Kwanini TPDC wanalipwa mshahara mkubwa kiasi hiki?

Wenzenu wakati wanasoma vitu vigumu kama petroleum engineering e.tc mlikuwa mnawasema vibaya ati wanasoma kama wametumwa na kijiji.

Leo wanapokea pesa ndefu mnawaonea dongo
Angalau na madaktari basi wangepewa katika viwango hivyo.

Na hao waliosoma madegree hayo sawa, lakini madereva wamesoma maengineering gani nao mishahara yao ni ya sayari ya mbali?

Kuna kipindi niliwahi kumtania mmoja wa wafanyakazi nikamwambia bora nije kuomba udereva huko kuliko huku serikalini na cheo hichi ambacho mshahara wake duh!
 
Nimeamini leo waswahili hatupendani kumbe ukianza kazi na mtu akiona mafanikio yako anapata kijiba cha roho
 
Sasa japo.kuna siri nyuma huenda iyo prado kaivuta kwa mkopo
 
Aisee si afadhali na mimi unipatie connection hapa na kadiploma kwangu. Huko itakuwa kuna afadhali kwa kweli.
 
Mimi ninadhani hoja ingekuwa kuiomba serikali iboreshe na maeneo mengine lakini siungi mkono kutaka na wengine washushwe.
 
Acha ujinga wewe kwa kuleta taarifa ya uongo hapa jukwaani. TPDC kwa mtumishi anae anza kazi hapati kiasi hicho cha mshahara ni uongo na isitoshe TPDC wanalipwa mshahara moja kwa moja kutoka Hazina kwahiyo tafuta taarifa utajua ukweli,lakini acha kupotosha jamii. JamiiForums futeni hii thread huu ni uongo
 
dismas fuko mzee niliishi naye mtaa mmojaa ni mtu wa dini sanaa na mkalimu sana.
 
We inakuuma nn..tulia tulia kwenye kumbi za kimataifa hahaha mpwayungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…