Kwanini Rais Samia anatumia ndege za ATCL kwa safari zake hata fupi badala ya ndege ya Rais?

Hapana,ile ndege ya rais gulfstream,gharama zake ni kubwa sana,ni bora mara mia atumie airbus

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hao Malawi wana viwanja vikubwa tu, kama kile cha Blantyre na Lilongwe vya kuweza kutua ndege kubwa tu, na hata Air Malawi wana Airbus na Boeing 747 na Bombadier za kutosha zinazofanya safari zake ndani na nje ya nchi...


J
Malawi ipi yenye 747? Hawa si ni maskini wa kutupwa
 
Nadhani moja ni kibiashara zaidi (economic diplomacy) kuitangaza ATCL,kuitangaza Tanzania na vivutio vya kiutalii..

Pili 5H-ONE ni ndogo sana kiuwezo kubeba ujumbe alioongozana nao kulinganisha na hii 5H-TCH..

Mengine ya ziada ni social distancing kuepuka uviko 19 nadhani..
 
Na report ya CAG haitakaa izungumzie hasara iliyotengenezwa na ATCL mpaka Bimkubwa akitoka madarakani.

Hizi routes za Dar-Dom nazo anapigia hilo hilo pipa.
 

Mimi sioni kama ni tatizo sana ilimradi kusiwe na ndege zime park kama zote zinafanya kazi haina shida. Vilevile inawezekana anasafiri na watu wengine mfano wafanyabiashara wa Tanzania
 
Asante ndugu naomba ubia wa huu uzi wako. Yaani umetoa nyongo kwa hiki kinanikera. Ndege kubwa kwa safari fupi ni gharama. Na kama wanajaa ujumbe watu 120 ni ubadhirifu. Wakijidai wanakodisha atc inalipwa kibiashara pia ni ubadhirifu.
Magufuli alijitahidi kuendesha serikali kama ceo wa kampuni. Wakati wote kuona faida na hasara. Kwa ajili hiyo akachukiwa sana na wapigaji.
 
Am sorry...I meant B737's... pamoja na kuwaita maskini shirika lako la ndege wanaoperate kwenye route nyingi jointly na Ethiopian Airlines kuendelea kusurvive ktk kipindi hiki kigumu....
Malawi ipi yenye 747? Hawa si ni maskini wa kutupwa
 
Huyu ndiye Big Brother wa SADDC, Mkuu wa SADC, wote wanamwangalia yeye. Tungewachekea wasaliti wetu angeenda na Kenya Airways.
 
Hiyo hoja ni ya msingi sana. Kupeperusha hilo dude ni gharama kubwa sana!
Na sisi ndio walipa kodi
Sasa mnataka atembee na msafara wa magari mengi ka mwendazake hyo ndio hasara ila ndege ninafuu, pia hyo Airbus haichakai kuliko kukaa tu chini bila kutumika mda mrefu
 
Dah watu mkikosa vitu vya msingi huwa mna hoji hata mambo yasiyoeleweka, ama kweli binadamu hatuna jema
Dah. Mkuu na wewe unasema matumizi ya ndege za ATC siyo ya msingi? Ni ya msingi kweli kweli. Safari moja ya ndege inatumia gharama kubwa. Halafu kumbuka hizi ndege zimenunuliwa kwa ajili ya shirika la ndege. Ina maana hazifanyi kazi? Kama zinafanya, inapotumika kumbeba rais abiria ambao wamekata tiketi na walipangiwa kusafiri nayo wanasafiri na nini? Na kingine: rais anayo ndege yake iliyonunuliwa kwa ajili yake. Kwa nini haitumii? Na pia: Kama Magufuli asingenunua hizo ndege angesafiria nini? Kumbuka hizi ndege zimegharimu fedha nyingi za wananchi hivyo ni lazima wahoji matumizi yake.
 
Sasa mnataka atembee na msafara wa magari mengi ka mwendazake hyo ndio hasara ila ndege ninafuu, pia hyo Airbus haichakai kuliko kukaa tu chini bila kutumika mda mrefu
Ndiyo kusema walinunua ili kuja kukaa chini tu? Haisafirishi abiria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…