Ujinga na upumbavu upo kwa kiasi kikubwa sana katika jamii yetu, wengi wetu ni wajinga tulio pitiliza.
Katika mkusanyiko wowote wa vijana hakuna hoja hata moja inayo jadiliwa hata kwa bahati mbaya.
Piya hata kwenye mitandao hii ya kijamii nayo kwa kiasi chake inakusanya watu haswa vijana na baadhi ya watu wazima, cheki maudhui yanayojadiliwa katika mijadala mbalimbali, ni ujinga ulio vuka ujinga wenyewe.
Njoo hata hapa jamii forum ona mijadala inayojadiliwa kwa wingi, ni ile isio na tija, mada za mapenzi, ngono, burudani na zisizo na kichwa wala miguu ndio zinapokelewa kwa bashasha sana, ona hata mada ya sekfika sijui utakuta mtu yupo kule tokea mapambazuko ya jua mpaka usiku wa manane kazi kuomba picha na kutuma picha, mara licha ya kucha mara picha nywele na ujinga mwingi usio elezeka.
Ona mada za kufumaniwa na kufumania, ona uzi wa kula tunda kimasiara na nyinginezo nyingi za kijinga na kuumiza wengine kihisia ndio zinapendwa mno!
Twende kwenye vituo vyetu vya redio, hata ile redio ya taifa TBC ni ujinga mtupu, vituo vya redio kila kona, maudhui yake sasa!
Michezo, burudani, matamasha, kamari ,miziki, hadithi za kutunga zisizo na kichwa wala miguu, tokea asubuhi mpaka asubuhi, bado vituo vya redio vya kidini ni miujiza face tu ndio ina trend.
Nenda facebook, nenda instagram,nenda tweeter, tik tok sijui, ni ujinga mtupu.
Nenda hata bungeni ni ujinga mtupu!
Wakati huo wigo wa umaskini unazidi kua mpana
Izingatiwe pia wigo wa kupatikana kwa elimu umekua mkubwa pia.