Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Nimesikitishwa sana na tabia ya baadhi ya watanzania kuonyesha uwezo mkubwa wa kutabiri vifo, kuvifuatilia vitokepo na kusema sababu ni UVIKO-19 na kadhalika.
Ni juzi tu tumeondokewa na aliekuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kwandikwa.
Haijaelezwa kinaga ubaga kuhusu kifo chake lakini huko Twitter imeelezwa kuwa sababu ya kifo chake ni UVIKO-19
Marehemu Elias Kwandikwa amekaa wizara ya ulinzi kwa muda akimsaidia raisi wa sasa wa Zanzibara Dr Hussein Mwinyi ambae ndie alikuwa waziri wa Ulinzi.
Lakini kinachonitatiza ni jinsi vifo vya baadhi ya hawa watu, historia zao na jinsi watabiri wanavyoweza kusema kuwa "akitoka huyu bado yule" bila woga wala wasiwasi.
Kwa mfano marehemu Kwandikwa hadi kifo chake alikuwa akishughulikia suala la magaidi wa Msumbiji kuhakikisha hawaingii tena nchini kupitia mikoa ya kusini khasa Wilaya ya Kibiti.
Lakini baada ya kufariki mara tu mtu asema "na bado mpaka wote waishe".
Je, ni nguvu gani iliyopo nyuma ya matamko kama haya?
Katika nchi ambazo hazizingatii umakini katika kudhibiti taarifa na kuzushughulia ipasavyo bila kutoa vitisho, makaripio na matamko kupitia msemaji wa serikali ni Tanzania.
Ila haiwezekani watu wakawa huru kabisa kutamka mitandaoni kwamba anaefuata baada ya kufa huyu ni CFD au IGP au KBD na kadhalika na wakaachiwa tu hivihivi kuwepesi.
Napenda kutoa ujumbe kwa kiota akaacho ndege wetu mzuri wa Tai.
Hiki kiota ni moja ya viota vichache ambavyo vinaaminika.
Ingawa nasikia mbawa moja imejeruhiwa lakini nina matumaini utapona na utaweza kuruka sawasawa.
Nina matumaini siku si nyingi utaweza kuruka juu zaid na zaidi kuona kila kitu.
Kwa sasa tulia tu upone na na nina uhakika unaona baadhi na wale sungura walo chini wakuona kwa mbali ukiwa huweza kushuka kwa kasi.