Kwanini Tanzania ya sasa Watu wa hovyo kijamii na matukio ya hovyo ndiyo yanashabkiwa na 'Kutrendi' sana?

Kwanini Tanzania ya sasa Watu wa hovyo kijamii na matukio ya hovyo ndiyo yanashabkiwa na 'Kutrendi' sana?

Kutrend - Kiswahili
Kushabikiwa - kiingereza

Yote maneno ni Sawa huwezi kutrend bila kushabikiwa

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
kutrend ni Kuvuma
kushabikiwa ni kupata ufuasi au kuungwa mkono

kuna tofauti hapo kuvuma kitu chochote kiwe kibaya au kizuri,kinaweza kuvuma, kuwa gumzo

Kushabikiwa lazima kitu kiwe na wapenzi!!..wanaokikubali
 
Bashite aliwahi kukosoa umaarufu wa hovyo wa pierre likwidi akaishia kudhihakiwa na kuoga matusi
...Hivi kweli Pierre Likwidi aliishia Wapi? Jamaa alinunuliwa Hata Tiketi ya Kwenda Kuishagilia Taifa Stars!...
 
Kwa mfano Mtu (Bondia) wa hovyo na very Unprofessional Karim Mandonga (ambaye hata Kupigana hajui) na ana Upuuzi mwingi anashabikiwa na kusifiwa kila Kona huku akitrendi ila aliyempiga na anayejua Ngumi Bondia Kaoneka haimbwi, asifiwi, hashabikiwi na hata 'hatrendi' pia hadi Kuonekana ni Mshamba fulani hivi.

Naanza sasa kuamini kuwa kuna shida ndani ya Vichwa vya Watanzania wengi kama tunasapoti Mambo Hasi na Upuuzi mwingi wa Kimatukio katika Jamii yetu hii tukidharauliwa na kuitwa Majuha (Fools) tutakuwa tunakosewa Adabu na wanaotuita hivyo?

Inasikitisha mno tu na haingii Akilini!
Weka na ekizampo bazi...
 
Kwani nchi nyingine watu design hii hawapati uungwaji mkono mkubwa? Kama yule mcheza mpira airways Speed aliyekuwa clearly offside. Week hii ametrend sana huko duniani alipocheza mechi ya hisani
 
Ujinga na upumbavu upo kwa kiasi kikubwa sana katika jamii yetu, wengi wetu ni wajinga tulio pitiliza.

Katika mkusanyiko wowote wa vijana hakuna hoja hata moja inayo jadiliwa hata kwa bahati mbaya.

Piya hata kwenye mitandao hii ya kijamii nayo kwa kiasi chake inakusanya watu haswa vijana na baadhi ya watu wazima, cheki maudhui yanayojadiliwa katika mijadala mbalimbali, ni ujinga ulio vuka ujinga wenyewe.

Njoo hata hapa jamii forum ona mijadala inayojadiliwa kwa wingi, ni ile isio na tija, mada za mapenzi, ngono, burudani na zisizo na kichwa wala miguu ndio zinapokelewa kwa bashasha sana, ona hata mada ya sekfika sijui utakuta mtu yupo kule tokea mapambazuko ya jua mpaka usiku wa manane kazi kuomba picha na kutuma picha, mara licha ya kucha mara picha nywele na ujinga mwingi usio elezeka.

Ona mada za kufumaniwa na kufumania, ona uzi wa kula tunda kimasiara na nyinginezo nyingi za kijinga na kuumiza wengine kihisia ndio zinapendwa mno!

Twende kwenye vituo vyetu vya redio, hata ile redio ya taifa TBC ni ujinga mtupu, vituo vya redio kila kona, maudhui yake sasa!
Michezo, burudani, matamasha, kamari ,miziki, hadithi za kutunga zisizo na kichwa wala miguu, tokea asubuhi mpaka asubuhi, bado vituo vya redio vya kidini ni miujiza face tu ndio ina trend.

Nenda facebook, nenda instagram,nenda tweeter, tik tok sijui, ni ujinga mtupu.

Nenda hata bungeni ni ujinga mtupu!

Wakati huo wigo wa umaskini unazidi kua mpana

Izingatiwe pia wigo wa kupatikana kwa elimu umekua mkubwa pia.
 
kutrend ni Kuvuma
kushabikiwa ni kupata ufuasi au kuungwa mkono

kuna tofauti hapo kuvuma kitu chochote kiwe kibaya au kizuri,kinaweza kuvuma, kuwa gumzo

Kushabikiwa lazima kitu kiwe na wapenzi!!..wanaokikubali
Hana Akili huyo Ndugu pamoja na hao waliompa Likes hapo. Anadhani MINOCYCLINE ' Gifted Intellectually, Knowledgeable, Challenger and Well Informed Person' nimekurupuka tu Kuyaandika / Kuyatumia haya ( hayo ) maneno Mawili.
 
Tengeneza pesa kwa wajinga na ukishindwa jua wewe mjinga tu....

Mandonga na genge lake wako very smart

Pesa ziko kwa wajinga shida ni kuvuta pesa zao ki urahisi ...ukiona mtu ameliweza Hilo jua Yuko very smart
 
...Hivi kweli Pierce Likeidi aliishia Wapi? Jamaa alinunuliwa Hata Tiketi ya Kwenda Kuishagilia Taifa Stars!...
Ndiyo ujue kama Taifa tulikuwa na huenda bado ni Wapumbavu sana tu Ndugu.
 
Kwani nchi nyingine watu design hii hawapati uungwaji mkono mkubwa? Kama yule mcheza mpira airways Speed aliyekuwa clearly offside. Week hii ametrend sana huko duniani alipocheza mechi ya hisani
Kwahiyo Mpumbavu akitrendi Ulaya au Marekani ni justification kuwa lazima na huku Kwetu Afrika ( hasa Tanzania ) akitokea wa Kufanana nae basi nasi tumuunge mkono?

Huna Akili.
 
Ujinga na upumbavu upo kwa kiasi kikubwa sana katika jamii yetu, wengi wetu ni wajinga tulio pitiliza.

Katika mkusanyiko wowote wa vijana hakuna hoja hata moja inayo jadiliwa hata kwa bahati mbaya.

Piya hata kwenye mitandao hii ya kijamii nayo kwa kiasi chake inakusanya watu haswa vijana na baadhi ya watu wazima, cheki maudhui yanayojadiliwa katika mijadala mbalimbali, ni ujinga ulio vuka ujinga wenyewe.

Njoo hata hapa jamii forum ona mijadala inayojadiliwa kwa wingi, ni ile isio na tija, mada za mapenzi, ngono, burudani na zisizo na kichwa wala miguu ndio zinapokelewa kwa bashasha sana, ona hata mada ya sekfika sijui utakuta mtu yupo kule tokea mapambazuko ya jua mpaka usiku wa manane kazi kuomba picha na kutuma picha, mara licha ya kucha mara picha nywele na ujinga mwingi usio elezeka.

Ona mada za kufumaniwa na kufumania, ona uzi wa kula tunda kimasiara na nyinginezo nyingi za kijinga na kuumiza wengine kihisia ndio zinapendwa mno!

Twende kwenye vituo vyetu vya redio, hata ile redio ya taifa TBC ni ujinga mtupu, vituo vya redio kila kona, maudhui yake sasa!
Michezo, burudani, matamasha, kamari ,miziki, hadithi za kutunga zisizo na kichwa wala miguu, tokea asubuhi mpaka asubuhi, bado vituo vya redio vya kidini ni miujiza face tu ndio ina trend.

Nenda facebook, nenda instagram,nenda tweeter, tik tok sijui, ni ujinga mtupu.

Nenda hata bungeni ni ujinga mtupu!

Wakati huo wigo wa umaskini unazidi kua mpana

Izingatiwe pia wigo wa kupatikana kwa elimu umekua mkubwa pia.
What do you think could be the Solution?
 
Tengeneza pesa kwa wajinga na ukishindwa jua wewe mjinga tu....

Mandonga na genge lake wako very smart

Pesa ziko kwa wajinga shida ni kuvuta pesa zao ki urahisi ...ukiona mtu ameliweza Hilo jua Yuko very smart
I agree with you 100%
 
Ni heri hata mandonga unaweza sema ni comedian anayetumia low intelligence ya watz kupiga pesa, vipi wahuni na makahaba wa bongo Muvi na bongo fleva kufanywa kioo cha jamii? Halafu utakuta maelfu ya watu eti wamegawanyika mara timu wema, mara timu Zari, mara timu Mobeto!! Unataka ushahidi gani kujua tumekuwa taifa la wajinga?

Kama unadhani ni huko tu, basi hujafanya uchunguzi wa kutosha. Angalia thread nyingi zinazoanzishwa humu. Zenye wachangiaji wengi ni zile zinazoshabikia mambo ya aibu. Sasa hai ndio vijana, nguvu kazi ya taifa, wazazi wajao, unatarajia tuna taifa la namna gani?
 
Watu wengi sana nchi hii wana stress za kufa mtu, so wakipata kitu cha kuwafurahisha/kujifariji kidogo inawasaidia kurelease stress zao. Kwa mfano issue ya waziri kushindwa kufafanua kwa ufasaha TRAT na TRAB, wajinga walivyoshabikia utadhani labda inawapunguzia ukali wa maisha
 
Mtaje huyo aliyetugeuza mazuzu,
Hili nalo ni swali la kizuzu, wenzetu wamemudu kuigonganisha spacecraft na astronoid, jaribio la kwanza kabisa kufanywa in a modern science, wewe endelea kuuliza viswali vya kizuzu na kugombonia vijiajira ushwara
 
Mleta mada uko sahihi.

Kuna wimbi kubwa sana la wajinga haswa vijana (15 - 45) ambalo limeibuka kama nzige kwa miaka ya karibuni.
Limeharibu hata lugha yetu adhimu ya kiswahili kwa uandishi wao wa kivivu na wa hovyo. (ivi, cku, apana, xhule na upuuzi mwingine kama huo).
Ni kundi lililoanza kuonekana huko FB likasambaa na mwisho limeenea kila mahali sasa.

Hapa JF enzi hizo kulikuwa na watu makini wenye kutoa mada na hoja za moto ila baada ya hili kundi kuvamia huku, mambo yamebadilika mada zimekuwa ni za kupalilia ngono na mambo mengine ya kijinga. Imebidi watu wengi makini wakimbie na waliobaki wawe wapole.
Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom