Wote tunafahamu Mwenge wa Uhuru ni moja ya tunu za Taifa letu. Kwa kuwepo kwa mbio za mwenge nchi nzima siyo tu ni utaratibu, lakini ni hamasa kwa jamii kujenga uzalendo.
Kwa vile tayari tuna janga la Covid-19 ni vyema tukazingatia namna pendekezwa hasa kuepuka mikusanyiko mikubwa. Ukiangalia namna mbio za mwenge wetu zilivyo na jinsi umati mkubwa wa watu unavyokusanyika kuulaki ni hatari tupu. Ni asilimia ndogo sana unawakuta wamevaa barakoa! Nimebahatika kuwa maeneo fulani Mkoani Mwanza na kushuhudia haya niliyoyaeleza.
Na omba viongozi husika walione hili kuwa ni janga. Kimsingi sipingi mbio za mwenge, ila tumchukue tahadhari. Kwani, ni lazima sana kila unapolala kulundika watu mikesha, na vivyo hivyo uzinduzi wa miradi yetu, siyo lazima wahudhurie watu wengi.