Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Ni kweli kabisa mkuu, Mimi ni mmoja wapo kwenye ile posti nilijaribu kutuma comment yenye content ya utani ilikuwa inasomeka hivi najinukuu hapa:.." Best airlines ni kwa ulaya na Bara Asia Africa tuna Air Sumbawanga".. mwisho wa kunukuu....,,Sasa likes na comments nilizopata ni nyingi sana tofauti na ninapo comment kitu cha msingi na mawazo yakinifu katika habari nyinginezo huwa hamna likes hata moja...hii ina thibitisha wazi kwamba watanzania wengi tunapenda utani na kufagilia Mambo ya kijinga kuliko vitu vya msingi.Hata Facebook kwenye page za huko ukicomment kitu au habari kwa kutoa madini hupati support kubwa ngoja ucomment upumbavu sasa wajinga wenzio wanakuja kulike kwa nguvu sana kama mchwa,juzi Millard Ayo kapost mashirika ya ndege bora duniani cha kushangaza kuna watu kwenye post ile walikuwa wanatoa madini hatari hawakupata hata like au comment ila wapumbavu walioandika upuuzi like walizopata aisee nkasema Tz ujinga ni mwingi sana
