Kwanini Rais Samia anatumia ndege za ATCL kwa safari zake hata fupi badala ya ndege ya Rais?

Nadhani kuliko ipaki iwe mazalia ya Popo na viumbe wengine ni bora ipashwe pashwe

Hapo kwenye gharama za kuiendesha hio hesabu itiwe kwenye Hasara ya Mwendazake
Kama ni hivyo si ile ya Raisi ndio itapaki?

Kama ni kuzipasha moto, wapunguze nauli iwe kama ya Fast Jet, zitatembea sana
 
Si anaitangaza ATCL,
tena kipindi hiki safari zimepungua ni muhim kweli ikulu waichukue wazunguke nayo kuitangaza ATCL
Kwa hiyo ni sawa serikali kuzitumia bila busara?

Hata Ethiopian Airways, Rwandair, ni ndege za serikali.
 
Hao Malawi wana viwanja vikubwa tu, kama kile cha Blantyre na Lilongwe vya kuweza kutua ndege kubwa tu, na hata Air Malawi wana Airbus na Boeing 747 na Bombadier za kutosha zinazofanya safari zake ndani na nje ya nchi...

Hivi Malawi wana uwanja wa ndege kubwa kama airbus yetu kutua? Mi nadhani unatua kwanza Botswana au namibia halafu unavuka na gari Malawi. Mimi nilijua ni hizi cassena ndege za umwagiliaji wa pembejeo ndo zinaweza kutua Malawi.

barafu
J
 
Acha mama angalau aipashe moto Airbus yetu vinginevyo inge-park tu airport hatimaye ipate kutu!
Si watupe basi tuifaidi angalau kwa laki Dar Mwanza kama tatizo ni kuipasha moto!

Hata wakisema hizi ni safari za ilani ya uchaguzi ya CCM hatuna tatizo, tutapanda tu, "Wahi Mwanza na ATCL kwa laki moja!"
 
ATCL haina ndege, ndege ni za Serikali ambazo zinakodishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…