania na wakafungwa, ni lazima tuhame hosteli... kama huna ndugu mjini inabidi ukajibanze kwao mshikaji... vijamaa vifupi hivi havijachomekea mashati... vingi lakini vibabe mbaya....kituo cha fire ndo makutano yao kama konda fulani alileta taabu asubuhi... long time
 
Mimi ninachokumbuka kuhusu Tambaza ni tishio la kuchoma moto shule zote za Dar, sijui kama lilikuwa tishio la kweli ama la, lakini shule niliyokuwa nasoma enzi hizo (S/Msingi) waliletwa askari polisi wawili wakiwa na bunduki zao. Nikasema kweli Tambaza kiboko.
 
Enzi za Puza Tambaza ndio ilikuwa Tambaza.RIP PPuza ulikuwa mtemi.
 
Mangosongo,funza,obwago,miarji,matutu nk,walitukuta Nsumba.jamaa wskipenda sana misosiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…