Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Nauliza hili swali sababu kama wananchi tunataka kufahamu ukweli juu ya hili janga. Tunataka waziri wa afya, au msemaji mkuu wa serikali kila siku awe anatoa taarifa zilizo rasmi.

Mbona nchi za wenzetu ambazo zimekumbwa na hili janga kila siku lazima watoe taarifa rasmi kuhusu maambukizi,waliopona na waliofariki.

Au hapa Tanzania ndio kusema mambo yanaenda kimya kimya? Maana watu kila kukicha ni kutishwa tu na habari ambazo sio rasmi.

Mara tunasikia watu wanazikwa usiku, mara tunasikia rubani wa Tanapa alikufa kwa Covid-19,mara kuna maiti imekaa siku mbili mtaa wa Lumumba. Lakini hatusikii serikali ikikanusha wala kuwaambia ukweli wananchi.

Kwa jinsi hili janga lilivyo serious ilipaswa waziri wa afya au msemaji wa serikali angekuwa kila siku anakaa na wanahabari na kutoa takwimu na taarifa rasmi.

Lakini mtu mmoja ambae anamiliki jarida la mtandaoni (Pambazuka) anapoachiwa awe anaandika habari za uongo kuwa watu wanazikwa usiku kimya kimya ni jambo baya maana watu hofu inazidi kwa wananchi.

Inatoka habari kuwa madereva wanne watanzania wamepimwa huko Uganda na kukutwa na ugonjwa wa Covid-19. Hofu inazidi kuwa kubwa kwa wananchi.
Hivyo ili kuondoa hofu lazima mtupatie taarifa rasmi,kama nchi tupo wapi?

Maambukizi ni mengi? Yamepungua? Na wanaopona ni kiasi gani? Hii iwe kila siku na mruhusu kupigwa maswali na waandishi wa habari kama Andrew Cuomo gavana wa New York anavyofanya kila siku. Maana hatulali ni hofu tu.
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787]. Akili zitakurudi tu. Wakisema watu mnadhani wanamsakama wa nyumbani.

Odhis *
 
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787]. Akili zitakurudi tu. Wakisema watu mnadhani wanamsakama wa nyumbani.

Odhis *
Jaduong hili ni janga la kitaifa. Na kila hoja ambayo huwa naiweka humu ni kwa manufaa ya taifa letu. Weka siasa kando.
 
Ulijuliza kikao cha Mzee kuzungumzia Corona walialikwa wabeba bunduki na si wataalamu wa afya ?!.

Think big onghwise .

Odhis *
Kuna watu wengi walihudhuria pale, una uhakika wote ni wabeba bunduki?

Jaduong Acha ushabiki wa kisiasa.Au sababu alikuwepo Igp,Dg waTiss na Cdf ukajua hakuna watalaamu wa afya?
 
Nchi iliyozoea kupika data utaijua tu. Sasa data za korona hazipikiki kirahisi ni lazima watafute wapishi wazuri ndio wazipike na wakisha pika ndio unasomewa.

Ukiona umesomewa watu 50 basi wewe ongeza wengine 40 ili upate data kamili ambayo haija pikwa.

BTW mzee yuko chattle bado?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daily briefing ni Muhimu sana kama Wananchi tujue tulipo na tunakoenda ila pia Tupate statistics halisi ili tujue ukubwa wa tatizo na watu wazidi kutake tahadhari zaidi.

Nafikiri pia kuna Task force kama sijakosea PM ndio ana lead the team, Tungeomba basi walau kila jioni wapate live coverage na watuhabarishe wana Taifa hili.
 
Back
Top Bottom